Ninaomba tafsiri ya ndoto hii kwa mwenye kufahamu

Mama pretty

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2020
Posts
2,082
Reaction score
4,103
Wakuu, nimeshtuka kutoka usingizini takribani zaidi ya nusu saa iliyopita nikitafakari juu ya ndoto hii niliyoiota.

Nimeota nipo mazingira yangu ya kazi ( inaniunganisha mimi na wateja) kuna kitu mteja alijieleza lakini Meneja wangu hakumuelewa ila mimi nilikua nimemuelewa nikaamuru ahudumiwe kwa alichotaka ila kwa kuwa hakueleweka kwa Meneja akasema nitawajibika kwa damage yoyote atakayopata mteja kimoyomoyo nikasema sawa huku nikiwa na uhakika na nilichofanya na ile "ngoja tuone"!! ... at the end nikaonekana nipo sahihi.

Baada ya hapo nikataka kwenda washroom.. nimetoka nje kama kuna kichaka kidogo tu na mbele yake ndipo kuna washrooms.. nikaona nyoka mweusi mwembamba amejilaza njiani (sipo vizuri kwenye kutambua species za nyoka hapo mtanisaidia) .. ila akilini nikajisemea yule nyoka ni kama Meneja wangu (yani nafsi ya Meneja ndani ya nyoka)

Nikajisemea pale napita hivyo hivyo siogopi! Nikapita kwa kumruka kwa mwendo wa kawaida! Baada ya mwendo kidogo akaanza kunifuata! Hhm! Hapo nikajisemea huyu nimkimbie tu.. nkaanza kukimbia kwa speed mithili ya Kipchong!

Wakati nakimbia kwa speed kali ambayo kikawaida siwezi kukimbia nikawa nampitisha sehem mbaya mbaya.. kama mwenye miiba na kokoto nyingi.. na niliona nafurahia kumpitisha sehem hizo mpaka nikawa namcheka yani nkimuangalia !!!

Mwishowe na washroom nikaghairi nkasema na deal na huyu nyoka shenzi zake!! Kwa hiyo akawa kachoka tayari na kajeruhiwa kwa zile sehem nilizompitisha! Aliacha kunikimbiza akawa kakoma na mimi nilirudi ofisini nikiwa nimefurahi sana kwa kitendo kile.

Nikashtuka usingizini nikatafakari sana juu ya ndoto hii na kuamua kuipandisha hapa!

In reality Meneja wangu anapambana sana kunishusha cheo maana mimi ni msaidizi wake na hakuna popote nilipomkosea!.

Naomba mwenye tafsiri maana nimetafakari sana nashindwa kupata majibu!.
Nawasilisha.

Herbalist Dr MziziMkavu
Mshana Jr
 
Kwa kuwa huyo nyoka hakukudhuru ina maana Mungu anakulinda na anakupgania pamoja na vita inayoendelea chini kwa chini baina yako wewe na boss wako. Roho wa Mungu yupo ndani yako, na Mungu ameamua kukufunilia ili uone yanayoendelea / yanayokuja mbeleni.

Usiogope, Mungu yupo pamoja nawe, lolote baya litakalofanywa juu yako halitafanikiwa. Endelea kuomba/na kumshukuru Mungu.🙏
 
Tasfsir sahihi ya ndoto yako una uadui mkubwa saana katika kazi unapofanya Kama nyoka alikuwa Ni mdogo uadui wako Ni mdogo Kama nyoka uliyemkimbia Ni mkubwa tambua una uadui mkubwa saana maeneo unayoishiii
 
Kabla ya kulala ulikua umekula nini, kiasi gani? Mazingira uliyolala yapoje i mean kitanda na madirisha na idadi ya watu kitandani....Jana ulikua unawaza nini hasa ?
 
Mwongozo kupata tafsiri ya ndoto.
MAZINGIRA- Kazini unapofanyia
VILIVYOHUSIKA- Wewe, boss na nyoka
MAADUI- Nyoka
ULICHOKUWA UNAFANYA-kuhudumia mteja wakati boss kashindwa, kwenda washroom na kumkimbia nyoka.
HOW DID IT END- good or bad end

Hapa umefunuliwa yanayoendelea kazini kwako, kwa ufupi Meneja wako ni adui uadui unaotokana na kumzidi baadhi ya mambo (refer kitendo cha kumhudumia mteja wakati ye kashindwa kumwelewa) na hiki ndo chanzo cha uadui.

Pili uadui wenu ni utaendelea kwa sababu going to washroom ni kiashiria cha kweda kutoa unwanted au kujisafisha uwe clean zaidi. Uamzi wa kwenda washroom inaashiria adui iadha keshakuchafua au kafanya jambo la kukuharibia na analengo la ubaki hivyo hivyo ili adhima yake ifanikiwe ndo maana kuwepo kichaka chenye nyoka kilicho block lengo lako la kwenda washroom.

Tatu nyoka ni adui. Kitendo cha kukufata/kukukimbiza ni kwamba adui anakufatilia akudhuru. ( we all know, most of snakes are poisonous and kills). Kwa hiyo adui anaweza kuiua position yako kazini na pengine kajipanga kwa hilo. Hajafanikiwa kwasababu upo vizuri thatz why alionekana hajakupata na umempitisha mazingira yaliyomdhuru yeye instead of you.

Endelea kuwa karibu na Mungu kwa sala za kutosha as this is the only weapon. Ndoto ni spiritual monitor kutuonesh what is going on, what is coming and what happened ili tuchukue hatua.
 
Hiyo ni dalili tu ya kushindwa kwa adui yako, na sio kwamba ameshashindwa. Umesema umemchosha, je, akipata nguvu, si ataanza upya? Endelea kujiimarisha kiroho, maana ndio silaha yako.

Roho wako ana nguvu kuliko hao roho wengine (uchawi, mazingara, ushirikina, nk). Fimbo ya Musa (wakiwa Misri), ilipofanya maajabu ya kugeuka kuwa nyoka, ili kumfanya mfalme (Farao) aache kiburi na kuwaachia wanaisraeli, mfalme naye akawatuma wachawi wake, wafanye kama alivyofanya Musa. Nao wakafanya uchawi wao, wakatokea nyoka, lakini nyoka wa Musa akawameza wale nyoka wa uchawi.

Nyoka wa Musa alikuwa ni roho, na ndio maana akawashinda nyoka wa uchawi. Nawe utamshinda huyo nyoka kama utaendelea kuwa imara. Hivyo kwako, umeonyeshwa dalili ya ushindi, lakini usibweteke, endelea kusimama imara, ujilinde.
 
Kwa kuwa huyo nyoka hakukudhuru ina maana Mungu anakulinda na anakupgania pamoja na vita inayoendelea chini kwa chini baina yako wewe na boss wako. Roho wa Mungu yupo ndani yako, na Mungu ameamua kukufunilia ili uone yanayoendelea / yanayokuja mbeleni.

Usiogope, Mungu yupo pamoja nawe, lolote baya litakalofanywa juu yako halitafanikiwa. Endelea kuomba/na kumshukuru Mungu.🙏
Amen, nashkuru 🙏
 
Tasfsir sahihi ya ndoto yako una uadui mkubwa saana katika kazi unapofanya Kama nyoka alikuwa Ni mdogo uadui wako Ni mdogo Kama nyoka uliyemkimbia Ni mkubwa tambua una uadui mkubwa saana maeneo unayoishiii
Hakuwa mkubwa.. ukweli uadui ninao.. Mungu ni mwema ananipigania!
 
Back
Top Bottom