Ninahisi nimebugi, nataka tuandikishiane nimpe milioni 5 ya msingi. Anipe mwanangu atakapofikisha umri

Kwa hiyo umestushwa na mahali au ?

Mbona hueleweki mkuu, kama una uwezo wa m5 za kumpa why usitoe hata 1m ya mahali ukae nae tu
 
Kuna jamaa aliambiwa mahali m3 na nusu. Halafu hana kipato kikubwa lakini katoa laki 6 imeisha usiogope wanataja tu sio lazima ulipe zote
 
Bro pole sana
For sure huyo mwanamke mwambie unapostpond kutoa mahali Hadi Hali ya mama yako itakapotengemaa alafu angalia jibu atakalo kuambia akinuna tu fukiza kabisa onsport usisubiri chochote hata akiomba msamaha timua huyo Kama tu hujamuona hajari kuhusu Hali ya mama yako for sure siku ukiugua baada ya kuoa utafia ndani.
Alafu hiyo mimba sio yako. Usije kusema hatujakuambia
 
Mtoa mada,una ujinga na upuuzi mwingi!utakufa mapema!
 
Hapa ninaguswa zaidi kwa mama, kwani mama anasumbuliwa na nini. Nijibu hata kwa PM. By the way uoaji wa sasa tunaufanyia haraka sana kiasi mwisho wake tunakuja kujuta baadae. Pole in advance.
 
Hapa ninaguswa zaidi kwa mama, kwani mama anasumbuliwa na nini. Nijibu hata kwa PM. By the way uoaji wa sasa tunaufanyia haraka sana kiasi mwisho wake tunakuja kujuta baadae. Pole in advance.
Asante nitakujuza pm kiongozi
 
Kuhusu kuuguza hakuna shida kiongozi huko wala hitajio sio pesa Huko hitajio ni Mwenyezi Mungu amponye tumepambana sana kwa miaka minne alikua anapata unafuu ila now naona hali imechange kabisa.

Pamoja na hilo bado wewe na huyo mpenzi/mchumba wako mnatakiwa focus yenu yote iwe kwa mama anayeumwa mpaka atakapopata ahueni au Mola akimpenda ndiyo mrudi kwenye hayo mengine, kwani mna haraka gani?? Kama alivyodokeza mdau hapo juu hiyo haraka haraka ya huyo demu wako yeweza kuwa anataka kukuingiza kingi kabla hujaujua ukweli.
 
Kwani una shida ya uzazi? Una sababu ya msingi na usiri sana pole sana kwaivo mtoto awe wako, awe wa mwenzio iyo haina shida! Lazima uteseke kama alishajua shida ako ni mtoto bila kujali ni wako au la
 
Mkuu mpe million moja akalee mimba then akijifungua utalea mtoto million 5 ni nyingi mno kumbuka mama ni mgonjwa
 
IROKOS
 
IROKOS hata yeye ana araka ya kupata mtoto haijalishi hahaha
 
Ajiridhishe mtoto ni wake na akati anakwambia ana sababu na siri inayosababisha kutaka kupata mtoto?? We huoni yeye hajalishi mtoto awe wake au wa mhuni mmoja anachotaka ni mtoto!
 
 
Habari, Nimesoma maelezo yako na kuyaelewa ifuatavyo:-

Mosi, Ulifiwa na mke/mpenzi wako akiwa na kichanga tumboni hivyo kwa sasa huna mtoto lakini unahitaji mtoto kwa hali yoyote ukizingatia umri unakwenda na wenzio wenye umri kama wako wana watoto.

Pili, Uwezo wako kiuchumi siyo mbaya (uchumi wa kati) hivyo pesa ya mambo madogo madogo haikupigi chenga ikiwepo na ya kutuma nyumbani ambapo unauguza mama yako.

Tatu, Umepata mpenzi wa kijaluo mwenye mtoto wa umri wa miaka tisa (9) na yeye ana hamu ya kuolewa na kwa kuwa umeonyesha uwezo wa kumlea mwanae anataka umuoe haraka bila kujali unayoyapitia kwa sasa.

Ushauri wangu, Kwanza nakushukuru kwa kukiri kuwa umebugi (umekosea) Sasa unatakiwa kurekebisha makosa kwa kufanya ifuatavyo. Kuoa siyo jambo la kukurupuka, subiri kwanza ajifungue wakati mkiendelea kumuuguza mama yenu mzazi, pili tumia muda mrefu kumchunguza unayetaka kumuoa maana kwa mujibu wa maelezo yako (kama haumsingizii) inaonyesha hajali shida zako.

Wanawake wa Vyuoni (hasa vyuo vikuu) wanapitia mengi na wanajua mengi, sasa huyo wako amegundua una udhaifu hivyo anatumia udhaifu huo kukuendesha anavyotaka yeye. Simama kama Mwanaume unatakiwa kuwa mpangaji na muamuzi wa mwisho yeye abakie kuwa mshauri na asikupangie (au unaogopa degree yake!!😀😀).

Kwa maoni ya mmoja wa wadau ni kuwa Mwanamke mwenye mtoto (Single mother) aliyepata mtu wa kumlelea mwanae na kumuahidi ndoa si rahisi kumuacha na ukijaribu unaweza kulishwa hata vyura na mijusi na sisi wote ukatuona mmbwa. Hivyo hata ukitaka kumuacha ujipange usikurupuke anaweza kuuuwa au kukufanya kichaa.

Na ninavyohisi ameshawaambia ndugu zake kuhusu udhaifu wako hivyo nao wanakupelekesha tu. Kuhusu fedha hiyo milioni 5 usimpe maana atatumia itaisha kisha atakuja tena kwa ukali (maana ameshakuona poyoyo). KWA UJUMLA UNATAKIWA KUSIMAMA KIUME TENA KWA KUMAANISHA SIYO KUIGIZA.
 
Pole sanaa tuko katika zama za ajabu mno.
 
Kwahiyo unafikiri ukimpa hiyi 5mil ndio hatakuomba tena pesa? Tena uikabidhi na wazazi wake wakiwepo! Watagawa itaisha hakuna biashara itakofanyika na watakugeuza saccos kupita mtoto atakaye zaliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…