Nina uhusiano na mke wa mtu. Natamani kumuacha lakini inakuwa ngumu

Bro hii ni hatari! Unajua si halali kwako na ujue kabisa kuna watu watakuwa wameshamwambia mumewe sababu hakuna mahusiano ya namna hii yanayodumu kwa siri kwa muda mrefu!

Huyo mama mtu ameshamharibu mwanaye na Huyo binti hana maadili kabisa, asije siku akakuletea aibu ukashangaa!

Najua kwa nini inakushinda kutoka huko, kwanza nguvu ya uharibifu imewameza Wote wawili na kwa sababu hamna haki nguvu hiyo inawamiliki na mwisho wake ni mbaya kuliko unavyotegemea! Kama umeamua kweli kumuacha lazima uwe na sababu za msingi sana zinazoendana na maadili ya ndoa na si kwa sababu eti unamhurumia mumewe.

Kuna mambo mengi nayaona lkn ujue umetumbukia kwenye shimo, kuna impact kubwa sana nyuma ya jambo hili huenda hata usijue. Nadhani bwana Mshana akichangia hapa anaweza kukupa kwa haraka zaidi madhara ya ndani, sababu haya ya nje kila mtu anayajua nawe mwenyewe unayajua ndo maana unataka kutoka
 
Maisha ni machaguo na wewe umechagua hivi ulivyosimulia unafanya
Always there is a choice
 
Mkuu mimi siwezi kuongea sana, wengi wameongea na kuchangia mengi fanya ufanyavyo achana na uyo mke wa mtu ni heri utembee na kahaba lakini sio mke wa mtu
 
Kama kunakitu ambacho huwa kinaumiza sana wanaume ni pale anapobaini mke wake anagongwa na mtu mwingine, maumivu yake huwa hayafutiki kirahisi. Huyo jamaa inaonyesha bado anamwamini sana mke wake. Ila za mwizi ni 40. Kuna siku mtoa mada utakuja kugeuzwa bucha.
 

Mzee wa kazi mbalizi1 haya mambo magumu sana siyo [emoji1549]
 

There is exceptional to Every general rule
Hapa umeandika ukweli mtupu
 
Hiyo ndo laana ya kuvunja kiapo cha ndoa....! Hapo usipoangalia lazima ndoa moja ivunjike utaamua mwenyewe.......

Si unajifanya una huruma sana unashindwa kumuacha,ngoja uachwe wewe na mkeo na hicho ndicho kinachofuata...
 
Wewe ni mwanaume katili. Ukiona unakula vya watu na vyako vinaliwa pia.
 
Acha kujitete upuuzi wako,muache mkeo basi!! Unashindwaje kumuacha mchepuko? Mkeo una miaka mingapi nae? Unampenda kweli mkeo au upo nae tu sababu mmezaa na mnandoa??

Unajiendekeza tu ..... ila soon utavuna ulichopanda.

Nenda kwa mama yake kamwambie huyu kaolewa na mume wake ameshamjibu hivi juu yangu....! Wewe si unashindwa kumuacha mwambie mkweo avunje hiyo ndoa ya binti yake umuoe wewe! Na umuache mkeo usimpotezee muda uje kumuua kwa uchafu wako...
 
Namna ya kumsaidia ni kuachana na mkewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…