Ninaekereka au Kuchoshwa na hili linaloendelea sasa katika Redio nyingi za Tanzania nipo peke yangu au?

Ni kweli kabisa sasa hivi kuna hivi vipindi vya michezo sasa unakuta hao wachambuzi wako kibao na matangazo ndio usiseme.Naunga mkono hoja.
 
Ni kweli kabisa pia hao watu hawajasomea uandishi wa habari ni WAHUNI TU, serikali inatazama tu na kulaumu kwamba hakuna maadili
 
Kwanza redio nyingi hazifuati muda, kipindi cha kuanza saa 3kamili huanza na dk 10 kabisa......nadhani ni TBC pekee wanaofuata ratiba za vipindi..........
 
Kuna jamaa hawa wa3 tbc ni maongezi ya kibwege tu masaa ma3 unshangaa wapo kazini hawa??
 
Siku hizi redio chenga watangazaji wanapiga stori zisizokuwa na maana ndio maana mm nasikilizaga matangazo ya dura ya dunia tu.
 
Acha kelele wewe mwenyewe kwa jinsi unavyojitukuza kila senstensi lazima ujitaje jina lako.
 
Acha kelele wewe mwenyewe kwa jinsi unavyojitukuza kila senstensi lazima ujitaje jina lako.
Kwani GENTAMYCINE nikijitaja kila mara Wewe inakupunguzia au inakuongezea nini? Pumbavu.

Mimi ndiyo GENTAMYCINE ( alias ) Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer sawa? Mnanichukia lakini 24/7 kila muingiapo tu hapa JamiiForums lazima mtakodoa nimeandika nini au nimeanzisha Uzi gani.

Na GENTAMYCINE nitaendelea Kujipaisha sana tu hadi mkome na mkiona mnachukizwa kuliko na hii ID yangu 'Brand' kabisa tafuteni haraka Sumu ya Panya na Dawa ya Kuulia Kunguni korogeni katika Kikombe kisha mnywe Mfe kabisa sawa?

Cc: adriz
 
Hawa unawaonea Mkuu ' Uozo ' mkubwa uko Clouds FM, EFM, Magic FM na Wasafi FM.

Kidogo Radio One na RFA kuna Nidhamu na Kujielewa fulani ila siyo kwa hawa niliowataja.
Na wanaongea pumba sana, muda mwingine wanaongea matusi pia
 
Enzi za kina Misanya Bingi rip radio one, Fredwaa rip rfa. Na DJs wao ndani ya nyumba. Matangazo yapo but very controlled na contents za vipindi. Full enjoyment ya kusikiliza radio

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Vipindi vingi siku hizi ni vijiwe tu, redio station zinaajiri watu wasio na taaluma ya uandishi wa habari na utangazaji

Kuwe na bodi inayosimamia taaluma ya utangazaji na uandishi wa habari kama vile NBAA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…