Ninaomba tafsiri ya ndoto hii kwa mwenye kufahamu

Ninaomba tafsiri ya ndoto hii kwa mwenye kufahamu

Kabla ya kulala ulikua umekula nini, kiasi gani? Mazingira uliyolala yapoje i mean kitanda na madirisha na idadi ya watu kitandani....Jana ulikua unawaza nini hasa ?
Chakula kiasi cha kawaida..
Mazingira yangu yapo kawaida.. nalala peke yangu.. mawazo ya kawaida tofauti tofauti.
 
Mwongozo kupata tafsiri ya ndoto.
MAZINGIRA- Kazini unapofanyia
VILIVYOHUSIKA- Wewe, boss na nyoka
MAADUI- Nyoka
ULICHOKUWA UNAFANYA-kuhudumia mteja wakati boss kashindwa, kwenda washroom na kumkimbia nyoka.
HOW DID IT END- good or bad end

Hapa umefunuliwa yanayoendelea kazini kwako, kwa ufupi Meneja wako ni adui uadui unaotokana na kumzidi baadhi ya mambo (refer kitendo cha kumhudumia mteja wakati ye kashindwa kumwelewa) na hiki ndo chanzo cha uadui.

Pili uadui wenu ni utaendelea kwa sababu going to washroom ni kiashiria cha kweda kutoa unwanted au kujisafisha uwe clean zaidi. Uamzi wa kwenda washroom inaashiria adui iadha keshakuchafua au kafanya jambo la kukuharibia na analengo la ubaki hivyo hivyo ili adhima yake ifanikiwe ndo maana kuwepo kichaka chenye nyoka kilicho block lengo lako la kwenda washroom.

Tatu nyoka ni adui. Kitendo cha kukufata/kukukimbiza ni kwamba adui anakufatilia akudhuru. ( we all know, most of snakes are poisonous and kills). Kwa hiyo adui anaweza kuiua position yako kazini na pengine kajipanga kwa hilo. Hajafanikiwa kwasababu upo vizuri thatz why alionekana hajakupata na umempitisha mazingira yaliyomdhuru yeye instead of you.

Endelea kuwa karibu na Mungu kwa sala za kutosha as this is the only weapon. Ndoto ni spiritual monitor kutuonesh what is going on, what is coming and what happened ili tuchukue hatua.
Nashkuru sana kwa ufafanuzi..

Kwanza ni kweli hali ya uadui ipo kama ulivyosema kumzidi baadhi ya mambo ukizingatia mimi ni mdogo sana kwake .. yeye ni mtu wa early 1980's na mimi ni wa late 1990's na kuwekwa kwenye nafasi ya juu kutoka yeye ukizingatia niliipata moja kwa moja na wapo waliosota hapo kazini yani nimewakuta hawajapata hiyo nafasi ( kwa watu anaowakubali sana)

Pili ni kweli ameshafanya attempts kadhaa za kunichafua kwa MD kwa sababu ya uwezo nilioonyesha kazini. Lakini MD hakuona tatizo kwangu .. Meneja anatumia mwanya kwamba anasikilizwa kila jambo na MD!

Tatu ni kweli ananifuatilia sana ili nikosee anishtaki kuwa siiwezi kazi! Ni mwepesi sana kunitafutia makosa lakini Mungu ni mwema ananipigania na matokeo anayapata lakini hataki kuacha!
Mambo yamembadilikia ila hataki kuacha afanyacho! Mimi vita yangu ni ya kiroho ninaomba sana Mungu asimame mwenyewe apigane mimi siwezi peke yangu!
 
Hiyo ni dalili tu ya kushindwa kwa adui yako, na sio kwamba ameshashindwa. Umesema umemchosha, je, akipata nguvu, si ataanza upya? Endelea kujiimarisha kiroho, maana ndio silaha yako.

Roho wako ana nguvu kuliko hao roho wengine (uchawi, mazingara, ushirikina, nk). Fimbo ya Musa (wakiwa Misri), ilipofanya maajabu ya kugeuka kuwa nyoka, ili kumfanya mfalme (Farao) aache kiburi na kuwaachia wanaisraeli, mfalme naye akawatuma wachawi wake, wafanye kama alivyofanya Musa. Nao wakafanya uchawi wao, wakatokea nyoka, lakini nyoka wa Musa akawameza wale nyoka wa uchawi.

Nyoka wa Musa alikuwa ni roho, na ndio maana akawashinda nyoka wa uchawi. Nawe utamshinda huyo nyoka kama utaendelea kuwa imara. Hivyo kwako, umeonyeshwa dalili ya ushindi, lakini usibweteke, endelea kusimama imara, ujilinde.
Amen.. ndoto ni mlango wangu mkuu kwa ishara na mambo yaliyopo, yaliyotokea na yatakayotokea..
Kuna ndoto za kupuuzia na zingine si za kupuuzia.. nipo vizuri na Mungu!
 
Mungu aliweka ndoto ili aseme nasisi tukiwa nje na purukushani za dunia ambazo hutufanya tujifanye tuko busy na tusijali sauti yake.

Ndoto yako haihitaji tafsri yoyote, maana iko wazi Sana wala haina kificho chochote.

Anyways, ulipotaka kwenda chooni maana yake ulitaka kujutia/kubadilisha maamuzi sahihi uliyofanya/unayopaswa kufanya. Na huyo nyoka (roho mbaya) uliyekutana naye ndo atakushawishi/anakushawishi usifanye kilicho sahihi.

Ndoto inakusisitiza kufanya kile kilicho sahihi bila kuyumbishwa, lakini pia inakutahadhalisha kwamba kuna hila nyingi zimekuzunguka au zitakuzunguka mahali pako pa kazi. Shukuru kwamba hukufika huko chooni! Maana ktk njozi Hilo ni lango la kuzimu.

Kila ndoto inapoisha lazima uamke,, lengo ni ili uchukue hatua za maombi pale pale either kulinda uliochokiona ndotoni Kama ni kizuri au maombi ya kukibatilisha Kama ni kibaya. Bahati mbaya wengi wakishtuka ndotoni badala wafanye maombi, wanaanza kusimulia watu.

Nakukumbusha pia kwamba ndoto nyingi huelezea Yale yajayo (chache Sana hueleza yaliyopita).

Kulingana na Habakuki 2:2-3

Kisha, Mwenyezi-Mungu akanijibu hivi:

ā€œYaandike maono haya; yaandike wazi juu ya vibao, anayepitia hapo apate kuyasoma. Maono haya yanangoja wakati wa kufaa; ni maono ya ukweli juu ya mwisho. Kama yaonekana kuchelewa, uyasubiri; hakika yatafika, wala hayatachelewa"

Hivyo uliyoyaona katika ndoto yako yanaweza kuwa Kesho tu ukiwa kazini kwako au yakatukia baada ya siku/miezi kadhaa. Muhimu ni kwamba lazima yatatokea, hivyo Fanya linalokupasa.

~Jodeo~
 
Ndoto yako ipo wazi inajieleza na hata wewe mwenyew umafafanua wazi, hapo huhitaji msaada wa tafsiri. Jiongeze mwenyew...
All in all hata wewe pia ujitathimini mienendo yako kazini, usimnyoshee manager wako kidole kumbe wewe ndiye tatizo kazin na hujijui kama ni tatizo badala yake unamuona mwenzako ni tatizo...
Ndoto pia zinaweza kutumika kukuonyesha wewe upo sahihi ili tu zikupumbaze ujione unawindwa au unaonewa...
#TAFAKARI
 
Back
Top Bottom