Ninaishi kwangu (nimejenga) ila sina furaha

Ninaishi kwangu (nimejenga) ila sina furaha

Kama umejenga kwa hela za urefu wa kamba nakuambia hutakuwa na furaha maisha yako na mwisho wa siku kifo kibaya tu

Angalia wote waliokua wanaturingishia ma V8 leo wako wapi?

Sasa na wewe utajumuika nao tu maana mkipata huwa hamkumbuki hata sadaka halafu unataka uwe na furaha
Kuna masikini choka mbaya lakini tabasamu lao sio la dunia hii
 
Furaha ni zaidi ya materia thing's na wewe ulijiaminisha ukijenga utakuwa na furaha kumbe hola, jifunze kutafta peace of mind na furaha ya ndani kuliko kuwekeza furaha kwenye material things, above all usisahau Sala na kazi bila hivo furaha itazidi kupaa
 
Imeandikwa;

“ tafuteni kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambapo hakuna atakaemuona Mungu pasipo huo”

Kaombe msamaha kwa ulowakosea,

Watangazie msamaha walokukosea,

Epuka chuki, ghadhabu, hasira, uchungu , wivu, husuda n.k

Lipa madeni ya watu.

Ulowazulumu warudishie vitu vyao

Jifunze Neno la Mungu na kulipokea moyoni mwako.

Mwamini Roho Mtakatifu na umpe nafasi moyoni mwake aishi.

Mojawapo ya tunda la Roho Mtakatifu ni furaha.
 
Back
Top Bottom