Nina umri wa miaka 30, naishi kwa kaka yangu, watu wananidharau naombeni ushauri

Nina umri wa miaka 30, naishi kwa kaka yangu, watu wananidharau naombeni ushauri

Ww ni fakeni sana ulikuwa wapi muda wote ulipokaa kwa kaka yako usijishughulishe, leo ndipo ukauze simu ili uanze maisha na utakufa masikini nyie ndio wale mkibebwa mnajilegeza badala ukaze popoma mkubwa ww
Daah..kaka najutia sana hayo maisha kiukweli nimechezea muda najua mno
 
Habarini za weekend ndugu zangu natumai mmeamka vema sana.

Mimi kuna jambo kidogo linanitatiza nahitaji ushauri wenu.

Ni hivi january ya mwaka 2020 kaka yangu alikuja mkoani basi baada ya kutusalimia aliamua kunichukua na kuja nae hapa dar es Salaam.

Basi baada ya kuja huku alinipeleka kwa mtu mmoja kwa ajili ya kunifunza ufundi wa CCTV ila mambo hayakwenda vizuri, baadae akanipeleka DIT nikajifunza ufundi wa simu.

Ila baadae tukaja gundua pale chuo wanapiga brash tu lakini ufundi kamili unakuwa bado hauko fresh baada ya kumaliza nikaonekana bado sijawa fiti. Ila kwa kipindi chote hicho nipo na bro kapanga chumba kimoja.

Basi nikaamua kutulia kwanza home, kumbuka hapo tayari nishamaliza miaka miwili na sijapiga hatua yoyote na hapo bro kashatumia kama milioni hivi kwa ajili yangu lakini ni kama amna alichokifanya.

Sometime naona kabisa kama anasononeka maana kajitoa sana kwa ajili yangu ili nifanikiwe lakini inaonekana kama hakuna kitu alichokifanya na kila siku lazima aniachie hela ya matumizi.

Sasa hicho kitu kinaniumiza sana moyo hapa tayari nishamaliza miaka mitatu ila bado sina chochote na mbaya zaidi majirani pia wameanza kuniletea dharau.

Kuna kibinti fulani hivi nilikitongoza pia kinanipenda sana, sasa walivyojua wakaanza kumjaza maneno kwamba mimi sina chochote ndio maana miaka yote naishi kwa kakaangu.

Ilimbidi yule binti aniache halafu mbaya zaidi hapo tunapokaa vijana wengi ni umri wangu tayari wameoa na wengine wana magari yao kiukweli naona aibu sana. Hata nivae vizuri bado inaonekana sio chochote, naambiwa nafugwa. Kiukweli hii hali inaniumiza.

Sina pesa ila hapa nawaza kuuza simu yangu niende nikatafute chumba uswahilini huko nilipe hata miezi mitatu halafu nianze kujichanganya kitaa kuliko hizi fedhea nazozipata hapa home.

Note: Umri wangu ni miaka 30, naombeni ushauri ndugu zangu nipo katika msongo mkubwa wa mawazo.
Hauko peke yako ila toka hapo kwa bro wako haraka,nenda kajichanganye mtaani au rudi kijijini ukalime
 
Hio milioni 1 sema kutojua tu, Braza angeomba fundi simu yeyeto akufunze ujuzi kwa kujitolea ndani ya miezi 3 ungekuwa na ofisi YAKO mwenyewe. Ufundi simu unalipa ukiwa mtu na ofisi popote tu unafungua, soko ni kubwa kwa maana KILA watu wawili mmoja ana simu na hatujafika level ya kutupa simu mbovu na kununua mpya ni wachache sana, wengi simu ukaa nazo hata miaka 5.
 
Naona aibu kwa maneno nayoongelewa hapa home kwamba mimi nafugwa
Sasa aibu ya nini wakati huo ndio ukweli kua unafugwa.

Yaani kwa jiji lililojaa fursa kila mahali kwamba huwezi tengeneza hata 5k kwa siku ya kukuwezesha kujitegemea

Vaa sura ya kazi ingia graund mambo ni mengi sana ya kufanya ingia jukwaa la biashara kule ideas kibao zimewekwa tena ambazo haziitaji kua na mtaji zaidi ya afya yako tu
 
Sijashindwa tatzo sina connection hata ya kupata kazi nilishaomba humu hata kuwa kama kibarua sikupata msaada
Maisha sio connection,kwani wote waliofanikiwa walipata connection.
Connection haikufuati kitandani bali wewe ndie unaitafuta connection.
Hii nadharia ya connection huwa sizielewi nachojua KILA mtza ana mtu au ndugu yake ana shida ya Kazi hata meneja muajiri, waziri, boss wa kampuni,sijui nani wote hawa Wana ndugu wasio na ajira. Siamini Sana Katika connection Ili utoboe.
Usilale home ondoka home kazunguke changamana na watu bora ukashinde njaa mjini kuliko kushiba home, mtembea bure sio mkaa bure lazima utapata wazo
 
Tatzo lako ni uoga miaka 30 ukiamua 40 unakula kiulaini tu, piga chini ubishoo pambania kila sent usichague kazi , save ata 1000 kila sku , achana na wanawake na pombe ikibidi piga nyeto
 
Kwa kuanzia fundi CCTV anahitaji nini zaidi ya vitu vichache kama Wire cutter, Tester ya umeme, Screw drivers, Nyundo, Pliers, RJ45 Crimping Tool Kit...vitu vingine kama ngazi n.k unaweza hata kodisha, materials ya ufundi ni juu ya mteja unapompa quotation yako ikiwemo insulation tapes, conduit pipes, connection boxes n.k
Umemsaidia na kuwasaidia wengi.

DIY bora kabisa
 
Habarini za weekend ndugu zangu natumai mmeamka vema sana.

Mimi kuna jambo kidogo linanitatiza nahitaji ushauri wenu.

Ni hivi january ya mwaka 2020 kaka yangu alikuja mkoani basi baada ya kutusalimia aliamua kunichukua na kuja nae hapa dar es Salaam.

Basi baada ya kuja huku alinipeleka kwa mtu mmoja kwa ajili ya kunifunza ufundi wa CCTV ila mambo hayakwenda vizuri, baadae akanipeleka DIT nikajifunza ufundi wa simu.

Ila baadae tukaja gundua pale chuo wanapiga brash tu lakini ufundi kamili unakuwa bado hauko fresh baada ya kumaliza nikaonekana bado sijawa fiti. Ila kwa kipindi chote hicho nipo na bro kapanga chumba kimoja.

Basi nikaamua kutulia kwanza home, kumbuka hapo tayari nishamaliza miaka miwili na sijapiga hatua yoyote na hapo bro kashatumia kama milioni hivi kwa ajili yangu lakini ni kama amna alichokifanya.

Sometime naona kabisa kama anasononeka maana kajitoa sana kwa ajili yangu ili nifanikiwe lakini inaonekana kama hakuna kitu alichokifanya na kila siku lazima aniachie hela ya matumizi.

Sasa hicho kitu kinaniumiza sana moyo hapa tayari nishamaliza miaka mitatu ila bado sina chochote na mbaya zaidi majirani pia wameanza kuniletea dharau.

Kuna kibinti fulani hivi nilikitongoza pia kinanipenda sana, sasa walivyojua wakaanza kumjaza maneno kwamba mimi sina chochote ndio maana miaka yote naishi kwa kakaangu.

Ilimbidi yule binti aniache halafu mbaya zaidi hapo tunapokaa vijana wengi ni umri wangu tayari wameoa na wengine wana magari yao kiukweli naona aibu sana. Hata nivae vizuri bado inaonekana sio chochote, naambiwa nafugwa. Kiukweli hii hali inaniumiza.

Sina pesa ila hapa nawaza kuuza simu yangu niende nikatafute chumba uswahilini huko nilipe hata miezi mitatu halafu nianze kujichanganya kitaa kuliko hizi fedhea nazozipata hapa home.

Note: Umri wangu ni miaka 30, naombeni ushauri ndugu zangu nipo katika msongo mkubwa wa mawazo.
usisikilize ya watu, mjini ni shule, akili unazo wewe mwenyewe, jipange ufanye uamuzi wako mwenyewe na si kwa kusukumwa na mtu
 
Achana na mambo ya kwenda kupanga wakati huna kipato cha uhakika. Hapohapo kwa kaka yako jichanganye mtaani
Jiunge na uvccm bro...huko ni kulamba asali Tu...na tena unaonekana unapenda Sana kung'aa..huko watakung'arisha ...wewe KAZI yako ninkusema alipo mama vijana tupo...baassiii...
Taratibu zao zikoje mkuu
 
Back
Top Bottom