Ninakukaribisha JF Dr.Joyce Ndalichako.

Ninakukaribisha JF Dr.Joyce Ndalichako.

Sideeq

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2009
Posts
2,422
Reaction score
434
Ninatumia nafasi hii kukukaribisha Dr.Ndalichako hapa JF huku nikizingatia ufinyu wa wakati wako ambapo nina uhakika kabisa kuwa utakuwa unabanwa na majukumu mbalimbali kuanzia ya kikazi hadi ya kifamilia.Hili ninalielewa fika.

Pamoja na hayo ningefurahi sana Dr. kama utachukua sehemu ya wakati wako na kuungana nasi hapa angalau masaa mawili matatu kwa wiki ili utufaidishe katika yale ambayo umebahatika kuyafahamu na kuyaelewa.Ninatumia neno kubahatika kwa sababu si wengi katika Tanzania hii ambao wameipata fursa uliyoipata! na kwa sababu zisizoweza kuzuilika sikuwahi kukupongeza wakati ulipopata fursa hii adhimu lakini sasa hivi pokea pongezi zangu za kuukwaa Udokta.

Kiumri nafikiri nitakuwa ni mdogo kwako lakini hapa JF kuna watu wazima na kama waswahili wasemavyo "penye wazee hapaharibiki jambo" ikitokea kupinda kwa kauli za baadhi yetu basi watu wazima wapo hapa wa kuyarekebisha mambo, hivyo suala la kufikiria kuwa utavunjiwa hishma yako liondoe kabisa mawazoni mwako.

Binafsi nimetokea katika jamii ya watu wenye sifa ya ukarimu na kikawaida huwa tunawakirimu wageni wetu vizuri sana.

Karibu JF Dr.Ndalichako karibu sana na jisikie upo nyumbani.
Karibu tena Dr.
 
alishajiunga au unamshawishi ajiunge? Nakubaliana na wewe kwamba huyu ni mtu muhimu sana hapa, atasaidia watu kuelewa mengi haswa majukumu ya taasisi yake ambayo imekuwa ikitupiwa lawama matokeo yanapokuwa mabovu bila kuzingatia ukweli kwamba siyo kazi ya taasisi hiyo kufundisha bali kupima kwa mujibu wa syllabus.
 
alishajiunga au unamshawishi ajiunge? Nakubaliana na wewe kwamba huyu ni mtu muhimu sana hapa, atasaidia watu kuelewa mengi haswa majukumu ya taasisi yake ambayo imekuwa ikitupiwa lawama matokeo yanapokuwa mabovu bila kuzingatia ukweli kwamba siyo kazi ya taasisi hiyo kufundisha bali kupima kwa mujibu wa syllabus.
Sina taarifa za kujiunga kwake hivyo ninamshawishi ajiunge.
 
Ajafika bado tu?
Usiku mwingi huu halafu pengine anahitaji kuishauri familia kabla ya kujiunga, pengine anahitaji muda wa kufikiria n.k vilevile binafsi mimi mkaribishaji ninampa na kumkubalia mgeni wangu kila aina ya udhuru.

Tumia muda wako Dr.
 
Naungana na wenzangu katika kumkaribisha dr. Ndalichako,namuheshimu sana huyu mama katika masuala ya kiutendaji, na amekuwa akinifanya nijenge imani wa wanawake kuwa na wao wanaweza. Hongera sana mama.

Napenda pia kutoa ushauri wangu kwa uongozi wa JE, wahakikishe watu wote ambao ni viongozi kwenye jamii zetu ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao wapo humu, basi wawe verified mambers, inakuwa vyema zaidi.
 
waje wengi huku jf ili twende sawa
wamejua ni nini maana ya jf, wakaribisheni tupambane kwenye hoja.
 
Kashaijabutege nimeipenda sana hii sahihi yako
"NAKUSHUKURU MUNGU KWA KUIADHIBU CCM MCHANA KWEUPE, BABA NINAKUOMBA UZIDI KUWAUMBUA, KWA KUYAWEKA WAZI MCHANA WANAYOYAFANYA USIKU. OMBI KWA MUNGU: MUNGU WEWE NI MWEZA WA YOTE, NA SIKU ZOTE UNAYASIKILIZA MAOMBI YA WAKUCHAO, NAKUOMBA UKAFUNGE NGUVU ZA GIZA ZINAZOINYEMELEA M4C; NA UVUNJE MIPANGO YOTE YA MASHETANI WALIOPO NDANI YA CHADEMA. AMINA"

"Mbabe" wa Nyambali Nyangwine.
 
Last edited by a moderator:
Hii tabia siipendi. Mbona mimi sikukaribishwa!

Hii ni aina utoto wa kutajana majina.
 
ninatumia nafasi hii kukukaribisha dr.ndalichako hapa jf huku nikizingatia ufinyu wa wakati wako ambapo nina uhakika kabisa kuwa utakuwa unabanwa na majukumu mbalimbali kuanzia ya kikazi hadi ya kifamilia.hili ninalielewa fika.

Pamoja na hayo ningefurahi sana dr. Kama utachukua sehemu ya wakati wako na kuungana nasi hapa angalau masaa mawili matatu kwa wiki ili utufaidishe katika yale ambayo umebahatika kuyafahamu na kuyaelewa.ninatumia neno kubahatika kwa sababu si wengi katika tanzania hii ambao wameipata fursa uliyoipata! Na kwa sababu zisizoweza kuzuilika sikuwahi kukupongeza wakati ulipopata fursa hii adhimu lakini sasa hivi pokea pongezi zangu za kuukwaa udokta.

Kiumri nafikiri nitakuwa ni mdogo kwako lakini hapa jf kuna watu wazima na kama waswahili wasemavyo "penye wazee hapaharibiki jambo" ikitokea kupinda kwa kauli za baadhi yetu basi watu wazima wapo hapa wa kuyarekebisha mambo, hivyo suala la kufikiria kuwa utavunjiwa hishma yako liondoe kabisa mawazoni mwako.

Binafsi nimetokea katika jamii ya watu wenye sifa ya ukarimu na kikawaida huwa tunawakirimu wageni wetu vizuri sana.

Karibu jf dr.ndalichako karibu sana na jisikie upo nyumbani.
Karibu tena dr.

siamini kama atakuja. Akija swali la mwanzo. Necta umekifanya kigoda cha kanisa kwa kuwafelisha waislam na kuwapendelea wakiristo. Swali kwanini umeamua kutumia njia kwa watz wenzio?
 
Back
Top Bottom