Smile kwanza ni kweli huishi vituko, hiyo siyo hoja ya kubishaniwa.
Ok, nimejitahidi sanakufuatilia uzi na kugundua machache,
1.0 Hujaweka wazi msimamo wa jamaa kama anataka kukuoa au hataki? Halafu sijaona sehemu yoyote katika post yako ukionyesha kama umepropose ndoa na jamaa akareject zaidi ya kuonyesha jamaa kaomba mzigo na wewe bado humuamini kama ukimpa atasepa au la?
Kwa mantiki hiyo bado nina mashaka na wewe kama unahitaji ndoa au unahitaji mtu wa mahusiano lakini ambaye hatakuumiza.
2.0 Aidha umejisifia kuwa kitu ni OG, inalipa n.k Kwangu huu nauona ni uzushi kwani huwezi kujisifia mwenyewe zaidi ya kusifiwa hasa na mtumiaji. Mpaka hapo hujatupa list ya nyuma kama ulishawahi kuwa na mahusiano yoyote zaidi ya huyo jamaa aliyekuwa mpenzi wako kisha akakuacha. Ingefaa ukatoa ili kufanya comparisons ya hao wa nyuma kama walikuwepo, huyo wa kati aliyekuacha na huyu wa mwisho kwa nini hapati tunda?
Majibu mengi na mazuri yangetoka kwao kwa nini walikuacha hasa huyu ambaye ulimpa na kukuumiza kwa kukuacha. Unaweza kuta hao jamaa labda malalamiko yao yanafanana labda kitu haivuti, hujitumi mamaa, hujui kumpokea mwanaume n.k lakini simananishi upo hivyo.
3.0 Unajua wanaume hawaachi wanawake only for the sake of ngono. Totaly No. Mwanaume anaweza kukufuatilia kwa muda mrefu sana lakini pindi mahusiano yenu yakifikia kuwa wapenzi basi mtu huanza kufanya integration of other factors apart from sex hasa kama lengo lake si kufurahia kukumega kwa siku moja moja.
Akigundua hakuna combination nzuri baina ya other factors na sex relation basi gap hiyo ndiyo inayoweza kuunda kuachwa. Ngoja ni clarify. Hebu fikiria mwanamke mzuri lakini na keshatoa penzi na mwanaume anagundua labda uelewa wake wa mahusiano anaona umeisha kwenye ngono tu, anaweza kuona hutamfaa mbeleni. Mfano mwanamke anatakiwa aonyeshe akiolewa suala la kupenda ndugu siyo shida na halitakwa shida. Other complications hasa life style, kuna wengine ni wanawake wa kutumia na jamaa in future anahisi hataweza kumantane.
Kwa hiyo zipo sababu nyingi sana zinazopelekea kuachwa nje ya kutompa mpenzi wako ngono, na ndiyo maana wanandoa wanatengana au wapenzi licha ya kupeana tunda.
4.0 Katika maisha hakuna hedging ya 100%, namananisha eti useme fulani nikimpa hataniacha na fulani ataniacha. Tunachofanya kuwa marisk taker. Kinachotufanya tukubali au tuache ni peace of mind. Ikiwa katika kipindi hicho chote hujaonyesha wasiwasi wa kama si mwaminifu basi ana haki ya kupewa hiyo kitu. Kwa nini?
Kiukweli ulimwengu wa sasa umetofautiana sana na ule wa kale, zamani wanawake walikuwa wanjisitiri sana na hata utamaduni wetu ulipewa heshima. Lakini siku hizi hali imetofautina na kuunda hali ya matamanio kuwa kubwa sana.
Sasa, katika mahusiano kuwa na mpenzi halafu hamna ngono ni kama KUWA NA MWAVULI KATIKA MVUA KISHA MWAVULI HUO HAUKUNJUKI INA MAANA HAUNA MSAADA WA KUTOKUKUFANYA USILOWE. Ni kweli, kwa nini nikutongoze wewe kisha niishie kutaka kutembea na wanawake wengine wakati wewe upo? Endapo nitafanya hivyo moja kwa moja nitakuwa nimeunda dharau kwako hata kama usipojua.
Jamani yapo mengi ya kujadili lakini suala la kuuliza mtu eti nimpe au nisimpe hilo kwangu haliniingii akilini, nadhani huja automatically hasa mhusika anapotimia akili kwa kuona hakuna viashiria vibaya siku za usoni.
Kwa mantiki hiyo kumnyima jamaa niliyoiita haki yake katika poluted environment si haki, hiyo ni kwa maono yangu.
Pls Smile take few minutes to smile on this post.