Ninaposema Mwafrika kapunjwa akili na Mungu kwa makusudi kabisa muwe mnaelewa. Rejea ajali ya ndege Bukoba 06/11/2022

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari

Mimi nitazungumzia vitu vichache tu kati ya vingi vilivyojitokeza jana ambavyo vinaonyesha ufinyu wa akili wa viongozi wetu ambao ndio wanawakilisha uhalisia wa wananchi.

1. Ziwa Victoria pamoja na ukubwa wake na umuhimu wake kiuchumi serikali haijaweka boti angalau 4 za dharura kwaajili ya kufanya uokoaji na dharura.

2. Kuajiri kwa uchache Askari na maafisa wa jeshi la zimamoto na uokoaji pamoja na kuwapa vitendea kazi vichache . Jeshi la zimamoto na uokoaji lina watumishi wachache sana na vitendea kazi pia vichache. Hakuna KITUO CHA jeshi la zimamoto na uokoaji kando ya ziwa ili kudeal na dharura za ziwani.

3. Viongozi haraka wamekimbilia kutoa majibu ya sababu ya ajali ile ndani ya masaa machache ili kulinda ugali wao. Ni wazi Mwafrika kakosa utu na ni mbinafsi asiyekubali kuachia nafasi.

Maelfu wanavushwa na vivuko hapa Tanzania kila siku huku pembeni kuna kiboti kidogo cha uokoaji kinachoweza kuokoa watu 10-20 huku kivuko kina maelfu ya abiria. Hili nalo muende mkalitizame. Na ajabu zaidi kiboti hicho kidogo cha uokoaji kimepark pembeni hakina hata habari.
 
Mimi lawama zote nawarushia CCM maana ndiyo Serikali inayoongoza nchi.
Serikali ya CCM inaona ma Toyota VX V8 ni muhimu kuliko uhai wa mwananchi.

Kiongozi wa CCM anakurupuka na matamko ya kisiasa, aache watu wa plane crash investigation wafanye kazi yao.

Hii nchi msishangae kusikia Black box imeibiwa ili tu kufanya uchunguzi wa kitaalamu usifanyike kumlinda PM na kauli yake asije akaumbuka.
 
Hii ajali ukiangalia kwa upana na marefu yake. Ni ajali yakukosa uwajibikaji. Yani tumerudi kule tumetoka. Jiulize angekuwa hai Mzee Magu.... End
Ni kweli mkuu Magu angekuwa hai angeruka kama spider-man toka Chato akaidaka ndege juu kwa juu akaiweka pale airport BK safi kama alivyookoa watu pale Ukerewe mpaka hakufa mtu hata mmoja au hapo vipi sukuma gang mwenzangu
 
Mimi mwenyewe nilimshangaa Waziri Mkuu kuanza kutoa majibu ya ajali ya ndege wakati watu hawajaokolewa. Anasema kwanini ndege imeanguka kama vile ilikuwa inapata, hakujua kama mbele ya kichwa cha ndege kimekatika. Police, Zimamoto na jeshi wamekaa pembeni wanashangaa, baada ya kufanya kazi zao za Kutoa Usalama na uokozi baada ya kuwajibika, wamewaachia wavuvi wanaojua kuvua samaki wafanye kazi za kiuokozi.

Sasa hivi walinda Usalama karibia wote wanachojua ni kufika eneo la ajali na kukaa pembeni huku wakipiga picha na kutumiana, halafu wanawaachia wananchi ndio wafanye kila kitu. Na hili tatizo ni la awamu zote za uongozi wa nchi hii.
 
Ni kweli mkuu Magu angekuwa hai angeruka kama spider-man toka chato akaidaka ndege juu kwa juu akaiweka pale airport BK safi kama alivyookoa watu pale Ukerewe mpka hakufa mtu hata mmoja au hapo vip sukuma gang mwenzangu
Hawa wenzetu akili zao ni finyu zaidi.
Kila kitu angekuwa Magu.
Bahati nzuri Mimi Magufuli namfahamu kwa sura zote mbili.
Kama mtumishi wa Serikali na watu
Namfahamu pia kwa maisha ya kifamilia
Hawa wanaoshoboka nao hawajui chochote kuhusu Magu
 
Kwahiyo kuokoa majanga yanayotokea baharini pamoja na ziwani ni jukumu la nani?

Tafadhali msichanganye kitengo cha Jeshi cha Navy na kitengo cha Jeshi la Zimamoto na Uokozi...Ni vitengo viwili tofauti na vipo wizara mbili tofauti...

Mara nyingi Jeshi la JWTZ hushirikishwa kwenye uokozi wa mambo ya kiraia, kwa sababu wao hupitia mafunzo ya uokozi katika aina tofauti tofauti za majanga na wana divers pia lakini hilo sio jukumu lao la msingi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…