Ninachokumbuka kuhusu Nyakati za John Pombe Magufuli

Ninachokumbuka kuhusu Nyakati za John Pombe Magufuli

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Habari na poleni sana kwa msiba.

Niseme tu kwamba wengi wanaweza kusema mengi kuhusu Msiba huu ila mimi naweza kusema Jambo Moja. Maisha ni zawadi, tuyaenzi. ujifunze kutoka katika maisha ya Magufuli; Maisha ambayo yaliacha alama.

Mwaka 2010 mara baada ya uchaguzi mama yangu mzazi aliniuliza "Sasa akitoka Kikwete nani atakuwa Rais" Nilimtazama nikamwambia hata wewe unaweza kuwa Rais au hata mimi pia naweza kuwa Rais. Raia yeyote wa Jamhuri ya Tanzania anayo haki na wajibu wa kuwa RAIS wa nchi hii. Pamoja na hayo nilimchokoza kwani wewe ungependa nani awe RAIS. Mama yangu kwa nguvu kabisa akasema "MAGUFULI" Kwa kuwa nilimfahamu Magufuli vyema nilimwambia Jambo moja tu. Magufuli atakuwa RAIS ila utamkataa. Nikamwambia Magufuli anafanya kazi nzuri ila nafasi ya urais hasa kwa nchi yetu inahitaji zaidi ya mtu anayefanya kazi nzuri. Nilimwambia kwamba kuongoza taifa sio kazi Rais. Ni kazi ambayo inahitaji neema na huruma ya Mungu ili uweze kuifanya katika ukamilifu wake.

Kazi ya kuongoza nchi ambayo ina watu wa silka, tabia, tabaka, historia, matarajio, matamanio, maono, mitazamo tofauti huku nchi ikiwa na changamoto mbalimbali. Vipaumbele mbali mbali inahitaji karama ya kimungu ili kuweza kuindesha kikamilifu. Nchi hio inapokuwa katika dunia ambayo nayo ina mataifa ambayo nayo yana mirengo tofauti tofauti basi ujue kabisa kwamba kazi ya urais inakuwa ngumu zaidi.

Kazi ya urais inakuwa ngumu zaidi pale unapokuwa na cheo ambacho kina mamlaka makubwa sana kikatiba,nguvu kubwa sana kijeshi na uwezo mkubwa sana huku ukiwajibika kwa Mungu tu na kwa dhamira yako inakuwa ni ngumu zaidi. Hivyo basi anayetamani kuwa Rais anatamani kitu chema lakini kuwa RAIS wa nchi ni jambo gumu sana. Unapokuwa rais wa nchi unawajibika kwa kila jambo, kila mtu na kila hali. Watu wote wanakutazama wewe.

Ikafika mwaka 2015 na Magufuli akawa Rais na ndani ya MIEZI 6 yake ya mwanzo MAMA YANGU akamkataa. Sitaeleza sababu ila najua kwamba mengi yalitokea na labda yalikuwa tofuati na matarajio yake lakini alimkataa. Mimi nikamwambia MAMA hata kama mimi ningekuwa RAIS wa nchi hii ningefanya aliyofanya Magufuli ingawa ningefanya tofauti kidogo. Ningetumia nguvu kubwa zaidi katika kujenga mifumo kuliko kubomoa mifumo. Ningetumia nguvu nyingi katika kujenga uwazi badala ya kufichua siri. Ningejenga zaidi uwajibikaji wa kimfumo kuliko kuwajibisha watu. Ningejenga zaidi uzalendo wa kimfumo na sio uzalendo wa kiimla. Ningetaka nikumbukwe kama kiongozi niliyewainua watanzania. Hata hivyo binafsi nilijua kwamba Magufuli hakuwa mtaalamu wa kujenga mifumo ila hakuwa anapenda mifumo mibovu pia.

Hakuwa anapenda kuona mambo hayaendi. Hakutaka kuona watu wanateseka. Kwa sababu hio alijikuta akivunja mifumo na taratibu nyingi na kujikuta tunaingia katika zama ambazo taifa halikuwa na mifumo. Mifumo iliheshimiwa pale tu ambapo ilimpendeza yeye ila pale ambapo haikumpendeza aliikataa na kuweka amri yake.

Sio kila mtu alipenda tabia yake kwani kuna watu ambao walinufaika na mifumo hiyo mibovu na alipoikataa waliona maslahi yao kutishiwa. Na pia kuna waliopenda tabia yake ya kutokuheshimu mifumo kwa ni iliwawezesha wao kuneemeka kwa kutumia udhaifu wake katika kutaka mambo yaende bila kujali mfumo hasa mfumo unapochelewesha mambo. Huyo Ndiye Magufuli niliyemfahamu Tangu akiwa Mwanafunzi, Mwalimu, Mbunge, Naibu waziri, Waziri na Rais.

Hakuwa comformist. Udhaifu wake mkubwa ulikuwa na katika uwezo wake wa kutengeneza mifumo.Simlaumu kwani katika historia ya nchi yetu mtu pekee ambaye alikuwa fundi wa kutengeneza Mifumo alikuwa na hayati Benjamini Mkapa. Ndio. Mkapa alikuwa na uwezo wa kutengeneza mifumo, kuisimamia na kuiheshimu. Hata hivyo pamoja na uwezo wake huo hakuwana na uwezo wa kujenga nidhamu kwa wengine kuheshimu na kuisimamia mifumo. Hii ni kwa sababu watanzania tumekuwa na kasumba ya kuheshimu mifumo pale tu inapotufaa.

Naandika haya kama mtu ambaye nafuatilia sana historia ya chi yetu na watu. Kama mtu ambaye ninayo access ya kuzungumza na watu wenye nafasi nyeti serikalini na ambaye pia ninayo access ya kuzungumza na watu wa chini kabisa katika magenge na vijwe. Siandiki kwa ushabiki wala kwa ajili ya kutaka kumtukuza mtu au kumkejeli mtu bali ninaandika huku nikimlilia Magufuli.

Magufuli hakuwa adui yangu alikuwa ni rais wangu.Tangu aingie madarakani nimekuwa mkosoaji wake. Hata nisipomkosoa kwa uwazi ila ndani ya moyo kuna mambo sikukubaliana naye lakini nilimheshimu kama rais wa nchi.Nilitambua kwamba kama mwanadamu hakuwa mkamilifu. Nilitambua pia kwamba kuna uwezekano pia kwamba mimi ndio mwenye kasoro na sio yeye. Hivyo basi namjua Rais wangu.

Rais Magufuli alitaka kufanya mengi na amefanya mengi.Kwa kadiri ya uwezo na nafasi yake amefanya mengi. Ameonesha uthubutu na ujasiri ila pia kuna mengine ambayo hayakwenda sawa.Kuna ambao walimwangusha katika uongozi na kuna ambao walisababisha ashindwe kufikia malengo yake. Kuna ambao hawakumwelewa na kuna ambao walimchukia bila sababu na kuna ambao walimchukia wakiwa na sababu. Hata hivyo ukweli utabaki kuwa ukweli. Ukimtoa Nyerere Magufuli ni mmoja kati ya viongozi bora wa zama hizi. Kwa kipindi cha miaka 6 tu ameweza kuthibitisha kwamba INAWEZEKANA kuwa na ndoto kubwa na kuanza safari ya kuzifikia.

Naumia sana nikifikri kwamba Magufuli pamoja na Katibu mkuu wake KIJAZI sasa hawapo tena. Katika wilaya ya UBungo imesimama kumbukumbu,Kijazi Interchange na Magufuli International Bus Terminal. Miradi ambayo kwa hakika ni alama ya Nyakati hizi zao.

Nataka sasa niseme tu kwamba nitamlilia Magufuli kwamba hatakuwepo wakati tutakapopanda TRENI yetu ya kwanza ya SGR, hatakuwepo wakati tutakapowasha umeme wetu wa Bwawa la Nyerere. Namlilia sana Magufuli kwa sababu nilitamani sana aendelee kuwepo. NIlitamani sana atimze ndoto zake kwa taifa letu kwa nyakati zetu.

Mungu Mpokee mja wako John Joseph Pombe Magufuli na uendelee kutulinda na kutubariki Watanzania wote

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un​

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana Libarikiwa-Apumzike kwa Amani

Raha ya milele umpe Ee Bwana; Na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa aman
 
Kupigwa risasi kwa Lissu, Kupotea kwa Ben Sanane na Azory....!!
 
Basi sawa! Ndiyo hivyo tena. Ameshafariki. Tumtakie tu pumziko la milele. Sisi sote tu wasafiri. Tujiandae muda wote kwa kutenda mema badala ya kutumia nguvu kubwa, kuwaumiza wengine.
 
Basi sawa! Ndiyo hivyo tena. Ameshafariki. Tumtakie tu pumziko la milele. Sisi sote tu wasafiri. Tujiandae muda wote kwa kutenda mema badala ya kutumia nguvu kubwa, kuwaumiza wengine.
Mkuu hapo kwenye kumtakia pumziko la milele, ni kwamba:-

Mwili ukishaacha roho hapo hapo nafsi inaanza kutumikia adhabu kutokana na matendo yako ya hapa duniani.

Mwanadamu hajapewa mamlaka yoyote na mwenyezi Mungu ya kuiombea maiti (mwili) iliyopo duniani kwani kwa kufanya hivyo ni kumdhihaki mwenyezi Mungu kwani NAFSI tayari ilishanyakuliwa na ishaanza kutumikia adhabu. kwa hiyo maombi huwa hayana maana yoyote ile.

Maombi yoyote baada ya kifo huwa ni mbwemwe tu za kufurahisha na kupeana matumaini ambayo kiuhalisika hayapo katika ulimwengu wa kiroho.
 
Tutamkumbuka kwa mazuri mengi aliyotenda katika uongoz wake , mapungufu yenye yapo hayakosekani, R.I.P
 
Halijanichoma kwa lolote! Kwa sababu halinihusu. Kama ni hao mafisadi na majizi wote unao wataja, wapo humu CCM!
Mimi siko ccm , ukweli ni kwa mba majizi na mafisadi yapo kila mahali sema Jpm alifanya kaz kubwa Sana ya kuyazibiti na kuyakamata , pale alipotenda jema ni vyema tukatoa hata pongezi Mkuu , Jpm aliilinda Sana fedha ya Uma huo utabaki ukweli daima.
 
Mkuu hapo kwenye kumtakia pumziko la milele, ni kwamba...
Mkuu,kwani mbwembwe zina ubaya gani?Kwani wewe una mashaka na huruma ya Mungu na ukuu wake?Kwamba Mungu hawezi kuamua vile inavyompendeza?Mkuu Mungu atoaye Mamlaka Ndiye mkuu wa ulimwengu na Jina lake Libarikiwe.
 
Mimi siko ccm , ukweli ni kwa mba majizi na mafisadi yapo kila mahali sema Jpm alifanya kaz kubwa Sana ya kuyazibiti na kuyakamata , pale alipotenda jema ni vyema tukatoa hata pongezi Mkuu , Jpm aliilinda Sana fedha ya Uma huo utabaki ukweli daima.
Wewe hujui ulisemalo. Kwa nchi yenye mfumo dhaifu wa kiutawala/Katiba, ni ndoto kuwaondoa hao majizi na mafisadi.

Kilichotokea wakati wa utawala wake, ni kubadilisha tu aina hiyo ya majizi na mafisadi! Kutoka watu wa mfumo wa JK, kuja wale wa huyo JPM. Watu waliendelea kupiga kama kawaida.
 
Nihitimishe kwa kusema Hayati apumzike mahali pema
 
Wote tunaomboleza msiba, ila je ameacha legancy gani nyuma yake? Je, now Watanzania life styles zetu zimekuwa bora zaidi? Je, nchi imekua na amani ya ukweli? Mradi au miradi gani imekamilika ya kujisifia?

Je nchi inajiendesha kwa taratibu za utawala bora? Whats happen kwa Watanzania waliopotea kwenye mazingira ya utatanishi au kuuliwa?

Elewa President wa nchi ndiye mlinzi mkuu wa raia wake,je bado tunapendana na kuzikana bila kujali ideology za kila mmoja wetu?RiP President Magufuli .
 
Niko na huzuni kuu.

Licha ya mapungufu yake mengi, ila alionyesha uthubutu.
 
Habari na poleni sana kwa msiba.

Niseme tu kwamba wengi wanaweza kusema mengi kuhusu Msiba huu ila mimi naweza kusema Jambo Moja. Maisha ni zawadi, tuyaenzi. ujifunze kutoka katika maisha ya Magufuli; Maisha ambayo yaliacha alama...
Amina
 
Back
Top Bottom