Ninaekereka au Kuchoshwa na hili linaloendelea sasa katika Redio nyingi za Tanzania nipo peke yangu au?

Ila times wanafanya kipindi watu 2;kipindi kinanoga sanaa
 
Inshu ya kipindi kimoja kuwa na watangazaji wengi ilianzia clouds fm,na hawa majamaa vipindi vyao vilikuwa poa tu.

Tatzo limekuja kwa hz redio zingine zilizoiga utaratibu huo ndo wamefeli kabisa,imekuwa ni full makelele redion na story ziszokuwa na maana
 
Kuna wa KISS FM asubuhi wanaosoma magazeti yaani wanakera mno...bla bla kibao kuna mmoja somebody Lupokela anapenda sn porojo halafu hana details sahihi ya mambo anayochangia yaani kama wapo kijiweni hivi wanapiga kelele tu
 
Ptiuuu yaani wamezubaa Hao radio one na RFA unakuwa kama unasikiliza dhifa ya kiserikal loooo hapana go on clouds utangazaji wao hauchushi nachukia limtamgazaji eti karibu ndugu msikilizaji wetu,Ndugu mtamgazaji swagg lazima ziwemo wajameni..
Hawa unawaonea Mkuu ' Uozo ' mkubwa uko Clouds FM, EFM, Magic FM na Wasafi FM.

Kidogo Radio One na RFA kuna Nidhamu na Kujielewa fulani ila siyo kwa hawa nniliowataj
 
Viiivooo!! Love Vivoo love Tanzanja, " moja ya upuuzi huo!!
 
Hili jambo hata mimi linanikera sana, nadhani hii walianzisha clouds kwy power breakfast na jahazi japo wao walikua wachache na walikua wanapishana kwa namna ambayo kila mmoja alikua na sehemu yake au segment yake maalum.

Tatizo ninalo liona ni kwamba hawa wenye radio wamekosa ubunifu na kupenda dezo kwa kucopy anachofanya mwingine na anayecopy bila aibu anajitaba yeye ni bora zaidi na sio wasikilizaji wasifie.

Sasahivi ndio umeibuka hiyo kwy vipindi vya michezo, kila mtu mchambuzi na anajua zaidi na wamerundikana kwelikweli kwy kipindi kimoja, huwa nasikiliza wakati mwingine 88.1 kipindi cha michezo jioni ili nimsikilize Tigana Lukinja, lkn kuna mtangazaji mmoja hapo yani anapendaga aongee yeye tu muda wote na akidaka mic atabwabwaja dkk 10 peke yake hadi wenzie wanamkatisha lkn unakuta bado ana ng'ang'ania

Pia kuna tatizo la kuona fikra au mitazamo yao ndio sahihi (hii zaidi ipo clouds). Wamekua wavivu unakuta mambo kwa mfano ya kanuni...badala ya kuchimba kuipata inasemaje au kutafuta wahusika...unakuta nao wanaishia kuacha maswali na wanajiuliza tu labda itakua hivi au vile badala ya wao kama chombo kutafuta habari sahihi

In short, hadhi ya utangazaji na watangazaji pamoja na vipindi imeshuka sana na kuna wakati unaweza kubadili stesheni 3 na ukashindwa kutofautisha ni radio tofauti unless wapige jingle ya radio yao.
 
Aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM katika kipindi cha Sport Extra, Mbwiga Mbwiguke ametambulishwa rasmi kuwa mtangazaji mpya wa kipindi cha The Score Board kinachorushwa na kituo cha radio cha Times FM "Sasa sina wasiwasi, sifanyi kazi usiku kama najenga daraja" sikuhizi uwandishi wa habari hausomewi tena, Mpoki nae ni mtangazaji Efm
 
Nimeshtushwa na Taarifa hii ya Mbwiga Mbwiguke kwani hakuna Mtu ambaye kila tukikutana nae Vijiweni Kwetu alikuwa akisema kuwa kwa Utu wa Shaffih Dauda aliyemuibua akiokota Chupa za Maji Chamazi na Wema wa Marehemu Ruge Mutahaba na Urafiki wake na MD Joseph Kusaga tokea wakisoma wote Shule ya Msingi Forodhani kamwe asingeweza kuhama CMG.

Kweli nimeamini 'Fedha' humbadili Mtu.
 
Niliacha kusikiliza clouds matangazo dakika 25 content dakika 5

Naona na wasafi nimepunguza pia
 
Umenikumbusha enzi za akina Abdallah Majura na kipindi chake cha Kipusa enzi hizooo
 
Masoud Masoud redio gani mkuu?
 
Mi nafikiri ni kuwaonea tu maana hizo vipindi ndio vinapendwa na hii ni ishara kwamba tatizo ni jamii ya kitanzania sio redio
Siyo kweli mkuu, angalia comments nyungu za huu uzi, watu hawapendi kabisa ila cha kufanya ndo hawana...
 
Mkuu hata huko Clouds kipindi kama power breakfast yule Barbra au Sam sasali wana kazi gani pale?? Ilitakiwa pale awe ni Kipanya na Siza basi, wengine wote ondoa kule....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…