Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Wakuu, ukweli ni kwamba tangu suala la kuagiza Dreamliner lilipotangazwa, niliingiwa na wasiwasi sana juu ya uwezo wa ndege hii kujaza abiria kwa safari za ndani na nje.
Wasiwasi wangu umezidi kuongezeka niliposikia kuwa hata baada ya matangazo mengi juu ya kuanza safari za ndani kwa ndege hii na nauli ya chee, imeshindwa kujaa kwa safari yake ya kwenda Mwanza na kurudi. Uwezo wa Dreamliner ni kubeba abiria 262. Hadi sasa safari ya Mwanza ya asubuhi ni abiria 244 na ya mchana abiria 158. Ikumbukwe kwamba mara nyingi safari ya kwanza huwa inakuwa na hamasa kubwa na abiria hupatikana kuzidi uwezo wa ndege.
Sasa je, hizi ni dalili kwamba huko mbele tunaweza kuwa na tatizo la kujaza ndege yetu kwa safari za ndani au nje? Uwezekano huo upo, na ATC wanapaswa kulikubali hilo. Je, tumenunua tembo mweupe?
Sidhani kama kuna lolote tunaweza kufanya kwa safari za ndani zadi ya kushusha bei hata zaidi kama "promotional fares". Ni afadhali ushushe nauli ili upate abiiria wengi katika kile wachumi wanaita "economies of scale".
Kwa safari za nje, ningewaomba ATC wafikiri kwa haraka kufanya mpango wa aidha ku-partner na mashirika mengine, ama kuwa na "code sharing" arrangement hasa na mashirika ya nchi zinazotuzunguka kama Malawi, Msumbiji, Rwanda, nk, pamoja na nchi ambazo ATC watakuwa wanapeleka Dreamliner, kama India na China. Sijajua kwa nini Dreamliner haijapangiwa safari za South Africa - ambapo tunaweza kuwapunguzia South Africa SAA kuwa na safari moja kwa siku badala ya mbili ili kutoa nafasi kwa Dreamliner. Tukienda Johannesburg (ningeshauri kwenda Johannesburg kupitia Cape Town, yaani Dar-CPT-JNB-DAR), tunaweza kuwa na code sharing na nchi zote za SADC. Hata Nairobi, Kenya Airways wana safari karibu tatu za kuja Dar, tuwapunguzie hadi moja kwa siku ili tuanze na route hizi.
Hadi sasa angalia kwamba bado tunasimama peke yetu, hata code sharing hatuna. Ukweli ni kwamba hata safari za nje kwenda sehemu kama Mumbai huenda kuna Watanzania hawatapanda Dreamliner ya ATC kwa kuwa watataka kupanda ndege ambazo wako kwenye programu zao za "frequent flyer" ili wanufaike na kupata mileage au kuongeza status za uanachama wao.