Nina wasiwasi na hii Gari, ushauri wenu

bado nna wasi wasi kdgo nan alikwambia gear box huwa inamwagwa oil if hmna any faults ?
 
Toyota IST ni kagari kadogo sana kuwa na complications za namna wewe umeelezea. Toyota IST ni very simple kuimaintain na kuifanya idumu.

Kwanza hayo maoil umetaja ni too expensive sijui hata kwann unajitesa kuyanunua.

Hapo kwenye oil tumia tu Total 5w-30 ,na kwenye gear box tumia ATF ya total pia. Wala usicomplicate maisha. Tazama pia vitu vidogo vidogo kama timing belt na fan belt then maisha yaendelee.
 
Amesema wazi yeye ni mgeni wa gari,hapa ndipo anapata sasa uzoefu zaidi..
 
Gari yako ni nzima kabisa kwa mujibu wa maelezo yako,usijali utapata uzoefu kadri muda utavozidi songa..
 
Kila ukifanyiwa Service hakikisha unakuwepo--kama haupo uwe unamwamini SANA huyo fundi.
Range ya kubadilisha oil ni km3000 had km5000 kwa hizi oil zinazopatikana kila mahali(option bora kabisa ni Castrol au Total 5W-30)
Unaponunua gari kutoka Japan--unashauriwa kufanya service ya Oil,kubadilisha filter,aircleaner filter etc--Gearbox oil kama itaonyesha dalili za kuisha nguvu(fundi mzuri anaweza kukuambia kwa kuigusa tu ile oil uzito wake),pia mokorokoro ya chini kama utasikia inagonga gonga,hakikisha kila kitu kimekazwa vizuri(muombe fundi akuangalizie).
Kwa swala la gari lako kutoa maji kwenye exhaust-ni jambo la kawaida,tena zuri--hii inamaanisha mafuta yanachomwa vizuri na hakuna oil inayochomwa wakati engine inazunguka.
RPM kukaa chini ya 1--that is perfect--inatakiwa iwe hivyo ukiliwasha tu inapanda hadi 1.5 then inashuka hadi 0.5.
KITUNZE KIDUMU.
 
Nilipenda sababu inakaa muda mrefu 10,000km ndo nabadilisha tena oil
 
Nilipeleka garage inayoeleweka na mafundi makini, aliikagua gari akaona record ya service ikiwa japan ikaonekana gearbox oil haijabadilishwa gari ina 74,000 km akasema aichek oil kweli ilikua ni chafu nyeusi kabisa akasema tubadili akaweka t4 sijui og,

Toka nimefanya hio service gari naona hta nikanyage mafuta vipi rpm haizid 2 ikipanda sana 2.5 inarud 2 au chini ya2 fasta. Naona mabadiliko.

hio lique molly ni mbaya? Nisaidien
 
Nilipenda sababu inakaa muda mrefu 10,000km ndo nabadilisha tena oil
Unecessary expenses. total will do u just fine.... Hizo kilometers zote unataka utembee bila gari kufanyiwa service?!
 
Hayo maji ni matokeo ya joto la hewa inayotoka kwenye engine kukutana na ubaridi katika ile Bomba kwa ndani. Ndio maana huwezi kukuta hiyo hali nyakati za mchana kwa gari ambayo imeshapiga misele na bomba la Moshi limeshakuwa na joto kali na kavu.

So haina uhusiano na hali nzuri ya engine wala ubora wa service.

Kuhusu gari kutoa Moshi mweusi ni matokeo ya kuunguzwa kwa mafuta mengi kuliko kiwango. Hii inaweza kuwa ni matokeo ya Air filter ambayo imezongwa na uchafu yaani vumbi, changamoto ya mfumo wa utemaji mafuta yaani injection system, au manifold ikiwa imejiziba.......lakini pia zipo sababu zingine......
 
Unapoondesha ina fikia speed ya juu vema , i mean umeshawahi kuitest katika barabara iliyonyooka?!

Ukipata muda usiku pita nayo bara zile kama bagamoyo rd, mandela rdc, samunujoma etc..... Pale utaweza elewa namna ya kuelewa performance yake.
 
Bagamoyo road ndo daily niko na hii road, naweza kufika hadi speed 100 na gari imetulia nimefanya wheel balance & alignement hta nifike 100 rpm haizd 2 nataka niende mkoani hapa nais ndo nitaisoma vzr zaid.
 
Mmmmmmhmn..... Ngoja niende maabara kwanza then nitakuja na majibu.
 
Bagamoyo road ndo daily niko na hii road, naweza kufika hadi speed 100 na gari imetulia nimefanya wheel balance & alignement hta nifike 100 rpm haizd 2 nataka niende mkoani hapa nais ndo nitaisoma vzr zaid.
Sidhani kama kuna shida hapo. Kwa upande wangu naweza kufikisha 100, na RPM ipo kati ya 2 na 3.

Jaribu kukanyaga mafuta kuona mshale unavyopanda.
 
Pia

Moshi ukishapita kwenye catalytic converter moja ya product huwa ni ni maji ambayo hutoka kama mvuke,

Mengine hucondese ndio hayo matone tunayoona nadondoka mengine mengine hutoka kama mvuke.
 
Pia

Moshi ukishapita kwenye catalytic converter moja ya product huwa ni ni maji ambayo hutoka kama mvuke,

Mengine hucondese ndio hayo matone tunayoona nadondoka mengine mengine hutoka kama mvuke.
Yeah very true
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…