Ninakubaliana na Rais hakuna vita ngumu kama ya uchumi, tushikamane

Ninakubaliana na Rais hakuna vita ngumu kama ya uchumi, tushikamane

dndagula

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
1,602
Reaction score
1,650
Maisha ni uchumi na uhuru wa kweli ni uchumi. Wale waliosomea siasa Uchumi yaani political Economy wanajua uhusiano wa siasa na uchumi. Pia wanafahamu uhusiano wa binadamu juu ya uzalishaji.

Kimsingi mapambano yoyote ya kisiasa msingi wake ni uchumi ni nani apate nini na kwa wakati gani. Taifa letu linapita kwenye kipindi kigumu kutokana na jitihada za Rais wetu kuleta mageuzi ya kiuchumi ili kulifanya taifa kujitegemea na kwa kulinda raslimali zake.

Hivyo vita vya ndani na nje ya nchi kama taifa na Rais wetu ni matokeo ya jitihada hizo na matamanio ya kundi la ndani ya nchi kushirikiana na mataifa nyonyaji nje.

Kihistoria kuanzia wakati wa biashara ya utumwa, ukoloni na sasa ukoloni mambo leo Afrika imekuwa mhanga wa ukandamizwaji na mataifa makubwa kunufaika na raslimali ipatikanayo Afrika.

Fika Ulaya ujionee ilivyojengwa kwa raslimali zetu na biashara ya utumwa enzi hizo. Mataifa haya hayataacha kupigania kututawala kiuchumi yakijua raslimali iliyopo ni muhimu kwa mustakabali wa mataifa hayo.

Kelele tunazosikia kwenye siasa ndani na nje ya nchi ni vita ya kiuchumi. Hivyo watanzania tushikamane na Rais wetu dhidi ya unyonyaji huu.

Aidha vyombo vya dola, serikali na mifumo yote haina budi kujengwa upya kwa mwelekeo wa falsafa ya kizalendo na kujitegemea ili kukabiliana na vita hii ambayo hujitokeza katika sura na mbinu mbalimbali zisizo na kikomo.
 
Kwa hiyo vita ya kiuchumi ndio inawaelekeza muue watu, mteke, muwabambikie makesi, mpole uchaguzi, muengue wagombea wa upinzani na mpitishe wa kwenu bila kupingwa?

Kwa akili hizi Bora wazungu wawanyooshe kweli ili mjifunze kueshimu utu na ubinadamu wa wengine
 
Kushirikiana na wezi na dhulumati wengine dhamira zinagoma kabisa jombi.

Je, kuna mpango angalau wa kubadilika?
 
Tuko kwenye vita ya uchumi demokrasia inatumika kama mwamvuli tuu
 
Hata enzi za Nyerere kulikuwa na mapambio ya hivi hivi. Tulikuwa tunaimba sifa za Nyerere kukata mirija ya wakoloni nk, ila tuliishia kuvaa viraka, bidhaa kama sukari, sabuni, mafuta ya kupikia nk viligeuka kuwa anasa. Wakenya tuliokuwa tunaambiwa wanaendeshwa na mabeberu wakawa wanatuchora tu kwa kujipaka mafuta ya kupikia.

Kosa lile lile linajirudia miaka 40 mbele! Hivi sasa cement bei ni kizungumkuti, mafuta ya kula na sukari bei juu na zinaendelea kupanda, tunaingizwa kwenye umaskini wa lazima kwa propaganda za uzalendo uchwara.
 
Achana nao vilaza hawa. Wanafikiri hii ni miaka ya 70 watawadanganya watu kwa propaganda zao uchwara
 
Back
Top Bottom