NALO LITAPITA
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 333
- 90
Wanabodi habari ya majukumu!.
Ninakuja kwenu na wazo langu na maombi kadhaa kwenu juu ya wazo hili.
Ninahitaji kufanya kilimo cha Papai katika eneo la Mkuranga.Ninapanga kuanza kilimo hiki kwa kuanza na heka moja kwanza.
Katika kutaka kujifunza nimegundua mambo kadhaa kuhusu kilimo hiki,ikiwa ni pamoja na kwamba kilimo hiki ni sharti uwe na uhakika wa upatikanaji wa maji kwa kipindi cha mwaka nzima,katika kusomasoma nikaona eneo la Mkuranga likitajwatajwa kuwa aridhi yake inakidhi kilimo hiki.Kwakuw ninaishi Dar es Salaam nimeona pia kwangu itakuwa nafuu hata kutembelea mradi.
Tafadhali naomba nisaidiwe mambo yafuatayo;
I) Katika wilaya ya Mkuranga ni eneo/maeneo gani hasa ambayo ninaweza kupata shamba la hekari moja kwa bajeti ya 500,000 mpaka 700,000 shamba ambalo halituhamishi maji na ambalo liko karibu na chanzo cha maji hususani mto husiokauka kwa kipindi chote cha Mwaka?.
ii) Kama kuna mtu anafahamu eneo lolote Mkuranga ambalo kilimo hiki cha Papai kinafanyika angalau kuanzia nusu heka na kuendelea anisaidie kunielekeza/ mawasiliano yao nipate kwenda kujifunza zaidi kabla ya kuanza kutekeleza mradi wangu huu.
iii) Kama kunamtu anafahamu mtu anayeuza shamba lenye vigezo nilivyovitaja hapo juu tafadhali aniunganishe.
iv) Ushauri wowote muhimu kutoka kwa yeyote mwenye mwanga na ulimaji wa Papai Tafadhali anishauri kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi