Ninaomba msaada nina tatizo la tumbo kujaa gesi na kupata choo kigumu

Ninaomba msaada nina tatizo la tumbo kujaa gesi na kupata choo kigumu

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Ndugu zangu mimi na sumbuliwa na matatizo ya tumbo langu alihumi apana
Bali kuna kipindi na sikia maumivu kama nachanwa na kitu tumboni
Napia na jamba saana na migurumo tumboni na nina sikia miguu kuregea
 
Matatizo yako yatakua kwenye utumbo mdogo, nenda hospitality kubwa wanaweza kukupa dawa ya kunywa kabla ya X-ray, dawa huweka alama katika sehemu zenye matatizo.
 
Nilikuwa nayo hii shida wakati fulani mwaka huu, baada ya vipimo nilipatwa na "amoeba" usihofu nenda kituo cha afya uanze matibabu
 
Nina tatizo la tumbo kujaa gesi sana. Na kibaya zaidi na pata choo kigumu. Na nina jamba sana.

Sasa leo nilivyo cheki kinyesi changu nimeona kama kuna matone kidogo kidogo ya damu
Sijui hili ni tatizo gani.

Nilikwenda hospital docter aliniuliza dalili tu ninazo sikia nikamwambia akanigusa tumboni alafu akasema sina tatizo lolote zaidi ya gesi tu tumboni.

Sasa nataka kuhuliza mtu mwenye gesi tumboni anaweza kupata cha ngumu?

Ambayo ina matone damu?
 
Kafanye kipimo cha H pylori stool antigen test na Stool analysis mbeleni hali ikiendelea baada ya matibabu fanya OGD na Colonoscopy.

But hakikisha mlo wako una mboga za majani, Matunda na Maji mengi na Usikae na choo kwa muda mrefu.
 
Acha kukaa mda mrefu bila Kula, epuka vyakula vya kukobolewa hata ulaji wa wali kila sku sio mzuri , epuka kutumia Sana vinywaji vya viwandani eg soda , hasa Pepsi na hasa unapomaliza tu Kula , na hata maji ya bardi sana mara unapomaliza Kula, epuka kukaa kaa Tu bila kazi inayohusisha viungo vya mwili kufanya kazi ...!! Vyakula vya asili ni suruhisho Bora zaidi
 
Zingatia lishe nzuri..kwamfano kama hutumii ugali wa dona. Tumia ugali wa dona angalau kwa siku 4mfululizo utaona tofauti ya choo kinachotokana na sembe na kile cha dona.

..jaribu pia kutengeneza juisi ya ukwaju nzito sio hizi za dukani tengeneza mwenyewe au tumia mapapai,
usiache kunywa maji ya kutosha

kula kwa wakati..unapokaa muda mrefu bila kula mfumo wa chakula hufyonza maji yote yaliyopo kwenye mabaki ya chakula.

Jaribu hizo mbinu angalau kwa siku 4 tu ukiona inasaidia basi itakufaa kwa siku zote
 
Hilo la gas tumia eno liver salt. Kuhusu choo kigumu, kula Makande na maziwa mtindi kisha uje utoe mrejesho hapa. Kuhusu kinyesi kuwa na chembe za damu, hapo ni maumivu yakizidi muone daktari.
 
Nina tatizo la tumbo kujaa gesi saan. Na kibaya zaidi na pata choo kigumu.

Nenda pale Dakawa (Morogoro) Siku ya Jumamosi kunakuwa na Mnada mkubwa.

Mtafute Mmasai anaitwa Isaya anatengeneza dawa nzuri sana za magonjwa ya tumbo na kupunguza unene.

Tena anatengenezea hapo hapo mnadani. Nina imani ukitumia utapona.
 
Kunywa lita tano za maji kwa siku, chemsha maji weka ndimu na kahawa kunywa, kula matunda kwa wingi, fanya mazoezi ya kukimbia kilometers 5 kila siku, kula tikiti kubwa moja kwa siku nadhani pale kwenye matunda ongezea, mwabudu mungu wako akuepushe na maradhi zaidi ya yote hii thread mods pelekeni kwenye jukwaa la Afya huku mwamba ataingia cha kike maana ni wanasiasa tupu
 
Nenda pale Dakawa (Morogoro) Siku ya Jumamosi kunakuwa na Mnada mkubwa, mtafute Mmasai anaitwa Isaya anatengeneza dawa nzuri sana za magonjwa ya tumbo na kupunguza unene. Tena anatengenezea hapo hapo mnadani. Nina imani ukitumia utapona.
Sawa isaya tumekuelewa, tutakuja
 
Back
Top Bottom