Ninapata milioni mbili kila mwezi nimeomba mkopo nimenyimwa

Ninapata milioni mbili kila mwezi nimeomba mkopo nimenyimwa

Huyu bwana ulichomshauri ni technical sana kwa mujibu wa biashara yake. Huyu amejikuta ana gari, anakodisha hotel analipwa mil2 anaona ni hela nyingiiiii. Mil2 ukiendesha mwenyewe, mafuta juu yako, service juu yako, matairi na Wageni wanataka AC, ukiwa na gari ya CC 1500 kuna nini hapo?? Mshauri arasimishe biashara, mengine matokeo.
Hebu tafuta sehemu niliyosema milioni 2 ni hela nyingi kisha uje hapa. Sijasema masuala ya wageni. Sijasema suala la AC wala service. Hapa acha uzushi Mangi. Kama huna hoja nyamaza.
 
Wewe unataka kukopa ili uongeze magari...kwanini usiongee na wadau humu ndani wenye magari wakupe kwa mkataba ili biashara yako ikue uwe hata na ofisi ndo ukope. Acha uchoyo. Nenda kamuulize Erick wa travel partner alifanyaje???
Ni ushauri wako. Ni mzuri ila bado sijafikiria hilo. Nikishindwa nitaangalia ushauri wako. Asante.
 
Wazo lako ni zuri sana, una uhakika ukichukua gari 3 zote zitapata wateja? Benki nyingi wanataka Bank Statement ndiyo waamini kuwa unamzunguko wa pesa kiasi unachosema, then wanakokotoa ni kiasi gani unaweza kulipa bila kuathiri maisha yako. Kama unataka mikopo anza kuweka pesa yako benki, otherwise kama mke wako ni mwajiriwa mtumie yeye kuchukua mkopo. Lakini jambo la msingi jitahidi sana kuirasimisha biashara yako. Hebu tembelea NMB na Postal Bank, ongea vizuri na afisa mikopo.
NMB hawez pata jaribu Akiba pia viwanja vyako katia hata Liz za vijij mana liz kubwa la halmashaur hawatoi akaunt yako inatakiwa iwe ina run uwe na biashaara zaid ya moja utapata mikopo fresh
 
Hujaelewa,.. Ukiingia mkataba na hotel ya kuwakodishia magari wewe unakuja default vendor. Yaani hata wakitaka basi watakwambia upeleke. Huyo mleta mada anafanya kienyeji ndo maana anakosa hati za kuombea mkopo. Nina maana huyu Hana hata faili la invoice na tax kwa hiyo akilipwa anakula na wake zake maisha yanaenda. Lakini hajui kuwa kuna finance inst. ambazo zinakopesha kwa kuangalia biz flow. Ninajenga hoja hapa kuwa Kama akiwa na logo na akapewa magari na watu kwa mkataba mzuri ni rahisi kujiimarisha na kupata ofisi. Kama hujaelewa basi.
. Siku zote usiseme usichokijua. Usiisemee nafsi ya mwenzio kwani usichokijua ni sawa na usiku wa kiza. Ninashukuru kwa kunielekeza sehemu ya kwenda kukopa.
 
Wazo lako ni zuri sana, una uhakika ukichukua gari 3 zote zitapata wateja? Benki nyingi wanataka Bank Statement ndiyo waamini kuwa unamzunguko wa pesa kiasi unachosema, then wanakokotoa ni kiasi gani unaweza kulipa bila kuathiri maisha yako. Kama unataka mikopo anza kuweka pesa yako benki, otherwise kama mke wako ni mwajiriwa mtumie yeye kuchukua mkopo. Lakini jambo la msingi jitahidi sana kuirasimisha biashara yako. Hebu tembelea NMB na Postal Bank, ongea vizuri na afisa mikopo.
Thanks kwa ushauri.
 
Hahahha, huo ni mjadala mwingine, wa hotel na guest house! Inaweza kuwa Hotel lakini wakawa wamewekeana misingi tu kwamba pesa isiyozidi kiasi fulani inaweza kulipwa cash kwa mhasibu, na bado ikawa Hotel. Hotels zingine zimeweka mikakatii ya kuwasaidia locals kuuza bidhaa zao kirahisi hotelini ili nao wanufaike na uwepo wa hotel maeneo yao, na wanalipwa cash, hilo halidisqualify hotel kuitwa hotel!! Kikubwa cha msingi ni huyu bwana kama anataka atambulike na akopesheke kirahisi kwenye taasisi za fedha anatakiwa arasimishe biashara yake.
Nimesema HOTELI niko mwaka wa tatu sasa. Rene Jr acha mawazo potofu... hivi kwanini Watz tuko hivi tunapenda kudhaniadhania tu... humu kweli kuna great thinker? Hii shida sana. Next time nitafikiria mara mbilimbili kuleta hoja za maana humu.
 
Nadhani haujanielewa tu, nilikuwa namjibu huyo jamaa aliyesema Hotel hawawezi kulipa cash mkononi itakuwa Guest. BTW, hata mimi nafanya kazi na Hotels kadhaa mkuu, japo kwa biashara yofauti. Nina kampuni ya Safety and Security, mara ya mwisho technician wangu amepewa 1.8M na Hotel moja Z'bar, cash mkononi baada tu ya kukabidhi kazi!! Nachomaanisha kurasimisha biashara ni kusajili Brela, TRA na mamlaka zingine husika, then unafungua akaunti ya kampuni Bannk, namna hiyo itakuwa rahisi wao kukupa mkopo kwa sababu mzunguko wako wa pesa unajulikana.
 
Nawashukuru wote kwa michango yenu. Niwatakie kila la heri.
 
Nyumba ninayo ila inatambulika na serikali ya mtaa. kiwanja kingine ninacho pia kinatambulika na serikali ya mtaa. Basi.
wewe bishara yako ndogo, anza kuomba mkopo kidogo then unapanda. anza kuomba 15 mln. lakini yawezekana uwezo wako wa kuserve hela katika account sio mkubwa. nenda NMB au CRDB jamaa hawana shida.
 
Kama biashara umerasimisha,wangekupa hata 3/4 ya mkopo
 
Ni nani aliekwambia real estate haikopesheki kwa sababu tu haina certificate of right of occupancy?

Nitafute nikufanyie Valuation/property appraisal ya nyumba yako uchukue mortage ufanye biashara zako,,na hata ungekua na nyumba isiyo na thamani ya kupata loan amount unayoitaka wewe unaweza ku pledge na hiyo gari (kutop up) kuongeza thamani ya collateral ili uongeze loan amount unayoweza kukopeshwa na benki
 
Uchumi wa nchi yetu upo illegular sana,mtu aliyejenga nyumba mpaka ikaisha hatakiwa kukosa mkopo angalau 50% ya value ya nyumba yake(hii kitu benki wanaiitaga loan to value ratio)
Huyu Mtu kwa wastani ka commit say 30 to 40 millions at total cost ya kiwanja to completion ya nyumba(kwa nyumba ya kawaida ya kuishi)huyu anatakiwa, bila kujali ni residential or anafanyia biashara through that property, anatakiwa awe na advantage ya malazi ya uhakika or apangishe kwa makazi or biashara ili agenerate profit au hata vyote viwili(in case ni residential cum commercial property) NA at the same time nyumba ndo most reliable collateral duniani so far(labda na govt bonds) na hivyo awe anaweza kukopea nyumba hiyo hiyo apate capital ya kufanyia shughuli nyingine

Maeneo ya kimara na mengine mengi sanaaa hapa tz yana challenge ya kutokuwa planned wala kutokupimwa(hii ni kazi ya serikali ,,ee Mungu saidia kuivusha hii nchi yetu)vinginevyo mtu mwenye nyumba nzuri tena hapa hapa dar sehemu kama kimara,na mwenye biashara halali yenye records nzuri kama alivyosema mleta mada hatakiwi awe anahangaika kuanzisha thread za kutafuta namna ya kupata mikopo ya kuboresha biashara yake,,benki ndo zilitakiwa zimtafute zim email kuwa 'ndugu unakopesheka,tunaomba tukuhudumie lakini hapa tz ni habari tofauti
 
Nawashukuru wote kwa michango yenu. Niwatakie kila la heri.

Ni nani aliekwambia real estate haikopesheki kwa sababu tu haina certificate of right of occupancy?

Nitafute nikufanyie Valuation/property appraisal ya nyumba yako uchukue mortage ufanye biashara zako,,na hata ungekua na nyumba isiyo na thamani ya kupata loan amount unayoitaka wewe unaweza ku pledge na hiyo gari (kutop up) kuongeza thamani ya collateral ili uongeze loan amount unayoweza kukopeshwa na benki
 
Issue sio kutambulika..,zina HATI hivi vitu mkuu

Sio lazima uwe na hati mkuu,,kuna kitu kinaitwa residential permit(kibali cha makazi) vinatolewa kwa maeneo ambayo hayajapimwa but watu wameshayaendeleza(kwa kujenga nyumba za kuishi specifically)

Hicho kibali cha makazi kinatosha kuchukulia mkopo
 
Back
Top Bottom