Ninaombeni connection ya kazi - Dar

Ninaombeni connection ya kazi - Dar

Nsombas

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2018
Posts
285
Reaction score
427
Habarini Wakuu.

Nipo mbele yenu ninaomba kuunganishwa na kazi ili mradi nipate kipato changu halali.

Nitaeleza kilichonikuta kwa ufupi.

Mimi ni mhitimu wa Shahada ya Usimamizi Wanyamapori (bado sijaajiriwa huu ukiwa mwaka wa 9). Nina familia ya watoto wawili ingawa kwa sasa ninaishi na mmoja na mama yake.

Kuna kipindi niliitwa interview Mkoa X, nilipofika wakaniomba hela 1.1 M ndipo nipate kazi. Sikuwa nayo, niliikosa ile kazi. Nikajiongeza nikaomba nafasi nijishikize Ofisi ya Serikali na nilifanikiwa nikawa nina hakika ya kupata elfu 60 kwa mwezi (inaitwa OC, waloajiriwa wanajua). Kile kipato ikanibidi nipange Geto, nile, ninywe n.k

Huku Dar mama mtoto ana kazi yenye mshahara wenye 6 zeros (1+M) (Awali niliandika 6+ digits, nilikosea nilichokuwa nina maanisha). Nikawa ninarudi Dar mara chache sana kwa mwaka. Mpaka mwaka jana nikaona nimejishikiza sana pale na bado sioni future hivyo nikaamua kurudi Dar.

Nimefika home maisha yakaendelea vema na mama mtoto.

Siku moja nikamwambia kwa kuwa wewe una kutana na wengi huko makazini, ninaomba nipambanie nipate pa kujishikiza sio lazima iwe kazi ya professional yangu. Akakubali. Nakumbuka nilimkumbusha mara 2 hivi akawa ananitajia nitaongea na Y na Z. Kumbe bwana Z ni mchepuko wake (hapo nilikua sijui).

Siku moja amerudi home toka kazini bwana Z akampigia simu mama mtoto nikiwa naye. Akapokea. Ila alivokua anaongea ilinipa mashaka kwasababu alikua anamjibu sivyo, mara kigugumizi (nadhani mnaelewa). Nikamwambia mbona unaongea hivo? Akanijibu ni mmoja wa niliyemuomba kazi kwa ajili yako.

Tobaaa! Nikashangaa ndio unamjibu hivo? Hiyo kazi nitapata kweli? Nikawa interested kujua zaidi. Mama mtoto akaniambia tuingie ndani, akili yangu ikaniambia huyu anataka amtumie jamaa msg (kama vile nilikuwepo akilini mwake). Tukaingia room ila mwenzangu akatoka Sebuleni na simu yake mkononi, nami kwasababu nimejua lengo lake nikatoka pia nikaenda nje moja kwa moja. Haraka akarudi room kutoka Sebuleni. Nami sekunde kadhaa nikarudi haraka room. La haula! Nikampokonya simu, kweli akawa amemwandikia jamaa asipige simu sababu amekamatwa (alikuwa bado hajaituma kwa jamaa).

Niliumia sana. Nikamkumbusha kuwa nilikuambia hii simu nina mashaka nayo na hata unachonielezea kwamba jamaa anakutongoza si kweli na hata macho yako yanaonesha unanidanganya. Akabaki hajui la kufanya.

Nilimtxt jamaa kwa maneno ya kuumiza sana ila hakujali wala nini. Mama mtoto alifuta ile namba ya jamaa. Nikasamehe. Zikapita wiki kadhaa. Jamaa akamtafuta tena mama mtoto na hapo mama mtoto alikua amenipatia simu yake (anataka niaminisha hana tena mawasiliano na jamaa).

Nikawa interested kujua ukweli wa natafutiwa kazi au kuna lingine. Nikachat na jamaa kupitia simu ya mama mtoto. Aisee! Mwishowe nikagundua hawa ni aidha walikua au ni wapenzi. Nikarudi kwa mama mtoto aniambie ukweli wa hili. Kweli bwana mama mtoto akasema nilipokuwa Mkoa X sikuwa namtumia hela hivyo akawa na jamaa kwasababu alikua anampa hela (Niliumia sana, nashindwa kueleza ila mwanaume aliyechapiwa mkewe anajua maumivu haya).

Nikajiuliza kumbe mimi ninapambana Mkoani, huku mwenzangu ana mahusiano mapya na anataka mchepuko wake uniunganishie kazi Ofisini kwao (hii ni dharau kubwa sana endapo ningepata kazi Ofisini kwa jamaa). Mama mtoto ana mshahara mzuri (1+M) lakini bado aliingia tamaa ya hela.

Nimeukubali ukweli huo, nikasamehe ila kusahau bado. Mwanamke nikamwambia kufuta namba ya jamaa wala si suluhisho. Ongea nae muelezee A, B, C. Akakubali. Siku moja tulipiga simu kwa jamaa akatublock.
Ni maumivu makali sana ninayo kwa kutokuwa na kazi. (Nimefupisha story, yanaumiza nikikumbuka zaidi).

Ninaombeni mnisaidie nipate kazi ili nisahau hilo jambo maana nitakuwa busy.
Nina tanguliza shukrani zangu za dhati kwenu wakuu.
 
Mwanamke akisha kucheat haitakiwi kurudiana nae. Cha kufanya hapo chukua kila kitu ndani uza kwa bei ya hasara hapa Nina maanisha uza takataka zote ndani utapata mtaji na pesa ya kupanga chumba uanze maisha uyo mwanamke muache na mtoto wako wakilala chini najua atapata vitu hata kwa kukopa wewe kapanbanie maisha Yako

Uza vitu vyote ndani au hamisha yey akiwa hayupo
Iwe mtaji wako
 
Mwanamke akisha kucheat haitakiwi kurudiana nae. Cha kufanya hapo chukua kila kitu ndani uza kwa bei ya hasara hapa Nina maanisha uza takataka zote ndani utapata mtaji na pesa ya kupanga chumba uanze maisha uyo mwanamke muache na mtoto wako wakilala chini najua atapata vitu hata kwa kukopa wewe kapanbanie maisha Yako

Uza vitu vyote ndani au hamisha yey akiwa hayupo
Iwe mtaji wako
Nashukuru kwa mawazo yako Mkuu
 
Kwani nani kasema mtoto ana hatia? Una uhakika huyo ni mtoto wako?
Ukiona mwanamke anang'ang'ana na mchepuko jua kuna tàtizo kubwa. Uatuawa bure.
Mtoto ni wangu, hili nina hakika nalo kwani nami sio mporipori.
Ungesoma vizuri mkuu. Jamaa ndiye alimtafuta tafuta mama mtoto kama mara 2 hivi bahati mbaya simu ya mama mtoto nilikuwa nayo kwa mara zote 2. Mwanzo jamaa alitublock wote ila kwa sasa namba yake haipatikani hewani tena
 
Dah q******ke umaskini mbaya sana tuendeleze mapambano wakuu

Pole sana kwa changamoto unazopitia mkuu mungu atabariki mambo yatakaa sawa
Mkuu, acha tu. Nimejitafuta sana ila sijakata tamaa. Ninaomba wadau wanisaidie niepukane na hiki kikombe
 
Back
Top Bottom