Nina wazo la Biashara ila sina mtaji

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
2,345
Reaction score
6,970
Wakuu habarini za leo, natumai mko kamili gado.

Ninalo wazo kubwa la biashara ambalo likitekelezeka hakika litanipatia ukwasi wa kutupwa na nitakuwa moja ya matajiri vijana kwenye hii nchi.

Tatizo sina mtaji wa kutekeleza wazo lenyewe, nachokifanya kwa siku hizi chache nakwenda kulisajili kwa umakini mkubwa kisha natafuta wadau tulifanyie kazi naamini litatupatia mafanikio makubwa mno.
 
TUKANA UONE Can u kindly share?or Hit my PM😊👋
 
Mkuu hapo ni sawa na kuwa na sight mirror ila gari huna.
 
Ni biashara gani? Ungetuambia ni kitu gani unataka kufanya, gharama, na mapato. alafu tunaweza kuangalia na kuona kama tunaweza kukupa mtaji.
 
Ni biashara gani? Ungetuambia ni kitu gani unataka kufanya, gharama, na mapato. alafu tunaweza kuangalia na kuona kama tunaweza kukupa mtaji.
Mkuu hapa tatizo ukiweka kila kitu kuna watu wanachukua wazo lako wanalifanyia kazi halafu wewe unaachwa mtu.

Kwa kifupi ni biashara ya usafirishaji inayohusu Daladala na Bajaji,siyo kwamba nimiliki Daladala au Bajaji la hasha!.
 
Mtaji kiasi gani?
 
Sio kwa Tanzania hii wazo tu likupe mtaji hiyo ni ndoto, pambana mwenyewe upate mtaji na uanze utekelezaji.
 
Mitaji mbona imejaa.

Anza kufanya urafiki na watu wenye pesa na wafanya biashara wakubwa, achana na mienendo yako ya sasa. Badilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…