Lyaka Mlima Jr
JF-Expert Member
- Mar 24, 2020
- 361
- 521
Uchumi wa Marekani kweli ni wa kuja kupigana vita vya kiuchumi na nchi ambayo inasaidiwa kujengewa matundu ya vyoo?Nchi ambayo ina import wembe kwamba bado haina techinolojia ya kuunda wembe, nchi inayo import toothpick.Maisha ni uchumi na uhuru wa kweli ni uchumi. Wale waliosomea siasa Uchumi yaani political Economy wanajua uhusiano wa siasa na uchumi. Pia wanafahamu uhusiano wa binadamu juu ya uzalishaji.
Kimsingi mapambano yoyote ya kisiasa msingi wake ni uchumi ni nani apate nini na kwa wakati gani. Taifa letu linapita kwenye kipindi kigumu kutokana na jitihada za Rais wetu kuleta mageuzi ya kiuchumi ili kulifanya taifa kujitegemea na kwa kulinda raslimali zake.
Hivyo vita vya ndani na nje ya nchi kama taifa na Rais wetu ni matokeo ya jitihada hizo na matamanio ya kundi la ndani ya nchi kushirikiana na mataifa nyonyaji nje.
Kihistoria kuanzia wakati wa biashara ya utumwa, ukoloni na sasa ukoloni mambo leo Afrika imekuwa mhanga wa ukandamizwaji na mataifa makubwa kunufaika na raslimali ipatikanayo Afrika.
Fika Ulaya ujionee ilivyojengwa kwa raslimali zetu na biashara ya utumwa enzi hizo. Mataifa haya hayataacha kupigania kututawala kiuchumi yakijua raslimali iliyopo ni muhimu kwa mustakabali wa mataifa hayo.
Kelele tunazosikia kwenye siasa ndani na nje ya nchi ni vita ya kiuchumi. Hivyo watanzania tushikamane na Rais wetu dhidi ya unyonyaji huu.
Aidha vyombo vya dola, serikali na mifumo yote haina budi kujengwa upya kwa mwelekeo wa falsafa ya kizalendo na kujitegemea ili kukabiliana na vita hii ambayo hujitokeza katika sura na mbinu mbalimbali zisizo na kikomo.
Tuna Techinolonia gani tunayo watishia Marekani au EU? si tunatumia Internet yao? hizi Facebook si za kwao?
Si tuna vaa mitumba kutoka kwao? how come tuvae mitumba yao then tuseme tuna vita na wao?
Ni hilo Bwawa la umeme? au Flyover ya Ubungo? ndo vitu tishio kwa Wazungu?
Katika Majimbo yote ya Marekani hakuna hata moja ambalo tunalikaribia na hatutarajii kulikaribia hata kwa miaka 200 ijayo, Jimbo kama California GDP yake ni kubwa kuliko nchi zote za Africa combined.
How come nchi ambayo inazidiwa pato na makampuni ndo ije ipigwe vita? BP wana turn over kubwa kuliko GDP yetu.
Marekani ana vita ya Kiuchumi na nchi kama China, EU na hao wakina Russia ila si chi kama Tanzania ambayo bado techinolojia ya kuuda pini bado hatuna.
Ulaya wana vita vya kiuchumi na nchi kama China, Russia na kadhalika na hata hivyo sio vita bali wanapambana kuhakikisha wanafaidika, China inapambana kuhakikisha inafaidika na EU na EU nao hivyo hivyo.
CCM wakisema tuna vita vya kiuchumi na nchi kama Kenya nitawaelewa ila sio hao ambao huwa wanatujengea vyoo vya shule, wanatupatia ARV, wanatupa vyandarua.
Hizi Propaganda ni za kijinga na kuna wajinga wameaminishwa na wameamini, ni bahati mbay nchi ina kiwango kikubwa cha watu wasio weza kureason.