Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
"Watu wamefanya importation [emoji23][emoji23]"
[emoji3516][emoji3516] puuzia maneno hayo hapo juu , mkuu usiwe na mawazo hasi kila muda si vizuri kwa afya yako umefanya jambo la maana kutomuuliza maana inaweza kuwa unamuhukumu tu bure.
Kama unampenda sana, na huwezi kumuacha; usiangaike kumuuliza chochote, wewe akija mpelekee moto maisha yaendelee.
Kwa sababu, itakuwa haina maana ya kumuhoji, huku ukiwa hauna uwezo wa kufanya maamuzi magumu itakuwa sawa na kupiga kelele tu.
Hana pa kwenda una maanisha nini?Bado mkuu atarud hana pakwenda
Yaani Dar to Singida, kaitwa na dada zake then hajashinda hata siku moja kesho anageuza, safari ya karibu km 550, alafu kwenda na kurudi kashuka dodoma!!!!!!! Then gari zimejaa hakuna usafiri, ghafla inapatikana gari ya dodoma!!¡!!! Mbona ni rahisi ku predict kwamba hakusafiiri hakua mbali na hakua nje ya mkoa!!!!
Wewe ni mwanaume mkuu head of the family!! You rule! You order Kama kiongozi wa familia inatakiwa uwe na sautiii inapobidi ukalii make wanawake akili zetu tunazijua wenyewe!Ninayo but nilimuacha aende sikutaka complicated yoyote lakini ishu ya kulala Dodoma ndo tatizo lilipo anzia sababu hiyo ratiba haikuwepo
wanawake walioajiriwa ni hatari sanaHabar wana JF,
Naimani mko wazima.
Kiukweli nimekuwa na wasiwasi na safari ya wife, sijui kwanini lakini ni safari ambayo siielewi kabsa wakuu. Nina mashaka nayo coz naona mapicha picha tu.
Ni kwamba wife kasafiri juzi ijumaa kuelekea Singida lakini safari yake sielewi elewi kabisa, kwasabubu kwanza ni safari ya kushtukiza lakini pia mpaka now sielewi aim ya safari ni nini mpaka now.
Alhamisi amerudi kutoka kazini usiku tunalala ndiyo ananipa taarifa ya kuwa kesho Ijumaa anasafiri, nikamuuliza unaenda wap? Akaniambia kapigiwa simu na dada zake wamemuita ambao wanakaa Singida. Nikamuuliza kunatatizo akasema hapana, ila sijui wanashida gani na mimi ndiyo wamenipigia simu niende.
Kiukweli nilikuwa nimechoka nahitaji kupumzika, sikutaka ku complicate kitu, nikamjibu sawa nikalala. Then asubuhi nikajiandaa nikaenda kazini vizur. Niko job ananipigia simu kuwa ndiyo anatoka home anaelekea stendi kupanda bus. Iikuwa almost kama saa 7 hivi mchana nikamjibu haya na nikamuuliza kama kunakitu chochote anahtaji akasema hapana yuko powa.
Basi nikakata simu lakini kiukweli ghafla akili yangu ilishikwa na wasiwasi juu ya safari yake but sikutaka ku doubt anything nikapotezea. Baadaya kupita kama lisaa akanitumia message kuwa amepata basi but akifika Dodoma atashuka kuna ndugu yake anamchuka then wanaenda wote.
Daah, sikutaka pia ku doubt wala mambo mengi nikamjibu sawa, nikaachana naye nikaendelea na kazi zangu, but bado sikuona sababu ya yeye kushuka Dodoma. By saa 2 ndiyo ananiambia ndiyo wanaondoka Dodoma nikamjibu sawa safari njema tukaacha hivyo. Basi mi nikarud home usiku kwakuwa nilishapita somewhere nikapata chakula nikafika home niko good, nikaoga nikaingia kwa bed nikampigia ananiambia kashafika ila kachoka na safari nikamuacha nikapumzika.
Sasa leo Jpili tumeongea asubuh vizur tu na tukaagana baadae by saa 7 mchana ananiambia ndiyo anataka kurudi leo. Nikamuuliza mbona hukuniambia asubuhi na kwanini usingeondoka asubuhi? Sijaona cha maana anachonijibu, basi nikamwambia haya kama unarudi leo. Tuakaacha baada ya kama nusu saa ananipigia simu ananiambia kuwa yupo stendi, mara gari sijui hakuna, mara zimejaa, mara nimechoka nasikia usingizi, nikamwambia sasa siungebaki ili uondoke kesho asubuhi akasema sawa tukaacha.
Baadae ananitumia message eti amepata gari ila linaishia Dodoma kwaiyo atashuka Dodoma. Aloo nikasema kimoyomoyo hapo Dodoma hapo siyo bure, coz kwenda kashuka Dodoma kurudi baada arud kesho kama kweli kakosa usafiri na tumekubalina anarudi kesho mapema na sidhani kama kweli alikosa usafiri by that time ananiambia kuwa kapata usafiri.
Ila unaishia Dodoma so ataenda kulala Dom, sikutaka ku complicate nikamjibu sawa basi nikaachana nae. Ila cha ajabu baada ya hapo akawa kimya hakusema kama kafika au laa. Yaani ndo ananitumia text saa hii, saa 5 usiku kuwa alifika salama ila alishindwa kuniambia coz vidonda vya tumbo vilimshika akafikia kupumzika. Heheheh nacheka ila najua mwenyewe wakuu but sijamjibu na sitamjibu lakini namsubiri arudi kesho nikitoka kazini anieleze vizuri kuhusu hii safar yake.
Japokuwa mimi siyo mtu wa kumchunguza mwanamke na sipendi kabisa kuchunguza mtu sababu naelewa what’s gonna happen.
Wakuu kama kuna la kuniongezea karibuni sana, uwanja ni wenu.
Ungemwambia naomba niongee na dada zako waliokuita , inamana umeoa ufahamiani hata na ndugu zake
Aiseee [emoji23][emoji23] watu wengine kama hamjaoa hata msioe.Duh nasoma hadi nalia kwa hasira, bro huu uzi labda kama umeamua kuchangamsha jukwaa ila kama ni kweli umekosea sana ..huyo mimi ningemuua kbs
Sasa ndugu yangu kama mkeo mbona ndugu zake wanamchukulia kama anaishi na muhuni fulani how come kwa dharula hivyo usipewe taarifa wewe kwamba mkeo anahitajika na kama kuna tatizo, kwa maana wewe ndiyo mkuu wa kaya na unajua kama nauli ipo au haipo wewe ndiyo unapaswa kumsuport kwa kujua wapi upate pesa ya fasta, isije kuwa mkeo kakuzoea sana anaona hauna maamuzi yoyote juu yake.Hapana mkuu ni mkewangu na niomemuoa