Ninaomba msaada wa mawazo yenu

Ninaomba msaada wa mawazo yenu

toccara

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2014
Posts
540
Reaction score
202
Habari,

samahani jamani ninatatizo ambalo limenikabili ninaomba msaada wenu, nina mdogo wangu alifanya kidato cha nne mwaka 2005 akapata division 4 ya 33, nilimwambia arudie hakutaka akaenda uganda akafanya kidato cha sita akapata principal pass mbili na subsidiary moja, principal pass hizo ni za kiswahili na fine art, na subsidiary pass ya geography.

Pia alifanya certificate ya graphisc design, baadae akataka kusoma tena akaomba kamapala international ya Dar akapata diploma ya business administration mwaka 2009, ila baadae akakataa kusoma sasa amekaa nyumbani matumizi nikampunguzia, jana kaniambia anataka kusoma ila mambo ya information technology.
Jamani mtu kama huyu anatakiwa kuanza kwa ngazi ipi?

Pia ni chuo gani kitaweza kumpokea? Au kozi gani anaweza kufanya? Ni msichana na kwa kuwa sasa maisha yamempiga chochote nitakachomwambia atafanya.

Naombeni mnisaidie mawazo nijue kwa kumuweka
 
Una moyo wa uvumilivu sana mkuu!huyo mdogo wako c ni mtu mzima kabisa,asa we unahangaika nae wa kazi gani?
 
Kwani ni mlemavu?! Mtafutie kazi. Atasoma mpaka wapi? Na umuambie wanaume siku hizi hawataki wake wavivu, ataishia kuwa small hausi ya kila mwenye vijisenti!
 
hata mimi nashindwa kushangaa!!..
Kumbe ni 'mbebez' lol!..mwambie mimi natoaga mihela kwa 'mbebez' super viwangoz you know!!
 
asanteni, siyo mlemavu ni mzima tuu
 
Kwani ni mlemavu?! Mtafutie kazi. Atasoma mpaka wapi? Na umuambie wanaume siku hizi hawataki wake wavivu, ataishia kuwa small hausi ya kila mwenye vijisenti!

kiukweli ananichosha tuu na siyo mdogo kivile tumepishana miezi 10 tuu kuzaliwa jamani wazazi wake wameshanawa mikono, kahamia kwangu sasa sijui nimfanye nini na hiyo IT anayotaka ikipatikana sijui atasoma yaani ni msalaba
 
Wala usikubali akutese. Tena umuambie asome magazeti ajiombee kazi, na ukiskia kazi mahali muambie aombe. No pocket money, nunua pads, lotion na deodorants bwaga hapo.

mie nna dadangu is 36 yrs old na anadeka kuliko huyo. Anafanya kazi professional kabisa na anakuomba kodi ya nyumba. Huwa namuambia nenda kakae kwa mshua pale, free rent ya kufa mtu hehehe.

C amefikisha miaka 18? Elimu aliyopewa inamtosha kucmama mwenyewe atafute kazi atajiendeleza mbele ya safari.
 
Hanna msomaji hapo anakuzingua tu Dada angu .
ashakuwa jimama mzima huyo anakula bule analala bule anakunya na kupendeza bule kuna vidume vinampanda coz anapendeza .
usumbufu na kudeka kunamwisho wake ww unakosea unaendelea kumlemeza.

mtafutie kazi huyo kama dunia ya elim ashapishana nayo akipigika ndani ya kazi ndio atashika adabu harafu unamwambia akazane ili aje ajiendeleze baadae kujisomesha kwa kujiwekea akiba ili aone
 
Wala usikubali akutese. Tena umuambie asome magazeti ajiombee kazi, na ukiskia kazi mahali muambie aombe. No pocket money, nunua pads, lotion na deodorants bwaga hapo.

mie nna dadangu is 36 yrs old na anadeka kuliko huyo. Anafanya kazi professional kabisa na anakuomba kodi ya nyumba. Huwa namuambia nenda kakae kwa mshua pale, free rent ya kufa mtu hehehe.

asante sana kwa wazo zuri, sasa kaja ofisini akaniambia kapata chuo kinaitwa Learn It hapo lumumba mnazi mmoja, ataanza kwa diploma ada ni 2.8m kwa mwaka, nimemwambia nitamjibu kesho, je kama atakuwa serious nimpeleke hapo? kiukweli ananiumiza sana, mume wangu ndiyo hataki hata kusikia hayo mambo nikimwambia ananiambia ni mdogo wako fanya unavyoweza, uwezo wa kumsomesha ninao, pia nimegundua hiyo graphics kuna vitu vichache sana ndiyo anaviweza.:A S 114:
 
Hanna msomaji hapo anakuzingua tu Dada angu .
ashakuwa jimama mzima huyo anakula bule analala bule anakunya na kupendeza bule kuna vidume vinampanda coz anapendeza .
usumbufu na kudeka kunamwisho wake ww unakosea unaendelea kumlemeza.

mtafutie kazi huyo kama dunia ya elim ashapishana nayo akipigika ndani ya kazi ndio atashika adabu harafu unamwambia akazane ili aje ajiendeleze baadae kujisomesha kwa kujiwekea akiba ili aone

nina hasara kubwa alitaka mtaji wa milioni 5 nikampa 6, nikasafiri, narudi nakuta vitz ipo nje nauliza naambiwa ya mama mdogo, kumuuliza kasema hakupanga kufanya biashara ya milioni 6 hivyo kaamua anunue gari, sasa hivi nimefunga kioo gari haina service wala mafuta limekaa tuu, nataka nimpangie vyumba kodi ya mwaka nimtafutie chuo nilipe ada ya mwaka, nimpe mtaji then nimbebe mpaka kwa wazazi wake nikambwage hapo kuwa msaa da wangu umeishia hapo atakuwa na hiari kukaa kwa mama yake au kwenye vyumba vyake
 
umesha play your part.mtu asiye jielewa ni mzigo.ukisaidiwa nawe onesha ushirikiano,sasa huyo hana ushirikiano.
Hiyo business administration inamtosha kuomba kibarua.pia wewe unajuana na watu hata kwenye saccos,microfinance companies kibao,customer care samsung,airtel aombe huko ajitegemee lasivyo atasoma mpaka azeeke na atakuwa mzigo.bado kidogo atakuletea ka baby.angekuwa na akili milion sita asingekuwa tegemezi teena.watu wanakopa milioni moja wamekuwa na maisha ya kujitegemea sembuse yeye ya kupewa? Da kweli umasikini wa akili ni mbaya kuliko wote.maoni tu haya kutokana na mtoa thread, other things remain constant,labda kakata tamaa
 
nakubaliana na wewe
 
nina hasara kubwa alitaka mtaji wa milioni 5 nikampa 6, nikasafiri, narudi nakuta vitz ipo nje nauliza naambiwa ya mama mdogo, kumuuliza kasema hakupanga kufanya biashara ya milioni 6 hivyo kaamua anunue gari, sasa hivi nimefunga kioo gari haina service wala mafuta limekaa tuu, nataka nimpangie vyumba kodi ya mwaka nimtafutie chuo nilipe ada ya mwaka, nimpe mtaji then nimbebe mpaka kwa wazazi wake nikambwage hapo kuwa msaa da wangu umeishia hapo atakuwa na hiari kukaa kwa mama yake au kwenye vyumba vyake

yaelekea wewe ni fogo sana mkuu?sasa hzo pesa unazotaka kuzipoteza hapo kwa huyo mdogo wako kwa kumlipia ada c ni bora ukasaidie watoto yatima na mungu atakubariki?
 
hahahahaha nimechekaje ila inaumiza

Dada Nami nipo kama yeye hivyo hivyo nilifeli form four sahiz nawatesa tu wazazi !

Nisaidie namba yake ya simu tubadilishane mawazo !

Ikibidi tuoane !
 
Back
Top Bottom