Nina umri wa miaka 30, naishi kwa kaka yangu, watu wananidharau naombeni ushauri

Nina umri wa miaka 30, naishi kwa kaka yangu, watu wananidharau naombeni ushauri

Ahsante sana mzee wa nondo nyuzi zako huwa zinani inspire sana

Maisha hakuna faida wala hasara.
Yasikupasue kichwa.

Fursa ulizonazo Kwa sasa,
1. Afya.
Hi ndio fursa namba moja. Kuna wenzako magonjwa yanawaandama kila iitwapo leo.

2. Ndugu anayekupenda.
Hii ni fursa ambayo wengi Hawana siku hizi. Wapo Vijana wenzako mamia hunipigia simu
Kunieleza changamoto zaidi ya zako.
Wewe unandugu anayekuthamini.
Itumie fursa hiyo vizuri Kabla naye hajakuchoka, fursa/baraka/nafasi zinatabia ya ku-expire hivyo ni vizuri kuzitumia vizuri.

3. Unakula na sehemu ya kulala.
Fursa ya Ndugu anayekupenda imetengeza fursa hizi mbili.
Ukishakula na kujua pakulala una-advantage ya kufikiria kw Utulivu nini chakufanya tofauti na MTU ambaye hanapakuishi wala pakulala.
Itumie fursa hiyo kujitafuta nawe uweze kujitegemea ili baadaye Kakaako asikuchoke.

4. Wewe ni mwanaume.
Kuzaliwa mwanaume pekee ni fursa kubwa ambayo hata Wanawake wenyewe wanaitamani.
Mwanaume umejaliwa nguvu na Akili.
Wakati Mwanamke amejaliwa tuu Akili nguvu za misuli Hana.
Hii inamaanisha unaouwezo wa kufanya kazi za nguvu au za Akili kujikwamua.

Toka, changamana na watu, ulizia kazi hat za dayworker, kutunza Bustani, au uza matunda, au jifunze kupaka Wanawake kucha,
Ni kazi rahisi zenye mtaji nafuu ambazo ukizifanya hazitakupa kikubwa lakini hautokosa Pesa ya kuvaa, Kula na sehemu ya kuishi. Ambayo hatua hiyo kibongobongo nihatua nzuri na yakumshukuru Mungu.
 
Habarini za weekend ndugu zangu natumai mmeamka vema sana.

Mimi kuna jambo kidogo linanitatiza nahitaji ushauri wenu.

Ni hivi january ya mwaka 2020 kaka yangu alikuja mkoani basi baada ya kutusalimia aliamua kunichukua na kuja nae hapa dar es Salaam.

Basi baada ya kuja huku alinipeleka kwa mtu mmoja kwa ajili ya kunifunza ufundi wa CCTV ila mambo hayakwenda vizuri, baadae akanipeleka DIT nikajifunza ufundi wa simu.

Ila baadae tukaja gundua pale chuo wanapiga brash tu lakini ufundi kamili unakuwa bado hauko fresh baada ya kumaliza nikaonekana bado sijawa fiti. Ila kwa kipindi chote hicho nipo na bro kapanga chumba kimoja.

Basi nikaamua kutulia kwanza home, kumbuka hapo tayari nishamaliza miaka miwili na sijapiga hatua yoyote na hapo bro kashatumia kama milioni hivi kwa ajili yangu lakini ni kama amna alichokifanya.

Sometime naona kabisa kama anasononeka maana kajitoa sana kwa ajili yangu ili nifanikiwe lakini inaonekana kama hakuna kitu alichokifanya na kila siku lazima aniachie hela ya matumizi.

Sasa hicho kitu kinaniumiza sana moyo hapa tayari nishamaliza miaka mitatu ila bado sina chochote na mbaya zaidi majirani pia wameanza kuniletea dharau.

Kuna kibinti fulani hivi nilikitongoza pia kinanipenda sana, sasa walivyojua wakaanza kumjaza maneno kwamba mimi sina chochote ndio maana miaka yote naishi kwa kakaangu.

Ilimbidi yule binti aniache halafu mbaya zaidi hapo tunapokaa vijana wengi ni umri wangu tayari wameoa na wengine wana magari yao kiukweli naona aibu sana. Hata nivae vizuri bado inaonekana sio chochote, naambiwa nafugwa. Kiukweli hii hali inaniumiza.

Sina pesa ila hapa nawaza kuuza simu yangu niende nikatafute chumba uswahilini huko nilipe hata miezi mitatu halafu nianze kujichanganya kitaa kuliko hizi fedhea nazozipata hapa home.

Note: Umri wangu ni miaka 30, naombeni ushauri ndugu zangu nipo katika msongo mkubwa wa mawazo.
Endelea na bidii ya kutafuta maisha hujachelewa kuna watu wana miaka 50 na mambo bado wapo kwa wazazi au ndugu zao.
 
Maisha hakuna faida wala hasara.
Yasikupasue kichwa.

Fursa ulizonazo Kwa sasa,
1. Afya.
Hi ndio fursa namba moja. Kuna wenzako magonjwa yanawaandama kila iitwapo leo.

2. Ndugu anayekupenda.
Hii ni fursa ambayo wengi Hawana siku hizi. Wapo Vijana wenzako mamia hunipigia simu
Kunieleza changamoto zaidi ya zako.
Wewe unandugu anayekuthamini.
Itumie fursa hiyo vizuri Kabla naye hajakuchoka, fursa/baraka/nafasi zinatabia ya ku-expire hivyo ni vizuri kuzitumia vizuri.

3. Unakula na sehemu ya kulala.
Fursa ya Ndugu anayekupenda imetengeza fursa hizi mbili.
Ukishakula na kujua pakulala una-advantage ya kufikiria kw Utulivu nini chakufanya tofauti na MTU ambaye hanapakuishi wala pakulala.
Itumie fursa hiyo kujitafuta nawe uweze kujitegemea ili baadaye Kakaako asikuchoke.

4. Wewe ni mwanaume.
Kuzaliwa mwanaume pekee ni fursa kubwa ambayo hata Wanawake wenyewe wanaitamani.
Mwanaume umejaliwa nguvu na Akili.
Wakati Mwanamke amejaliwa tuu Akili nguvu za misuli Hana.
Hii inamaanisha unaouwezo wa kufanya kazi za nguvu au za Akili kujikwamua.

Toka, changamana na watu, ulizia kazi hat za dayworker, kutunza Bustani, au uza matunda, au jifunze kupaka Wanawake kucha,
Ni kazi rahisi zenye mtaji nafuu ambazo ukizifanya hazitakupa kikubwa lakini hautokosa Pesa ya kuvaa, Kula na sehemu ya kuishi. Ambayo hatua hiyo kibongobongo nihatua nzuri na yakumshukuru Mungu.
Sawa kaka lakini binafsi kwa wazo langu naona hapa kwa bro nimeshakaa sana so nilikuwa na plan niuze simu yangu niongeze na pesa kidogo niweze kupanga chumba hata kama nitalala chini halafu niingie mtaani kujichanganya nahisi nikichukua hii hatua itanifanya nijitume zaidi kuliko kuendelea kubaki kwa bro maana tayari ntakuwa na majukumu tofaut na sasa
 
Baada ya kuchukua kadi nini kinafuata mkuu je nitaweza kuingiza kipato chochote kwa siku
Yes...kila siku nenda pale Lumumba...we sema sifa zote nzuri za CCM kwa kila.mtu...ingia mule ndani...Anza kuimba CCM mbele kwa mbele...mpaka kufikia Saa 10 jioni utakuwa na zaidi ya buku 10, hii ni uhakika ndugu...wahi haraka
 
Samahani kwa kauli hii mkuu ila wewe ni miongoni mwa vijana wa hovyo ktk taifa hili. Mtu wa miaka 30 kukosa conscious na msukumo wowote wa kufanya mishe yoyote ili ujilishe wewe mwenyewe tu ni tatizo pana sana. Kaka yako ana nia njema sana ila naye ameshindwa kujua tatizo lako la msingi ndio sababu msaada wake hauzai matunda

Kaka yako anapaswa kukufukuza hapo kwake uingie mtaani huko ukajitegemee kwa kukomaa kiume. Huko utanyooka tu na utajitambua kwa sababu mitaa haina huruma

Imagine hata hukuweza kufanya reasearch na kuchangia tu hata mawazo kwa kaka yako ili kwa hiyo hela kidogo aliyokua nayo upate chuo kizuri na fani nzuri yenye kukusaidia. Maana yake wewe umerelax ufanyiwe kila kitu. Wewe ni hovyo kabisa mkuu na unahitaji kuinuka,kujifunza maisha na kuchukua hatua za kiume!

Samahani sana kama itakukwaza
 
Yes...kila siku nenda pale Lumumba...we sema sifa zote nzuri za CCM kwa kila.mtu...ingia mule ndani...Anza kuimba CCM mbele kwa mbele...mpaka kufikia Saa 10 jioni utakuwa na zaidi ya buku 10, hii ni uhakika ndugu...wahi haraka
Duuh..kwahiyo ntakuwa naimba tu muda wote au kuna shughuli nyingine ntapewa na kuanzia asubuhi mpaka jion ntakuwa hapo hapo ofisini kwao
 
Vipi kaka na wazo langu la kuhama unalizungumziaje?
Kama mimi nakushauri hama tafuta getho uswahilini ukaishi. Ongea na kaka yako akulipie chumba kwa miezi 3. Ila kula juu yako.
Utakuja unishukuru. Kichwa bila kupata moto hakiwezi kufikiri
1. Unataka ule
2. Uvae
3. Ulipie chumba
4. Ununue vitu
 
Kiafrika Afrika, miaka 30 kwa mwanaume ndio kwanza kunakucha. Angekuwa mwanamke au mchezaji wa mpira, umri huo tungesema ni Mzee.

Hajachelewa, aende kwa mafundi akajitolee ili aongeze ujuzi
Sio kweli aisee. Hata yeye mwenyewe mhusika amekiri kuwa hapo mtaani vijana wa rika lake wameshamuacha kimaendeleo.

Miaka 30 ni umri ambapo mtu anakuwa ameshashika hela zake mwenyewe kwa muda wa kutosha tu hata kama bado anaishi kwa wazazi wake lakini hatakiwi kuwa anategemea pesa za wazazi wake. Awe anaishi kwa sababu anahitajika kukaa nao kuwasaidia labda ni wazee.

Kukaa kwa kaka miaka 30 hapana haikubaliki. Kaka sio mzee.
 
Kiafrika Afrika, miaka 30 kwa mwanaume ndio kwanza kunakucha. Angekuwa mwanamke au mchezaji wa mpira, umri huo tungesema ni Mzee.

Hajachelewa, aende kwa mafundi akajitolee ili aongeze ujuzi
Kama kijijini kwao kupo vizuri kwenye masuala ya kilimo amuombe kaka yake fedha za kwenda kuanzisha miradi ya kilimo. Akitulia kwenye kilimo atatoboa, siku hizi bei za vyakula na mazao mengine zipo juu sana.
 
Duuh..kwahiyo ntakuwa naimba tu muda wote au kuna shughuli nyingine ntapewa na kuanzia asubuhi mpaka jion ntakuwa hapo hapo ofisini kwao
Huyo kakwambia kiutani, lakini hiyo nayo ni fani inayoingiza pesa.

Inaitwa u-Mwijaku au uchawa.

Kuna mtu anaitwa Mwijaku mtandaoni mfuatilie sana mapito yake uanze kumuiga.

Kwenda kuimba sifa za CCM Lumumba ni sawa na kuwafundisha Injili wachungaji. Utapoteza muda.

Kinachotakiwa ni utafute watu wanaopenda sifa uanze kuwasifia mitandaoni na kujirekodi video. Mfuatilie Mwijaku utaona anavyofanya.
 
IDEAS ZA KUTOKA KIMAISHA KWA MTAJI MDOGO


1.Nunua pikipiki ya Dhamana ukaanza biashara ya Boda boda.
2.Fungua saluni
3.Mradi wa tofali za kuchoma
3.Fuga kuku
4.Somea ujuzi wowote
5.Mradi wa kushona nguo
6.kijiwe cha kuchomelea
7.kijiwe cha milango na madirisha ya aluminum
8.Mgahawa Mdogo
9.Kijjwe cha kahawa
10.Mashine ya kupukuchua mazao mfano mahindi, mpunga, mtama, karanga, nk
11.Mashine ya kukata nyasi, kupalilia
12.Kuuza mbuzi, kuku,
13.Biashara ya mazao.
14.kukodi bus, daladala na kuzisimamia upate cha juu
15.Kutengeneza sabuni, sanitizer, handwash,
16.Kutengeneza unga wa lishe
17.Kilimo cha umwagailiaji water pump, mbegu, madawa
18.Jiko la supu
19.kutengeneza mkaa mbadala
20.Kuuza chips
21.Kukaanga kuku
22.Kutengeneza vitafunio
23.Kuzalisha ethanol
24.kufuga poko mbuzi katoliki
25.Kufungua kilabu cha pombe za kienyeji
26.Kufungua vijiwe vya Kukusanya ubuyu maporini yakitimia magunia unaleta mjini
27.Kuuza juice
28.Kuuza juice ya miwa
29.Kijiwe cha kukaanga samaki jioni
30.Shughuli za upambaji kumbi
31.Kusambaza bidhaa majumbani
32.Kusambaza bidhaa basic needs kwenye maduka ya vijijini yaani unanua mjini unasambaza kwa oda viduka vya vijijini.
33.Kuzunguka minadani kuuza nguo za mitumba, vyombo, nk
34.Kufungua tuition center
35.Kufungua grocery
36.Kuwa wakala wa bidhaa za viwandani
37.kijiwe cha kukusanya taka za plastic, chuma,oil chafu na tairi chakavu.
38.Kufungua genge la kuuza basic home need
39.Kufungua ofisi ya kupiga nguo pasi.
40.Ofisi ya kutengeneza viatu na mabegi
41.Kutengeneza vyombo vya kupikia mfano, majiko, ndoo, sufuria, mifuniko, vikaangio, nk
42.Saluni ya kutengeneza kucha za wanawake
43......Jengea vyumba vitatu wazazi wako nyumba ya Bati upate baraka
44..Nunua shamba
45.Nunua ng'ombe wadogo watano kwa laki na nusu anza ufugaji.
Au nunua mbuzi anza kufuga
46.Fungua kijiwe cha kuonyesha mpira
47.duka la nguo za kupoint classic za mitumba piga pasi tundika kwenye enga
48..Ofisi za baiskeli za kukodi hapo unapata baiskeli nane
49..Duka la spea za pikipiki na baiskeli
50.Duka la dawa na vipodozi
51..ofisi ya kuchaji simu kwa sola vijijini
52..ofisi ya uwakala wa kutuma na kutoa pesa
53.. Bustani za kuzalisha miche ya miti na matunda
54... Ufugaji nyuki na kuuza asali
55.. Kuzalisha unga wa muhogo
56..Direct sale yaani door to door delivery hapa unakuwa na torori na speaker unapita KILA nyumba unauza bidhaa na kuchukua oda ya nini wanataka Ili kesho uwaletee.
57.Utengenezaji pellets chakula cha mifugo,samaki.
58..unga wa lishe
59..mikeka
60.bidhaa za mianzi.
61.utengenezaji wine,
62.usafi wa majumbani
63.kuuza uji wa ulezi,mchele
64.utengenezaji mbolea za mboji na za maji.
65.utengenezaji wa vigae vya cement na vya udongo.
66.kupanda miti kwa ajili ya nguzo na mirunda
67.utengenezaji wa ndala
68.utengenezaji viatu
69.Upondaji kokoto
70.ufundi simu na radio
71.Utengenezaji mifagio
72.utengenezaji crips za Mihogo,ndizi,viazi,nk
73.Utengenezaji tambi,ubuyu
74.panda mlonge,au nyonyo,au mibono au muarobaini Ili uje uuze mafuta,au utengeneze sabuni.
75.Kutengeneza siagi ya karanga
76.Home delivery hapa ni kupita KILA nyumba na kuchukua oda za mahitaji yao then unaenda kununua unawaletea
77.Utengezaji wa vifungashio vya karatasi
78.utengenezaji mitungi,vyungu,majiko ya udongo
79.Kuwatengeneza kucha wadada
80.Ufundi simu.
Chukua idea yeyeto hapa kama umekwama uanze vipi
 
Mwaka unaweza usiishe ukajikuta unarudi mkoani, maana kurudi kwa kaka yako utaona aibu. Embu toka tafuta ata kazi za saidia fundi, ukishakuwa na akiba ya kutosha ndo ukapange sasa.
Yani uko busy kutongoza mademu wakati unalishwa na kaka yako badala ya kupambana upate ridhki, eti kupendeza unataka kupendeza 🤣 ili mademu wakuone wakati huna kipato chochote. We mshukuru kaka yako kakushika mkono kakuleta mjini na kakupa hifadhi vitu vingine unatakiwa ujiongeze mwenyewe ata kama ni kubeba zege ili mradi ufikie malengo yako.
Hiyo kazi ya saidia fundi, niliipata mwaka 1997 akili ilinikaa vizuri. Yaani siku ya kwanza nililala kama nimekufa. Ila ilinipa uelekeo mzuri sana kwenye maisha yangu. Hadi sasa namshukuru Mungu mambo yangu sio mabaya sana.
 
Elimu ya bongo, huwezi maliza mafunzo alaf ukawa competent.

Kwavile ushapata basic knowledge ya ufundi simu, sogea kariakoo au kwa fundi yoyote wa hayo mambo, muombe uwe Msaidizi wake bila malipo, lengo ikiwa ni kupata ujuzi.

Baada ya hapo mambo yatajiset. Ila ukisema uanze kutongoza madem na huku hujajua unatoboaje, mwaka huu pia utaisha ukiwa kwa kaka yako.
Ushauri mzuri
 
Ww ni fakeni sana ulikuwa wapi muda wote ulipokaa kwa kaka yako usijishughulishe, leo ndipo ukauze simu ili uanze maisha na utakufa masikini nyie ndio wale mkibebwa mnajilegeza badala ukaze popoma mkubwa ww
Acha kumtuksna huyu bwana maisha ya mwanadamu Ni hadithi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Sawa kaka lakini binafsi kwa wazo langu naona hapa kwa bro nimeshakaa sana so nilikuwa na plan niuze simu yangu niongeze na pesa kidogo niweze kupanga chumba hata kama nitalala chini halafu niingie mtaani kujichanganya nahisi nikichukua hii hatua itanifanya nijitume zaidi kuliko kuendelea kubaki kwa bro maana tayari ntakuwa na majukumu tofaut na sasa

Usiuze simu.
Baki Kwa Bro.
Tafuta vibarua.
Kusanya Pesa kidogo kidogo Kwa mwaka na Nusu.
Ukishapata milioni moja au laki tano,
I. Nunua godoro, Nunua Niko la gesi na mkaa, Nunua sufuria nne. Bakuli, sahani na vijiko.
2. Nunua mapazia, shuka mbili na neti.
3. Nunua na neti.
Jumla hutomaliza 300,000
Inayobakia lipia Kodi zile za elfu 30-40 miezi mitatu.
Inayobakia Nunua chakula ndani kitakachokuaukuma hata miezi miwili. Kwa vile uko mwenyewe Hilo hatalitakushinda
 
Back
Top Bottom