Ninaamini Kabisa Mbowe angetaka kuendelea na Uenyekiti angeendelea lakini kwanini kaamua kumuachia Tundu Lisu?

Ninamjua Freeman Mbowe kitambo sana na Nina uhakika kama angetaka kubaki Uongozini angebakishwa Kwa nguvu ya Mifumo mbalimbali

Ninachojiuliza kwanini Mbowe kaamua kumuachia Tundu Lisu Chama?

Kuna nini mbele? Naendelea kufanya utafiti 🐼
Kamuachia au upepo haukuwa upande wake? Wapiga kura wamepiga kura mtu wanae mtaka. Full stop
Kafanyeni kazi
 
Ninamjua Freeman Mbowe kitambo sana na Nina uhakika kama angetaka kubaki Uongozini angebakishwa Kwa nguvu ya Mifumo mbalimbali

Ninachojiuliza kwanini Mbowe kaamua kumuachia Tundu Lisu Chama?

Kuna nini mbele? Naendelea kufanya utafiti [emoji209]
Mbowe alishindwa kwenye kura za wajumbe kwa n fasi ya wenyekiti, alipenda sanaa abaki ila ndo hivo, hana police au jeshi ambao linge laximisha matokeo
 
Umesahau mkuu,kitu kimoja.
Ungetag pia na nyuzi zako wakati wa joto la uchaguzi mkuu wa Chadema.Kipindi TL hajachukua hatamu ndo ingeleta utamu.

Maana nchi hii inaongoza kuwa na vinyonga na maiti zinazotembea
Sikutaka Yeriko, Ntobi na Wenje wajione Ndio wamembakiza Freeman Kitini

Sidhani kama utaelewa πŸ˜‚
 
Mbowe tangu 2019 alitangaza kuwa hatagombea tena uenyekiti, kilichomfanya agombee ni makubaliano binafsi na Samia akiamini kuwa makubaliano hayo yangekuwa na manufaa kwa Chadema, lakini kadiri siku zilivyokuwa zinasonga mbele kuelekea uchaguzi wenyewe aligundua kuwa wanachama wengi walihitaji mabadiliko na kama angeendelea na dhamira yake hiyo kwa nguvu aliyokuwa anasaidiwa na dola ushindi wake ungekiumiza Chama badala ya kukisaidia na kwa vile pamoja na mapungufu yake lakini Mbowe anaipenda Chadema hivyo alikubali kushindwa ili Chama kisalimike.
 
Mbowe alishindwa kwenye kura za wajumbe kwa n fasi ya wenyekiti, alipenda sanaa abaki ila ndo hivo, hana police au jeshi ambao linge laximisha matokeo
Una uhakika bwashee πŸ˜„
 
Ninamjua Freeman Mbowe kitambo sana na Nina uhakika kama angetaka kubaki Uongozini angebakishwa Kwa nguvu ya Mifumo mbalimbali

Ninachojiuliza kwanini Mbowe kaamua kumuachia Tundu Lisu Chama?

Kuna nini mbele? Naendelea kufanya utafiti 🐼
Hakuna kitu chochote zaidi ya kuamua tu kubadilishana vijiti,kama kuchuma kashachuma sana na maproject yake yanaenda vizuri,kaamua tu kuachana na mapresha ya siasa......
 
Ni Roho Mtakatifu ndiye amekufunulia haya, ubarikiwe πŸ˜„
 
Hakuna kitu chochote zaidi ya kuamua tu kubadilishana vijiti,kama kuchuma kashachuma sana na maproject yake yanaenda vizuri,kaamua tu kuachana na mapresha ya siasa......
Wakati Shule ya Msingi wanafundisha somo la SIASA ulikuwa umeshaanza shule au umeanzia kwenye Civics?

Samahani lakini
 
Ninamjua Freeman Mbowe kitambo sana na Nina uhakika kama angetaka kubaki Uongozini angebakishwa Kwa nguvu ya Mifumo mbalimbali

Ninachojiuliza kwanini Mbowe kaamua kumuachia Tundu Lisu Chama?

Kuna nini mbele? Naendelea kufanya utafiti 🐼
Hebu amka kakojoe urudi kulala tena. Kama Mbowe angetaka kumuachia Lissu chama asingehangaika kugombea tena. Angejitoa au asingechukua fomu. Full stop!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…