Ninahitaji Mwekezaji kwenye biashara yangu ya uzalishaji wa vipodozi

TRA hawawasumbui na hiyo systm?
 


Wee acha, thamani ya small industry is 20 mil, alafu mtu awekeze 10 mil, umpe shares 10%, umesomea uwizi huu wapi? Hesabu hata kidogo hujui au unajua umeamua kuficha, na uwekezaji sio eti mtu akiamua kutoa hela zake say 5 yrs from now na capital yenu imekuwa say to 200 mil eti utampa 10 mil yake, sio hivyo, utampa % shares ya value ya hiyo 200 mil ya wakati husika…

Hesabu yako inatakiwa kuwa hivi…

Total capital itakuwa 20 + 10 = 30 mil


So 10 mil shares out of 30 mil is 10 divide by 30

That is 33% of total shares….

So mtu akiwekeza 10 mil, atapata 33% of total shares

Sasa siku akimua kutoka katika biashara say 5 yrs na biashara imekuwa na kufikia 200 mil

Sasa utampa 33% x 200 = 66 mil

So akiweka leo mil 10 yake siku anatoka na miaka kadhaa mbele na biashara imekuwa to 200 mil, mwekezaji atapata 66 mil, sio 10 mil

Hivyo, uwekezaji usifanye kimazoea tu na bila kujua hesabu sahihi za uwekezaji, maana utadhulumu watu.
 
Yaani nimeshageuka mwizi? Naomba futa hiyo kauli ili twende vizuri

Nipo tayari kujifunza lakin sio kwakuniita MWIZI
 
Mi sijui hesabu za biashara na uchumi.
Ila niliona kwasababu wewe umepambania brand basi hiyo 10% ya annual profit iwe kwa mwaka wa kwanza then m waka unaofuata ipande iwe 15% kama asipojitoa mwekezaji.
Lakini je mtaji ukikua hiyo milioni 10 yake na yeye si inakuwa kwa asilimia kadhaa?

Kama miaka ikienda na mwekezaji akabaki na 10 milioni si itakuwa chuma ulete?

Lakini pia security ya mwekezaji / bima ya uwekezaji wake.

Ikitokea mambo yamebuma kwenye biashara " mtamuachaje" mwekezaji na keshatia 10 milioni yake?
 
Mkataba ni kwa mwaka mmoja kwanza kwani ndio mara yangu ya kwanza kufanya hili jambo so bado nipo kwenye kujifunza pia na kupata uzoefu wa namna biashara zinavyoenda na ndio maana nikatoa uhakika wa hela yako kutokutetereka endapo biashara ikiyumba kwa kipindi Cha mkataba



Nipo tayari kujifunza zaidi na zaidi ndugu yangu
 
Hii 10% sio mbaya hata benki mtu haipati hii faida akiweka hela mwaka mzima kwa 10m.

Pia wewe umeweka security kwa investors(yaani hapotezi lolote hata iweje).

Ila kwa investors mwenye ku take risk anaona hii 10% ndogo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…