Kitaja
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 2,836
- 1,382
Wana JF, kuna ukweli kwamba unaweza ukawa msomi sana na bado ukawa huna uwezo wa kutumia kisomo chako katika kuamua mambo. Kwa kifupi, mtu aliyesoma sana mambo ya utawala haina maana ndiye atakuwa mtawala au meneja bora sana kuliko wengine.
Kwa mantiki hii, nina wasiwasi sana na kesi zilizosimamiwa na Werema akiwa judge. Kwa kifupi namwona Werema kama mtu ambaye was probably one of the most incapable judges to have ever been appointed hapa Tanzania.
Ningependa sana kujua hukumu zake, na kesi ngapi alizohukumu zilikatiwa rufaa na rufaa hizo kufanikiwa. Wapi naweza kupata taarifa kama hizi?
Hata bila kupata taarifa zaidi itoshe tu kukubali ukweli kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania inakuwa na mwanasheria mkuu bomu kupita wote waliomtangulia.