Ninahitaji kufanya kilimo cha Papai katika eneo la Mkuranga

NALO LITAPITA

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
333
Reaction score
90
Wanabodi habari ya majukumu!.
Ninakuja kwenu na wazo langu na maombi kadhaa kwenu juu ya wazo hili.

Ninahitaji kufanya kilimo cha Papai katika eneo la Mkuranga.Ninapanga kuanza kilimo hiki kwa kuanza na heka moja kwanza.

Katika kutaka kujifunza nimegundua mambo kadhaa kuhusu kilimo hiki,ikiwa ni pamoja na kwamba kilimo hiki ni sharti uwe na uhakika wa upatikanaji wa maji kwa kipindi cha mwaka nzima,katika kusomasoma nikaona eneo la Mkuranga likitajwatajwa kuwa aridhi yake inakidhi kilimo hiki.Kwakuw ninaishi Dar es Salaam nimeona pia kwangu itakuwa nafuu hata kutembelea mradi.

Tafadhali naomba nisaidiwe mambo yafuatayo;

I) Katika wilaya ya Mkuranga ni eneo/maeneo gani hasa ambayo ninaweza kupata shamba la hekari moja kwa bajeti ya 500,000 mpaka 700,000 shamba ambalo halituhamishi maji na ambalo liko karibu na chanzo cha maji hususani mto husiokauka kwa kipindi chote cha Mwaka?.

ii) Kama kuna mtu anafahamu eneo lolote Mkuranga ambalo kilimo hiki cha Papai kinafanyika angalau kuanzia nusu heka na kuendelea anisaidie kunielekeza/ mawasiliano yao nipate kwenda kujifunza zaidi kabla ya kuanza kutekeleza mradi wangu huu.

iii) Kama kunamtu anafahamu mtu anayeuza shamba lenye vigezo nilivyovitaja hapo juu tafadhali aniunganishe.

iv) Ushauri wowote muhimu kutoka kwa yeyote mwenye mwanga na ulimaji wa Papai Tafadhali anishauri kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi
 
Mkuu nakushauri utembelee huko ukae hata siku tatu utafute shamba taratibu ukiweza pitia ofisi za vijiji ili upate taarifa sahihi kuepusha utapeli wowote.

Kama ulivyoainisha hapo juu papai inahitaji maji so utalazimika kupata maji kwanza yaani kuchimba kisima cha uhakika pamoja na kuweka tank kabisa, uwe na generator au solar ya kuvuta maji kupeleka kwenye tank.

Hakikisha shamba lako umeweka fence ya kuzuia mbuzi, ng'ombe kuepusha usumbufu kwenye papai zako.

Uwe na kijana wa kukaa shamba full time kumwagilia na kutazama shamba kwa ujumla.

Ukikamalisha hayo hapo juu utahitaji maandalizi ya shamba tayari kwa kupanda miche yako ya papai hapo wadau tupo...mimi nawafahamu wauzaji wa miche ya papai kama uko serious niaku connect.
 
Asante sana kwa ushauri huu Mkuu,Bei za uchimbaji wa visima unarange bei gani?
 
Safi sana. Ukianza kulipa kama ukihitaji dawa ya kilimo nipo hapa, nauza Supergro nzuri sana sana katika mazao hasa mapapai yani utaona matokeo yake ni mazuri sana. Matunda idadi yake mpaka size ya tunda na ladha itakuwa nzuri sana. Na ni organic, kwahiyo ni free from chemicals, na kuhusu kuchimba kisima namba yangu 0766317197 jirani yangu anachimba kisima ngoja nimuulize then nitakucheki for feedback
 
Mkuu.... Mimi naomba msaada hapa. Nimepanda mapapai ya mbegu fupi.... miche 20 nyumbani kwangu. Mapapai yale yameanza kutoa maua na miche 16 ni mapapai DUME. SuperGro Nimetumia..... Imestawi kweli kweli.... Hii mipapai DUME naifanyia nini ..... Hakika sipati picha unapopanda robo ekari na unakutana na scenario kama yangu. Naomba msaada kwenye hili.
 
Hiyo mbegu ulinunua dukani ikiwa kwenye pakti au ulinunua miche? Kama ukinunua mbegu dukani kwenye chanzo cha uhakika basi huwezi kupata miche dume, ila kama ulinunua miche hapo ni Rahisi kupata miche dume mpaka asilimia 50 kwani huenda aliekuuzia miche alitumia kuchuma papai kutoka mtini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chukua magunzi Kisha funga kwenye hiyo mipapai dume
 
Wanaoyajua mashamba Mazuri mkulanga hawapo humu jf ingia field kaa wiki Nzima. Hakikisha 95% ya muda upo field
 
Wakulima wa JF bana, sasa unatafuta shamba hapa JF ? ulitakiwa ulete uzi huu ukiwa huko huko field braza. Mkuranga ni Km 40 approx nenda.

Kilimo cha papai ni kizuri kama utazingatia vigezo na masharti - kwa ulivyoandika hapo yaonekana una habari sahihi - Best wishes.
 
Safi sana. Ukianza kulipa kama ukihitaji dawa ya kilimo nipo hapa, nauza Supergro nzuri sana sana katika mazao hasa mapapai yani utaona matokeo yake ni mazuri sana. Matunda idadi yake mpaka size ya tunda na ladha itakuwa nzuri sana. Na ni organic, kwahiyo ni free from chemicals, na kuhusu kuchimba kisima namba yangu 0766317197 jirani yangu anachimba kisima ngoja nimuulize then nitakucheki for feedback
kisima namm mdau nahitaji
 
Hiyo mbegu ulinunua dukani ikiwa kwenye pakti au ulinunua miche? Kama ukinunua mbegu dukani kwenye chanzo cha uhakika basi huwezi kupata miche dume, ila kama ulinunua miche hapo ni Rahisi kupata miche dume mpaka asilimia 50 kwani huenda aliekuuzia miche alitumia kuchuma papai kutoka mtini

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilinunua miche ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom