Ninani basi aliyewaambia wabongo pilau lazima ipikwe siku ya sikukuu?

Ninani basi aliyewaambia wabongo pilau lazima ipikwe siku ya sikukuu?

Ndio pilau haifanani na wali mweupe na kwakuwa sikukuu ni siku special lazima tupike pilau,otherwise una sababu zako zingine
Binafisi huwa naona pilau haina u special wowote ule. Pia sio mdau wake. sina sababu nyingine na ahsante kwa jawabu lako
 
We sababu kubwa ni kwamba hupendi pilau hilo tu,kama ungekuwa mdau basi usingeuliza
Watoto wako si wanapenda lakini?
Kuna vitu vyingi tu sipendi wala sio pilau tu swali langu ni kipi chaa maana zaidi hadi pilau iwe special siku za sikukuu ama sherehe? ndio maana nikasema hata ukisema labda viungo vyake ni ghali sana jibu ni hamna tofauti yake ni ndogo tu na wali wa kawaida kiasi kwamba mtu akiamua siku yoyote ile anapika lakini kuwa maaalumu siku ya sikukuu tu ndo huwa najiuliza sana.

Kama umenisoma vizuri nikiwa nimekaa watoto walianza kutambiana kila mmoja akimtambia mwenzeke kwao kuna pilau hii ina maana siku za kawaida haipikwi na haijazoeleka kupikwa ndio maana kwa watoto inaonekana ni chakula ch msimu
 
Back
Top Bottom