Nina wasiwasi sana na kesi zilizohukumiwa na Werema akiwa judge

Nina wasiwasi sana na kesi zilizohukumiwa na Werema akiwa judge

Wana JF, kuna ukweli kwamba unaweza ukawa msomi sana na bado ukawa huna uwezo wa kutumia kisomo chako katika kuamua mambo. Kwa kifupi, mtu aliyesoma sana mambo ya utawala haina maana ndiye atakuwa mtawala au meneja bora sana kuliko wengine.

Kwa mantiki hii, nina wasiwasi sana na kesi zilizosimamiwa na Werema akiwa judge. Kwa kifupi namwona Werema kama mtu ambaye was probably one of the most incapable judges to have ever been appointed hapa Tanzania.

Ningependa sana kujua hukumu zake, na kesi ngapi alizohukumu zilikatiwa rufaa na rufaa hizo kufanikiwa. Wapi naweza kupata taarifa kama hizi?

Hata bila kupata taarifa zaidi itoshe tu kukubali ukweli kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania inakuwa na mwanasheria mkuu bomu kupita wote waliomtangulia.
 
Hata bila kupata taarifa zaidi itoshe tu kukubali ukweli kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania inakuwa na mwanasheria mkuu bomu kupita wote waliomtangulia.

Ukweli ni kwamba JK anapaswa kujitafakari sana ikiwa Werema anastahili kuendelea kuwa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania. Unajua wengi wetu tumeshaanza kuona huenda Werema si kwamba hana busara kiasi cha kufanya anayofanya, bali anajua JK au mtu mwingine hawawezi kumfanya lolote hata aboronge kiasi gani.
 
Naona wewe ndio Werema mwenyewe umekuja kivingine. Sasa naomba kukwambia kwamba kusoma ni pamoja na kuwa mstaarabu na kuweza kujua baya na zuri. Sasa tofauti ya msomi na ambae ni mbumbumbu itaonekana wakati gani?

Mkuu kuna kitu ambacho wanasheria katika mfumo wa Mahakama wanakiita JUDICIAL HUNCH ,ikimaanisha tabia ,desturi miiko,mila na namna ambavyo mtu mwenye taaluma fulani ya Kisheria katika ngazi ya Mahakama na Hususan Judge anatakiwa kuwa.Kumbuka huyu ni mtu anaye hitajika kutumia busara,uvumilivu na hekima ya hali ya juu kwa kila anacho kifanya NI MTU AMBAYE SHERIA IMEMPA MAMLAKA YA KUSIKILIZA SHAURI NA KUTAMKA FULANI ANYONGWE HADI KUFA ... mtu wa namna hii hatarajiwi kutoa hadharani kauli nyepesi na za hovyo na vitisho kama alivyo fanya Bwana Werema.Kauli hizi ni za wapiga debe na kwenye vijiwe vya wavuta bangi.

Hili jambo ni kinyume kabisa na misingi na maadili ya Kijaji na ni aibu kubwa kwa aliye mteuwa na amewaaibisha Majaji wote.Hili ndilo Mh.Tundu Lisu alisisitiza umuhimu wa kuangaliwa upya kwa mfumo wa uteuzi wa Majaji hii . .Kwa Werema bado haja chelewa anaweza kuomba radhi na kukubali kuwajibika kwa kauli hii ya kipuuzi .
 
Kuwa msomi hakuondoi tabia za asili za binadamu kama kusahau, kughadhabika, kusinzia n.k na kuwa tabia hizo haina maana kwamba elimu yako haina maana. Kilichotokea Bungeni kwa AG na KAFULILA ni havihusiani kabisa na taaluma zao, ni tabia za asili za mwanadamu kama kukasirika n,k. Kudharau taaluma ya mtu kwa sababu tu ya kutamka neno fulani inaonesha ni jinsi gani tulivyo weupe kwenye vichwa vyetu.

kama usomi hauwezi kukusaidia kuacha tabia za asili za hovyo!umehudhuria darasani hujasoma na kuelimika.
 
kama usomi hauwezi kukusaidia kuacha tabia za asili za hovyo!umehudhuria darasani hujasoma na kuelimika.

Definitely. Sina wasiwasi kuhusu usomi wa Werema. Ninaamini ana vyeti kuthibitisha hili, vyeti ambavyo natarajia alivipata kihalali. Wasiwasi wangu mkubwa ni kuhusu kuelimika kwake.
 
Wana JF, kuna ukweli kwamba unaweza ukawa msomi sana na bado ukawa huna uwezo wa kutumia kisomo chako katika kuamua mambo. Kwa kifupi, mtu aliyesoma sana mambo ya utawala haina maana ndiye atakuwa mtawala au meneja bora sana kuliko wengine.

Kwa mantiki hii, nina wasiwasi sana na kesi zilizosimamiwa na Werema akiwa judge. Kwa kifupi namwona Werema kama mtu ambaye was probably one of the most incapable judges to have ever been appointed hapa Tanzania.

Ningependa sana kujua hukumu zake, na kesi ngapi alizohukumu zilikatiwa rufaa na rufaa hizo kufanikiwa. Wapi naweza kupata taarifa kama hizi?

Watanzania wenzangu, mimi huyu jamaa nilimuona kuwa tatizo hata kabla ya hili suala la Escrow. Ninarudia thread niliyoweka siku nyingi kidogo. Naona wasiwasi wangu umerihirishwa kwamba haukuwa wa bure. Natumaini JK atakuwa makini zaidi safari hii, kumyeua mtu ambaye kweli ana uwezo wa kushika bafasi hii badala ya hawa wasanii tuliozoea kuona wakiteuliwa kama sadaka mwenye kupata apate, mwenye kukosa akose!
 
Back
Top Bottom