Ninaombeni connection ya kazi - Dar

Dah pole sana Mkuu, limeniumiza sana hilo najua changamoto ambazo huwa tunapitia mambo ya kiuchumi yakiwa yamegoma. Sema nakusihi mrejee Mungu katika imani yako na uombe kwa bidii akufungulie njia za kiuchumi. Huo mkwamo sio wa kawaida
 

Attachments

  • Screenshot_20250227_214633.jpg
    230.9 KB · Views: 2
Pole sana kwa wakati mgumu unaopitia hakika utavuka salama na utakuwa imara.
Nashauri uendelee kuwa nae Wala usithubutu kumwacha kwani unaelekea kuyamaliza makandokando ubakiwe na kitu halisi ila ni suala la mda tu.
Maumivu unayopitia ni ya mda Wala usifikirie yatakuwa siku zote milele.
Kama unamwamini Mungu tenga mda zungumza nae, nae atakupa njia Wala usiwe dhaifu kwa kukosa nguvu ya pesa ndani, weka misingi ya familia Yako haijalishi kwa mazingira Gani itakusaidia sana.
Yashinde mawazo mabaya kwa mema nawe utajenga funzo kwa mwenza wako Wala usiyape nafasi yasiyojenga.
Unanafasi kubwa ya kujenga Wala usiwaze kisasi.
 

Attachments

  • 20241124_140551.jpg
    411.2 KB · Views: 2
Kiongozi huna haja ya kuonyesha unyonge mbele ya mkeo kwakuwa huna kazi .

Tafadhali simama kama mwanaume hata kama huihudumii familia Kuna namna flani unakuwa mpk mkeo anajiuliza hivi huyu akipata kazi au hela itakuwaje?

Acha unyonge dunia haina huruma
 
Mshara wa 60k Daresalaam umepanga chumba mtaa gani cha bei gani na nauli unatumia shingap per day, maji ya kunywa, Kula ukiwa kazini?, what about salio la dk, na mb unaweka shingapi kwa wiki mwenzio ana mshahara wa 6 digits? Akakubali kuwa kwenye mahusiano nawewe?
 
Mkuu hapo ni kwake, kwako au kwenu nyote??
Hizo stress za mapenzi + uchumi ni changamoto!!

Kazi za viwandani, godown vipi ushacheki hizo kwa kujishkiza maana ndio inakuaga last option hiyo kwa wengi.
Hapa tumepanga, awali nilikuwa vizuri financially hata nilikuwa nina uwezo wa ku-pay bills (nilitapeliwa hela yote, hii story nyingine).
Sijacheki hizo Mkuu sababu sina A wala B juu ya hizo kazi
 
Mkuu ungesoma vizuri.
60k nilikuwa napewa (OC) nikiwa Mkoa X sio hapa Dar.
Awali nilikuwa stable financially na mnapoanza mahusiano sio lazima mwanaume uwe na hela ndipo ukubaliwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…