MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Kulingana na UNESCO hadi mwaka 2015, kiwango cha watu wazima kusoma na kuandika cha ni 77.89% nchini Tanzania. Wakati kiwango cha wanaume kusoma na kuandika ni 83.2%, kwa wanawake ni 73.09%, kuonyesha pengo kati ya jinsia.
Kwa mujibu wa taarifa nyingi zilizopo ni kwamba Tanzania imeshuka kwa zaidi ya 10% kulinganisha na kiwango kilichokuwepo miaka ya 70. Ripoti zinasema Tanzania ilikuwa na literacy rate ya kwenye 90% ambacho ni kiwango cha juu sana kwa nchi. Kwa ufupi bongo kwa miaka hiyo watu karibu wote walikuwa wanajua kusoma na kuandika. Hakika serikali ya Mwalimu iliupiga mwingi.
Nimeanza na utangulizi huo uliokaa kisomi ili sasa nieleze kwanini nimeandika huu uzi. Kwa muda mrefu kuna nimekuwa nikikerwa mno na jinsi watu wengi wanavyoshindwa kuandika vizuri maandishi yao bila kukosea. Matumizi yasiyo sahihi herufi "L" na "R" yamekuwa changamoto kubwa. Isitoshe mtaani tunamoishi kuna watu wengi sana wasiojua kuandika kabisa wala kusoma. Wala halihitaji sana utafiti kujua kwamba kuna hili tatizo.
Mitandao ya kijamii imesaidia sana kujua ukubwa wa tatizo. Watu wengi mno ukisoma comments na captions zao utapandwa na jazba mno. MwanaJF FaizaFoxy huuliza kwamba huko shuleni ulienda kusomea ujinga? 🤣🤣. Watu maarufu wengi hasa wanamuziki na wanafilamu/maigizo (Bongo movie) wamekuwa vinara wa maandishi yaliyokosewa kuandikwa, iwe Kiswahili au kiingereza. Ukitembelea mtandao wa Facebook ndo utaona maajabu mengi hadi unatamani watu wanyang'anywe simu na kurudishwa darasani kwa lazima.
Mimi nashauri wazazi wawafuatilie watoto wao toka wakiwa wadogo ili kujenga mtanzania ambaye hatatia aibu kwa kushindwa hata kuandika na kusoma lugha ya kiswahili. Waalimu nao wasiwe nyuma kutimiza wajibu wao. Wale waalimu wa zamani wa mwandiko darasa la kwanza na la pili bado wapo? Serikali nayo ifuatilie kila kitu kwa karibu sana kwa sababu kwa ninayoyaona mtandaoni huenda tumeshashuka tena.