Nina umri wa miaka 30, naishi kwa kaka yangu, watu wananidharau naombeni ushauri

HUU MWANDIKO WA MTU MWENYE MIAKA 30, AFU MWANAUME..!! Ukiendelea hivi hutoboi..!! Kajichanganye kwenye mazege huko
 
Sijashindwa tatzo sina connection hata ya kupata kazi nilishaomba humu hata kuwa kama kibarua sikupata msaada

Mafundi wa CCTV wengi huwa ni mafundi wa kujitegemea, jaribu upite maduka mengi uwezavyo wanayouza vifaa vya CCTV na uache wasifu wako hapo na namba zako za simu...

Kuna watu huwa wanaenda nunua vifaa na huulizia mafundi madukani...
 
HUU MWANDIKO WA MTU MWENYE MIAKA 30, AFU MWANAUME..!! Ukiendelea hivi hutoboi..!! Kajichanganye kwenye mazege huko

Mafundi wa CCTV wengi huwa ni mafundi wa kujitegemea, jaribu upite maduka mengi uwezavyo wanayouza vifaa vya CCTV na uache wasifu wako hapo na namba zako za simu...

Kuna watu huwa wanaenda nunua vifaa na huulizia mafundi madukani...
Sawa kaka lakini sina msingi wowote hata vifaa pia maana sehem nyingine inahitaji uwe na vitendea kazi vya kutosha
 
Sawa kaka lakini sina msingi wowote hata vifaa pia maana sehem nyingine inahitaji uwe na vitendea kazi vya kutosha

Kwa kuanzia fundi CCTV anahitaji nini zaidi ya vitu vichache kama Wire cutter, Tester ya umeme, Screw drivers, Nyundo, Pliers, RJ45 Crimping Tool Kit, Cable puller...vitu vingine kama ngazi n.k unaweza hata kodisha, materials ya ufundi ni juu ya mteja unapompa quotation yako ikiwemo insulation tapes, conduit pipes, connection boxes, cables n.k
 
Rudi kijijini ukalime mkuu, pesa zipo mashambani au nenda kariakoo kwa mafundi simu uanze kutengeneza nao urafiki ujifunze bure then na wewe unatafuta goli lako, utaokoteleza pesapesa
 
Vp kaka na wazo langu la kuhama inalizungumziaje?
Mwaka unaweza usiishe ukajikuta unarudi mkoani, maana kurudi kwa kaka yako utaona aibu. Embu toka tafuta ata kazi za saidia fundi, ukishakuwa na akiba ya kutosha ndo ukapange sasa.
Yani uko busy kutongoza mademu wakati unalishwa na kaka yako badala ya kupambana upate ridhki, eti kupendeza unataka kupendeza 🤣 ili mademu wakuone wakati huna kipato chochote. We mshukuru kaka yako kakushika mkono kakuleta mjini na kakupa hifadhi vitu vingine unatakiwa ujiongeze mwenyewe ata kama ni kubeba zege ili mradi ufikie malengo yako.
 
Kama una smartphone nenda kariakoo kwenye maduka ya vitu mbalimbali piga picha katangaze fb au mitandao mingine ya kijamii unapoweka bei ongeza elfu mbili katika kila bidhaa au ata 4000 ilimladi bei isiwe kubwa Sana vijana wengi wanafanya hivi wanajiita mawinga na wanamaisha mazuri tu wamepanga na wanajitegemea umesema unashindaga kariakoo naimani utakuwa unajua machimbo ya vitu kwa bei rahisi all the best hutaki kuangalia flani anasema nini kuhusu wewe weka aibu pembeni nakuhakikishia ndani ya miezi 6 utakuwa umepiga atua
 
Sawa mkuu nimekuelewa sana
 
Vizuri
 
Ww ni fakeni sana ulikuwa wapi muda wote ulipokaa kwa kaka yako usijishughulishe, leo ndipo ukauze simu ili uanze maisha na utakufa masikini nyie ndio wale mkibebwa mnajilegeza badala ukaze popoma mkubwa ww
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…