Kwa yaliyotokea kwa Heche, Polepole, ukimya wa Gwajima, naona kabisa bora Lisu aendelee kukaa hukohuko mahabusu kuliko uraiani.
Nchi inatisha kwa sasa, na Lisu ndiye mtu pekee anayetazamiwa na wengi kuwavusha kwenye nchi ya ahadi.
Sasa tuangalie upande wa pili kama Lisu akarudi uraiani na hatimaye kutekwa, bila shaka nchi itarudi nyuma mno kwenye harakati za ukombozi maana hakutakuwa na wakuwasemea.
Wengi watazidi kujaa uoga na hatimaye wataunga juhudi tu za chama tawala hivyo vyama pinzani vitakufa rasmi na si rahisi kusimama tena labda ipite miaka si chini ya kumi.
Kama NCCR Mageuzi ilikufa, Cuf ambayo ndio ilikuwa mpinzani mkuu wa CCM leo hii kimekuwa chama dhaifu mno.
Ukiyafikiria ya Lisu utaishia kumuonea huruma tu maana uraiani na mahabusu kote si salama kwake labda aende kuishi mbali na TZ na kuacha kujihusisha kabisa na siasa.