Watu kama wewe mnaishi kwenye nchi ya kusadikika, mna imani pasipo maarifa. Ni kwa sababu kama unavyosema, kuna mashirika mengine ya ndege ndio maana nikasema nina wasiwasi kama hii ndege itajaza abiria katika safari zake. Unajua ushindani uliopo katika biashara ya safari za ndege? Na unajua damand ya seat za ndege kwa safari za ndani ya Tanzania?
Yaani unataka nijivunie tu vitu amavyo vinaweza kufeli bila kuwa pragmatic na realistic? Mie sio shabiki kipofu wa mambo anayofanya Magufuli bwana, pale anapofanya jema nitamsifia, pale tunapokurupuka nitasema. I am a realist but not pessimist - sijui kama unajua tofauti. Na ndio maana nikatoa mapendekezo ya nini ATC wanaweza kufanya. Watu kama wewe, dogmatic people, siku Magufuli akitangaza Tanzania tumeruhusu ushoga mtashangilia na kutaka kuandamana kumuunga mkono. Give me a break.