Ninaachana na A-Level naenda D.I.T kusoma Diploma in Mining Engineering, Inalipa?

Ninaachana na A-Level naenda D.I.T kusoma Diploma in Mining Engineering, Inalipa?

ah ah! toka ameingia pale Prof: Nyaumwa chuo kimeanza kurudi kama zamani, yule Prof: Kondolo alikua kama kaelemewa na majuku ivi so hata chuo kikaanza kupoteana..
Kwani Prof Kondoro siyo tena mkuu wa Chuo DIT?
 
Prof: Kondoro ndio mkuu wa chuo, ila toka ameingia Prof: Nyaumwa ambae ni (DPAF) aliingia pale mwaka juzi na toka ameingia mfumo wa chuo umeanza kua mzuri sana na chuo kinazidi kua kizuri kadri siku zinavyo kwenda.
Kwani Prof Kondoro siyo tena mkuu wa Chuo DIT?
 
Namshauri dogo aende huko DIT maana usije ukagonga Division four mbaya au zero ukapoteza uelekeo wa kimaisha,yupo dogo angu anapiga mambo hapo
 
kijana naona kama una uroho wa pesa ya haraka ndo maana unataka kufanya shortcat.kama unataka kuwa mtaalam kwenye fani yoyote usijaribu shortcut kwani soko la ajira linahitaji wasomi wenye digree moja au zaidi hivyo jiunge a lever. baadae chuo kikuu utafanikiwa

Mkuu relax..., shortcAt, a-leveR, dIgree
 
Ulimaliza mwaka gani DIT?

Tujadili hoja acha kutaka kunifahamu kiundani ndio maana natumia fake id kuwakwepa wachimvi kama wewe. Nikikuambia mwaka niliomaliza DIT itakusaidia nini wewe ndugu yangu Asprin ?
 
Last edited by a moderator:

Hehehehe Nyani haoni kundule LOL
  • ni sawa hawezi ona maana liko nyuma na yeye anaangalia mbele.... Asprin na georgeallen sikatai kosa,ila hapo nli refer kwenye hii kitu
    Higher Diploma
    Higher Diploma is part of the Bachelor degree. Students who wish to exit or fail to attain Bachelors degree but have successfully fulfilled the requirements for the awards of a Higher Diploma shall be awarded the Higher Diploma. (NTA 7)
    Bachelor of Engineering (NTA 8) Programmes

    The Bachelor of Engineering (B.Eng) programmes are for six semesters covered in three academic years, which include:
    i. B.Eng (Civil Engineering)
    ii. B.Eng (Computer Engineering)
    iii. B.Eng (Electrical Engineering)
    iv. B.Eng (Electronics and Telecommunications Engineering)
    v. B.Eng (Mechanical Engineering)

zote ni barchelor of engineering in something,nikachukulia maana hiyo hiyo kwa diploma of engineering in______nadhani mmeelewa,ila thanks kwa kuniweka sawa....
 
HABARI WANA JAMII
mimi nimhitimu wa kidato cha nne, ningependa kujua taratibu za kupata nafasi
ya kujiunga na DIT AU MIST, DIPLOMA. sikuchagua kupangiwa tech collg kabla
ya kufanya mtihani, je naweza kupangiwa kwa wakati huu na serikali??
pia ningependa kujua taratibu zote za kujiunga hapo kwa yeyote anaefahamu.
ninavo vigezo vya credit zinazohitajika hapo.
ahsanteni.
 
Kama hukuchagua DIT au MIST katika selection form itabidi utume maombi ila hautalipiwa ada
 
Hata mm nnazo credt za kutosh na nliweka DIT first choice bt naomben msaada wenu kati ya compter eng Vs telecom eng
 
Hata mm nnazo crdt za kutosh na nliweka DIT frst choice bt naomben msaada wenu kati ya compter eng Vs telecom eng
 
Dah, kweli maisha yamebadilika, mtoto mdogo unawaza mshahara? No wonder ufisadi hauwezi isha. Enzi zetu hadi tunamaliza level ya kwanza versity sikuwahi kufikiria "nitapata nini na kiasi gani"
 
Mi ni engineer niliyesomea hiyo kitu COET,mdogo wangu usithubutu kufanya hiyo kitu imepitwa na wakati labda petroleum engineering itakutoa

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mimi ni mhitimu wa kidato cha nne mwaka 2012. Katika matokeo yangu nimebahatika kupata Div One ya point 11...PHY-A, CHEM-A, MATH-A, BIO-C, Additional MATH-B....ningpenda kujua kati ya A level na DIT (technical education) ipi ni nzur zaidi, na kama DIT ni kuzuri zaidi, je Mining Engineering ina soko katika ajira (wahandisi hulipwa mshahara gani?)
Asenteni.

Mdogo wangu alimaliza form four 2011 Tanga Technical na kupata division one. Akachaguliwa kwenda kusoma PCM. Mdogo wangu ni mtundu mtundu sana. Akafanikiwa kwenda A level ambako alisoma muhula mmoja tu. Alinipigia simu na kuniambia "Kaka mimi siwezi kuendelea kusoma A level, kwa kipindi chote nilichosoma sioni mwelekeo wowote wa Electronics Engineering ambayo mimi ndio naipenda. Nimeshafanya utafiti kuwa DIT bado wanapokea maombi hivyo naomba unifanyie mpango". Nikawasiliana na wazazi na sasa yupo DIT akisoma electronics and telecomunication engineering. Ninachotaka kusema ni kuwa angalia nini roho yako inaridhika ndipo uangalie soko. Mfano mimi wakati naanza chuo IT ilikuwa ina soko sana ila pindi namaliza ajira zake ikawa inasumbua. Ila kwa sababu niliipenda IT niliweza kuwa mbunifu na kutojutia kusoma IT.
 
Naomba unisaidie ipi ni marketable compt eng vs telecom eng kwa sasa
usiangalie soko angalia wewe unapenda nini...mfano kama nikisema computer engineering inasoko kwa sasa je baada ya miaka sita au saba(ambapo wewe ndio utakua unamaliza degree ya kwanza) soko lake litakuaje??? KOZI INAWEZA KUA NA SOKO KWA SASA ILA BAADA YA MWAKA AU MIAKA MINNE SOKO LIKAJAA!!! cha msingi cheki nini unapenda!!
ila kwa ushauri computer engineering iko safi maana unaweza hata kujiajiri kwa urahisi tofauti na telecom engineering...
 
Mi ni engineer niliyesomea hiyo kitu COET,mdogo wangu usithubutu kufanya hiyo kitu imepitwa na wakati labda petroleum engineering itakutoa

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

mdau, wanitisha!!! kwani Mining iko vipi, waweza ingia ndani unieleweshe?
 
Mimi ni mhitimu wa kidato cha nne mwaka 2012. Katika matokeo yangu nimebahatika kupata Div One ya point 11...PHY-A, CHEM-A, MATH-A, BIO-C, Additional MATH-B....ningpenda kujua kati ya A level na DIT (technical education) ipi ni nzur zaidi, na kama DIT ni kuzuri zaidi, je Mining Engineering ina soko katika ajira (wahandisi hulipwa mshahara gani?)
Asenteni.

USIJARIBU IKIWA UNA MALENGO YA KUENDELEA NA MASOMO (KUPATA DEGREE)

Binafsi nilichukua uamuzi kama unaotaka wewe kuchukua mwaka 1999, japokuwa sikupata marks nzuri za kunifanya kupata nafasi ya kidato cha 5 kwa shule za serikali (wakati huo) mzazi wangu alikuwa tayari kunipeleka private school (kwa wakati huo zilikuwa chache), lakini nilikataa. Nilijiunga DIT (wakati huo inaitwa Dar Tech na kuchukua kozi ya Mech. Eng.); Utakapomaliza ili kuingia university itahitajika upata alama nzuri zaidi (ambapo sio rahisi), vile vile utahitajika kufanya kazi kwa miaka 2 kwanza kabla ya ku-apply chuo kikuuu (labda kama kuna mabadiliko), utakapoomba mkopo (wanapewa kipaumbele form 6) kwa sababu wewe tayari una ujuzi.

Usiwe na haraka, wengi wanapomaliza kidato cha 4 hutamani kufanya jambo ili aanze kutengeneza pesa.

Kuhusu marketing ya kile unachotaka kusoma.....!, soma au kuchukua kozi ambayo unaipenda (utakuwa tayari kujifunza zaidi) na sio kulingana na watu wanvyolipwa; inaweza kuwa leo na soko zuri katika ajira, lakini baada ya miaka 3 mambo yakawa tofauti na hii ilitokea katika miaka fulani IT ilikuwa inalipa sana na kila mmoja akakimbilia kusoma IT; leo hii usijaribu...........!!!
 
Back
Top Bottom