Ninasaidia wafanyabiashara waliopo mbali na Dar es salaam

Ninasaidia wafanyabiashara waliopo mbali na Dar es salaam

mapozzi

Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
75
Reaction score
52
Habari za leo wakuu
Mimi ni kijana mkazi wa Dar es salaam. Nimekuwa nikiwasaidia wafanyabiashara waliopo mbali na Dar es salaam katika kuwanunulia bidhaa kwenye maduka ya jumla yaliopo hapa Dar. Hivyo haimlazimu mtu kusafiri kutoka mikoa ya mbali kuja Dar kufunga mzigo, ambapo utakuta faida kidogo iliyokuwa aipate inakuwa ndogo zaidi kutokana na kuingia gharama za usafiri na malazi kwa kuja yeye mwenyewe. Ninawatumia mizigo kwa njia ya bus au lori kutegemeana na mteja atakavyochagua.
Ninafanya kazi hii kwa uaminifu mkubwa.

Bidhaa ambazo nimekuwa nikihusika nazo ni vyombo vya nyumbani/jikoni, viatu, T-shirts na Stationery etc

Commission ni maelewano

Kwa anayehitaji huduma yangu unaweza kunitumia msg pm au ukapiga simu no 0767407674
Karibuni
 
Unataka kusema commision yako itakua ndogo kulinganisha na gharama za usafiri malazi na chakula? Na una uhakika gani wanapata faida ndogo?
 
Faida kidogo penye usalama wa mataji ni Bora kuliko faida kubwa Ila usalama wa mtaji ni mdogo!! Wazo ni zuri Ila changamoto ni uaminifu .
 
Unataka kusema commision yako itakua ndogo kulinganisha na gharama za usafiri malazi na chakula? Na una uhakika gani wanapata faida ndogo?
Kwa wanaofanyabiashara wanaelewa pale anapoona gharama ya kufuata mzigo ni kubwa akilinganisha na gharama ya kuagizia mtu, anafanya maamuzi yanayompa yeye unafuu. Karibu
 
Faida kidogo penye usalama wa mataji ni Bora kuliko faida kubwa Ila usalama wa mtaji ni mdogo!! Wazo ni zuri Ila changamoto ni uaminifu .
Ni kweli usemacho usalama wa mtaji ni jambo la kuzingatia. Kwa kuwa ninaipenda kazi yangu Uaminifu ndio kanuni namba moja niliyojiwekea. Ukihitaji vielelezo kunihusu utavipata. Karibu
 
Kwa wanaofanyabiashara wanaelewa pale anapoona gharama ya kufuata mzigo ni kubwa akilinganisha na gharama ya kuagizia mtu, anafanya maamuzi yanayompa yeye unafuu. Karibu
Mh na gharama za kupenda virahisi kwa mfanya biashara anakua ashapigia mahesabu
 
Back
Top Bottom