Nina wazo la kuondoa msongamano wa watu Kariakoo, Dar es Salaam

Mr dark light

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2018
Posts
298
Reaction score
253
Habarini wakuu


lengo langu kubwa ni kuwafikia wateja walipo kwa bei ile ile ya kariakoo, kuwasaidia wafanya biashara wanaotoka mikoani na kufata mzigo, mtu mmoja mmoja anayefuata mahitaji kariakoo, hii itasaidia kupunguza foleni na msongamano wa watu pale kariakoo, itasaidia kutokutapeliwa, na kupata unachokihitaji kwa wakati muafaka, hata wa mikoani itawasaidia kununua bidhaa kwa bei ya kariakoo

Nahitaji watu ili tuweze kusaidiana kutimiza lengo hili

1: Mtu anayeweza kutengeneza application
2: mpiga picha mzuri sana
3: sponsor (kama atapatikana)

Wakiwa wakazi wa dsm itapendeza sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Idea yako ishafeli sababu wabongo zaidi ya Instagram na WhatsApp hawawezi kutumia app nyingine yoyote.

Kuna app ya kukata tickets za mabasi ya mikoani, hii hapa Welcome To StartMySafari, very useful, unakata kwa bei ile ile ya Ubungo bila kwenda Ubungo ila watu hawakutumia bado wanataka kwenda Ubungo ndo sembuse hiyo ya Kariakoo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa hayo ni mawazo yako, wangapi wanatumia kikuu, , unauhakika gani kuwa watu hawakat ticket kwa application, na vipi watu wanaotumia application kama kupatana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu idea yako ni nzr sn, km ukiwa na burning desire utafanikiwa,
Dunia inaendeshwa na teknolojia
Hiyo ni fursa ya kiteknolojia kama ukiwa na moyo utafika mbali
 
Watu wa mikoani ni watu wa mikoani tu, lazima waende kariakoo,ataenda kuhadithia nini huko mkoani?
mkuu hata nyie wa dsm...sasa hivi tunawajua vizuri sana...zamani ndo tulijua mnaishi kariakoo na posta kwenye maghorofa...kumbe kwenye maghorofa kwa asilimia kubwa ni makaratasi na makompyuta...nyie mnaishi kwenye mbavu za mbwa kama sisi tu wa mikoani.....hata nyie kariakoo mnaenda😛😛😛😛😛😛
 
Nitajie hii app
 
Sawa hayo ni mawazo yako, wangapi wanatumia kikuu, , unauhakika gani kuwa watu hawakat ticket kwa application, na vipi watu wanaotumia application kama kupatana

Sent using Jamii Forums mobile app
Nina uhakika sababu nimewahi kufuatilia closely. Start my safari jamaa aliwekeza sana kwenye hii ishu ila hakufanikiwa wala kurudisha pesa yake hata robo, watu bado wanataka kwenda stand wakakate ticket au wakijitahidi sana na kama wanamjua konda wanampigia konda simu na kutuma pesa mpesa.

Hiyo ni ticketing app ambayo ni very straightforward sijui app ya kununua vitu, bargaining, kufunga mzigo, kutuma nk kama itafanikiwa. I dare say it's bound to fail.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaitwaje hiyo app?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mfano dar arusha kawaida ni 25k kwa gar nying achana na zile wanaita luxury za maneno.
Kwny app 32800.kwann nisisubiria asbh pale stopover nadandia mbele mbele yao.
Weken room ya bargain
App lbda kwa root ya songea swanga kgoma mwanza nk
Ambazo nauli ni constant

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ambavyo wewe bado unadandia asubuhi mwingine vivyo hivyo ataenda kkoo mwenyewe hataki kulipa service fee. Wabongo ni wale wale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado inatumika hiii ?labda hajaitangaza maana mi huwa sipendi kukata tiket stendi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una wazo zuri mkuu. Ila njia unayotaka kuitumia sidhani kama itachangia kupunguza wingi wa watu kariakoo, ila itasaidia watu kupata kile wanachokihitaji kwa wakati kuliko kuzunguka mtaa mmoja kwenda mwingine mwisho wa siku unatokea ulipoanzia na bidhaa unayoitaka huyaipata.

Pia mkuu, ukiongelea app za kununua na kuuza bidhaa kwa njia ya kuangalia picha ya bidhaa na bei kisha kuwasiliana na supplier zipo mkuu, Mfano Jumia, Kupatana n.k, ila Tatizo watanzania hatujafikia huko, watu wanapenda waione bidhaa dukani na wakutane na muuzaji laivu na kuanza ku bargain bei.

Mwisho mkuu, kupunguza msongamano wa watu kariakoo ni kuathiri biashara za pale, maana katika msongamano wa watu ndipo biashara hufanyika. Nchi zote duniani zina maeneo ya masoko huria kama Kariakoo ambapo uhakika wa kupata bidhaa yoyote upo. Hivyo ule msongamano ndio fursa yenyewe.

Nadhani mkuu, Angalia zaidi namna ya kuboresha biashara ya pale Kariakoo kuliko kuwa na primary target ya kupunguza msongamano wa watu.

Ni mawazo yangu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…