Hi wote,
Mimi ni mdada nina umri wa miaka 34.
Tatizo langu kubwa ni kustuck. Yaani kila ninachowaza kufanya kujikomboa kiuchumi sifiki popote. Ninawaza mno ila nimestuck.
Hapa ni saa 9 usiku usingizi umekata nawaza tuu. Sina mtaji, sina chanzo chochote cha kupata hela niweze kufanya biashara.
Hata biashara yenyewe nikiwaza sipati picha kamili ntafanya biashara ipi although napenda sana shughuli za kilimo.
Naomba mnisaidie ushauri na mawazo. Natanguliza shukrani za dhati
Jifunze kutengeza maandazi funga kweny mifuko yawe kama ya viwandani uza hapi mtaani kwako kweny maduka.
Tengeneza sabuni ya maji nzuri nzito weka kweny chupa uza kwa watu mtaani kwako.
Tengeneza jik na shampoo uza mtaani kwako.
Karanga za mayai unatengeneza unapeleka kweny maduka matatu hadi manne.
Tengeneza chapati na uji uuze jion.
Jifunze kutengeza hair band wigs unauza moja kwa 25-40.
Nenda mnadani unanunua mapazia yanayofanana ya unauza, kama ni mafupi sana unanunua na pazia lingine moja linalofanania unapeleka kwa fundi unatengeneza dizaini tofauti tofauti hili kuongeza urefu angalau zifike futi 9.
Arusha Travolta bei ndogo nunua za mtumba na leather jacket za mtumba unauza online.
Nunua masweta mazuri ya watoto uuze online.
Night dress mnadani zinauzwa buku buku nunua uuze buku tatu kwa buku nne.
Mikoba ya mtumba unanunua hadi kwa elfu 5 tano mizuri kabisa unauza kuanzia elf 15-20
Amka tafuta pesa ya mtaji kama uwezi mwambie bwana ako akupe mtaji hata elfu 50.
Biashara yyte si mchezo unatakiwa ufanye bidii haswa.