Ninatumia nafasi hii kukukaribisha Dr.Ndalichako hapa JF huku nikizingatia ufinyu wa wakati wako ambapo nina uhakika kabisa kuwa utakuwa unabanwa na majukumu mbalimbali kuanzia ya kikazi hadi ya kifamilia.Hili ninalielewa fika.
Pamoja na hayo ningefurahi sana Dr. kama utachukua sehemu ya wakati wako na kuungana nasi hapa angalau masaa mawili matatu kwa wiki ili utufaidishe katika yale ambayo umebahatika kuyafahamu na kuyaelewa.Ninatumia neno kubahatika kwa sababu si wengi katika Tanzania hii ambao wameipata fursa uliyoipata! na kwa sababu zisizoweza kuzuilika sikuwahi kukupongeza wakati ulipopata fursa hii adhimu lakini sasa hivi pokea pongezi zangu za kuukwaa Udokta.
Kiumri nafikiri nitakuwa ni mdogo kwako lakini hapa JF kuna watu wazima na kama waswahili wasemavyo "penye wazee hapaharibiki jambo" ikitokea kupinda kwa kauli za baadhi yetu basi watu wazima wapo hapa wa kuyarekebisha mambo, hivyo suala la kufikiria kuwa utavunjiwa hishma yako liondoe kabisa mawazoni mwako.
Binafsi nimetokea katika jamii ya watu wenye sifa ya ukarimu na kikawaida huwa tunawakirimu wageni wetu vizuri sana.
Karibu JF Dr.Ndalichako karibu sana na jisikie upo nyumbani.
Karibu tena Dr.