Hivi karibuni Tume Huru ya Uchaguzi imetangaza na kuomba maeneo mbalimbali kutoa/kuleta mapendekezo ya kugawa majimbo ili kuongeza idadi ya wawakilishi/Wabunge katika Bunge letu la Jamhuri ya Tanzania.
Binafsi ninawaomba/kuwashauri kuachana kabisa na wazo hili la kugawa majimbo kutokana sababu zifuatazo:-
(1) Zoezi hili linaongeza bajeti kubwa ambayo ingeelekezwa kwenye maeneo muhimu.
(2) Mchango wa Wabunge wetu kwa sasa hayakidhi matakwa yetu sisi wananchi tuliowatuma na hivyo kuongeza majimbo ni kama kupoteza fedha.
(3) Nchi yetu ina tatizo la ajira. Vijana wengi wako mitaani kwa kukosa ajira. Fedha hizo zingeelekezwa katika maeneo yatakayotengeneza ajira kwa vijana wetu.
(3) Katika shule zetu bado kuna uhaba mkubwa wa miundombinu kwa mfano madarasa, walimu, madawati n.k. tuelekeze fedha hizi kwenye maeneo ya elimu kuliko kuelekeza kama mishahara, posho kwa wabunge wa majimbo mapya.
(4) Itakuwa jambo la busara pia kuyaunganisha yale majimbo yenye wabunge wanaowakilisha watu mathalani 8,000 ili uwakilishi wao uwe na watu 100,000 na kuendelea.
Tuwe na uchungu na nchi yetu. Tupeleke rasilmali zetu kwenye maeneo muhimu. Ninamwomba Mhe. Rais aingilie suala hili la wazo la kugawa majimbo mapya.