Nina Tshs. 45 milioni, Nifanye biashara gani?

Nina Tshs. 45 milioni, Nifanye biashara gani?

Nyaka-One

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2013
Posts
4,730
Reaction score
6,736
Wana JF,

Poleni na majukumu mliyonayo.

Ni kwamba mimi ninaishi Dar es Salaam. Umbali kutoka yalipo makazi yangu hadi city centre ni wastani wa kilometer 18. Nimeajiriwa sehemu ambako kwa maisha yetu ya kitanzania nadiriki kusema kwamba mshahara si mbaya kivile. Kutokana na ajira hii niliyonayo nimeweza kujenga nyumba ya kisasa kiasi fulani na pia kufungua miradi kadhaa hapa hapa jijini.Kwa kiasi kikubwa hii miradi inasimamiwa na mke wangu akisaidiwa na watu wengine tuliowaajiri.

Sasa kutokana na faida iliyopatikana kutokana na miradi hii ambayo imedumu kwa muda wa miaka minne napia saving yangu inayotokana na ajira yangu tuliweza kugawa hiyo faida katika mafungu makubwa mawili. Fungu la kwanza ikiwa ni kukuza mtaji kwa kila mradi uliopo na fungu la pili likiwa ni kufungua mradi mwingine mpya ambapo tuliutengea jumla ya Tshs. 45,000,000/=. Mradi huo mpya tulilenga kuufanyia nyumbani ili kuwa na usimamizi wa karibu (kwa maana ya kuuona kila siku) lakini usiohitaji uwepo wa mimi na mke wangu muda wote (kati ya saa moja na nusu asubuhi na saa kumi jioni)

Baada ya kutenga kiasi hicho chapesa tulifanya investment portfolio analysis na tukaona kwamba tungeweza kuwekeza pesa hiyo kwenye mradi wa ufugaji wa kuku wa kisasa wa mayai (2,000),kuku wa kienyeji (2,000) na pia kanga (1,000) na pia kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya ufugaji huo kama incubator, generator, n.k. Maamuzi ya kufanya mradi huo pamoja na factors zingine yalizingatia taarifa tulizokuwa nazo kuhusu faida nzuri ya ufugaji huo na pia eneo tulilo nalo nyumbani ambalo ni mita za mraba 2,600 na liko liko fenced.

Sasa taarifa nilizo nazo hivi karibuni soko la mazao ya ufugaji huu hasa kwa upande wa mayai ya kuku wa kisasa siyo zuri kutokana na uingizwaji wa mayai kutoka nchi jirani ambayo uuzwa kwa bei ya chini ukilinganisha na bei ya wafugaji wa hapa Dar. Pia gharama za ufugaji wa hao kuku na kanga kuonekana kuwa kubwa kulinganisha na hali ya soko kwa sasa. Hali hii imetufanya tusite kuwekeza kwenye mradi huu wa ufugaji (kwa ujumla wake) kwa sasa ili kuepuka hasara ambayo inaonekana kuwa wazi kwa macho ya haraka haraka.

Sasa ndugu zangu nikaona si vibaya kuja hapa JF ili ikiwezekana basi kupata ushauri wa mawazo mbadala ambayo tutayafanyia kazi na kuweza kuwekeza kiasi hicho cha pesa lakini wakatiwa kutoa ushauri naomba mzingatie kwamba mradi huo mpya unatakiwa ufanyikie katika eneo la nyumbani ninapoishi.

Natanguliza shukurani zangu kwenu wana JF.
 
Nakushauri ufuge kanga pia na Kwale bila kusahau mbuni pia bundi! maana mayai yao kipindi hiki cha uchaguzi yana dili sana kwa wagombea uraisi,ubunge na udiwani. Ni hayo tu.
 
nunua viwanja maeneo mbali mbali, viwanja vya kuanziav400msq bei isizidi 8m after 1year utauza si chini ya kuanzia 14m,

au tuingie mkataba nipe mimi hizo 45m ntakulipa 1m kila mwezi na mtaji wako utabaki kama ulivyo. mkataba miaka 2
 
Ahsante wadau kwa michango ya mawazo mnayoendelea kuitoa. Ila sehemu ya mawazo aliyotoa Ng'wanapagi imenichekesha. Yaani ushauri wa kufuga bundi. Sasa uchaguzi ukiisha na soko la hayo mayai ya bundi si litakuwa halipo tena hadi uchaguzi mwingine? Bundi wenyewe wanatisha na kutokana na bundi kuhusishwa sana na imani za kishirikina ufugaji wake utanijengea mahusiano mabaya na jamii inayonizunguka na pengine hata kupelekea kufukuza wateja wangu katika biashara zangu zingine.
 
wazo lako LA mwanzo LA kwenye ufugaji ni zuri sana ...... ukweli wa biashara hii ni kwamba huwa kuna low and high season, peak na pia kuna shackles mbalimbali ambazo ni risks kama biashara Nyingine ..... mfano ni mfumuko na uwingi Wa bidhaa sokoni ..... kama kweli unataka biashara haya so mambo ya kuogopa au labda we we unataka ufanye shughuli kwa maximum profit all the year .... hiyo haipo kabisa hata books of accounts zitakataa

kubali kukutana na challenges especially za competitor ..... unaweza ukapack Mayai yako ya kuku Wa kienyeji kwenye plastic trays za 12 eggs na ukauza kwa being ile ile .... tayari umeshakua tofauti na wengine

be creative on the same type of business others do, add value ... design a smooth and efficient distribution
 
Tumia millioni tano
Kupata uwanja wa wazi pale chamanz karibu na uwanja wa azam,chimba kisima na funga pampu..weka vijana fungua car wash..utatoka soon

Daah. Sema niko huku porini kunakonipa riziki yangu ya kila siku lakini ningekua Dar hili wazo ningeliiba na ndani ya wiki mbili nakuhakikishia ningekuwa nishaanza biashara. Wazo zuri sana.
 
habari

kwanza hongera kwa mtaji huo
nina wazo kwako huku mbeya kuna sehemu moja ina fursa ya biashara biashara yenywe ni mgahawa kwani sehemu hii ina chuo cha afya pia ina hospital ya wilaya lakini kuna upungufu wa mgahawa ambao upo standard yan kuna migahawa miwili tu ambayo nayo ni mchafu haipo standard wagonjwa na wanafunz, madoctor na wafanyakazi wote kwa ujumla wanapata shida kuusu chakula

hivyo unaweza ukajenga mgahawa ambao upo standard na ukawa unakuingizia zaid ya laki na nusu kwa cku ambapo ukipga hesabu kwa. mwez ni zaid ya m3 kwa kila mwez


ukiona linakufaa chek me 0765650028 piga au whatsaap
 
Bulldog na Primking: Nitafanyia kazi ushauri wenu kwa kufuatilia pale DSE.

Bwana Mapesa: You have a splendid idea. Nitalifanyia kazi wazo lako. Je una hint yoyote kuhusu minimum package ya vifaa vinavyotakiwa kwa ajili ya car wash na gharama zake (kwa hiyo minimum package)?

Zumbemkuu: ushauri wa kununua viwanja pia naupokea. Ahsante.

Bluetooth: Pia nakushukuru. Bado hatujakatia tamaa wazo tulilokuwa nalo awali kuhusu ufugaji. Ni kwa sababu tu nimeona ni busara kupata mawazo mbadala.

Delzzy: Wazo lako la kufungua decent restaurant huko Mbeya kimsingi siyo baya. Tatizo ninalo liona ni management yake ukizingatia kuwa mimi makazi yangu ni huku Dar na itakuwa shida kusimamia biashara ya mgahawa kwa kutumia remote. Ila ahsante sana kwa wazo lako.

Nawashukuru sana nyote mliokwisha toa mawazo yenu na mnaoendelea kutafakari nini cha kunishauri kuhusu ombi langu.
 
Back
Top Bottom