Wakuu, nimerudi tena kwenu.
MWANAMKE MSALITI HAPASWI KUPEWA SECOND CHANCE.
MSAMEHE KISHA ONDOKA.
Nilidhani utani kumbe kweli. Kama awali nilivosema, huyu Mwanamke kumbe ana rafiki yake wa kike ndiye wanajazana ujinga. Nimekuta wanawasiliana na kupeana updates na mbaya zaidi ni yule rafiki ake anaandika msg za kejeli na vijembe kwangu na kumtumia mama mtoto. Mama mtoto naye hana cha kusema anasema ngoja tuone mwisho wake litakuaje hili jambo.
Sasa nimeamua kuondoka, sijali tena kuhusu mtoto wangu. Ngoja niwaache waendelee kushauriana. Mwenzake yupo kwenye mahusiano yake anafurahia, yeye anashaurika utoto na ujinga. Halafu ajabu huyo huyo rafiki yake muda huu anamshauri mama mtoto aniombe tena msamaha. Ila wanawake daah!
Pamoja na kwamba amenipigia magoti kuniomba sana msamaha, ninasamehe lakini sifanyi ujinga wa kuendelea na haya mahusiano.
Ninatamani nimpige tukio (sio kumdhuru) ila huruma inanijia hasa nikitafakari masuala ya kidini.