Ninaombeni ushauri, kila ninachowaza kujikomboa kiuchumi sifiki mbali

Pole sana ,ila ukiona unakua na alot of thoughts juwa unakaribia kwenye maisha ya ndoto yako,usikate tamaa kazana,anza na kidogo ulichonacho
 
Una miaka 34 unalala pekee yako? Ndio maana una msongo wa mawazo. Tafuta mtu wa kulala naye akupeti peti kichwa kitatulia utapata suluhisho. Apo kichupa kimejaa tu ndio maana unakuwa hivo. Nani kasema mwanamke anaweza kuishi peke yake?!
Unaweza kuta huyo mwenye 34 yrs analala pekeyake lakini ana amani kuliko aliye na mwenza lakini wanalala mzungu wa nne

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole dada..!! uskate tamaa tafadhal.. ningependa kujua nn klitokea kwenye klimo??
 
Nilishalima vitunguu ila sikupata mafanikio. Bali napenda sana ukulima. Sana. Sijakata tamaa ramani zikisomeka tena nitarudi huko huko kwenye kilimo
Fungua mama lishe kwanza wzkati unakaa sawa
 

Kama una interest na kilimo hama ulipo hamia ndani ndani huko mashambani ujaribu bahati yako… au hamia nanjilinji mkoa wa lindi ukalime ufuta na mbaazi.. maeneo ya kulima yapo kibao ni we tuu kujitoa… ukikubali kuhamia nanjilinji me ntakusaidia sehemu ya kukaa(sio kwangu me Niko dar)na pa kuanzia ili utoboe..
 
Asante mno kwa ukarimu. Ubarikiwe.
 
Pole dada..!! uskate tamaa tafadhal.. ningependa kujua nn klitokea kwenye klimo??
Nilimuamini mtu ambaye amekuwa akilima vitunguu muda mrefu sana. Ila nilipigwa wakati wa mavuno nikapewa story nyingi, the rest is history.
 
Ulishawahi kufanya mapenzi?
 
Nilimuamini mtu ambaye amekuwa akilima vitunguu muda mrefu sana. Ila nilipigwa wakati wa mavuno nikapewa story nyingi, the rest is history.
Fafanua hapa, ulimwamini kama shareholder au ulikuwa msimamizi shambani kwa malipo ya percent wakati wa kuvuna?.
 
Jifunze kutengeza maandazi funga kweny mifuko yawe kama ya viwandani uza hapi mtaani kwako kweny maduka.

Tengeneza sabuni ya maji nzuri nzito weka kweny chupa uza kwa watu mtaani kwako.
Tengeneza jik na shampoo uza mtaani kwako.

Karanga za mayai unatengeneza unapeleka kweny maduka matatu hadi manne.

Tengeneza chapati na uji uuze jion.

Jifunze kutengeza hair band wigs unauza moja kwa 25-40.

Nenda mnadani unanunua mapazia yanayofanana ya unauza, kama ni mafupi sana unanunua na pazia lingine moja linalofanania unapeleka kwa fundi unatengeneza dizaini tofauti tofauti hili kuongeza urefu angalau zifike futi 9.

Arusha Travolta bei ndogo nunua za mtumba na leather jacket za mtumba unauza online.

Nunua masweta mazuri ya watoto uuze online.

Night dress mnadani zinauzwa buku buku nunua uuze buku tatu kwa buku nne.

Mikoba ya mtumba unanunua hadi kwa elfu 5 tano mizuri kabisa unauza kuanzia elf 15-20

Amka tafuta pesa ya mtaji kama uwezi mwambie bwana ako akupe mtaji hata elfu 50.
Biashara yyte si mchezo unatakiwa ufanye bidii haswa.
 
Nilimuamini mtu ambaye amekuwa akilima vitunguu muda mrefu sana. Ila nilipigwa wakati wa mavuno nikapewa story nyingi, the rest is history.
Pole dada...hapo juu kuna jamaa kazungumzia suala la kwenda nanjilinji unalionaje?
 
Usiweke much expectations kwenye Mambo hayo maana over expectations unaweza Leta sonona na magonjwa yanayoambatana na hayo..

Mwisho jitihada haishindi kudra,omba Mungu endelea kuchapa kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…