Usichukue mikopo ya muda mrefu chukua ya miaka miwili then ikiisha. Ukope tena
Haya ni mfano wa mawazo au maoni ya watu wenye roho mbaya,roho ambazo sio za kibiashara roho za kimasikini(sikushambulii wewe mkuu samahani ila nashambulia mawazo uliyoyatoa)
Yani tunashuri mtu asichukue mkopo wa muda mrefu ati kwa sababu benki watafaidika sana.
Badala yake tunashsuri watu wakope kidogo kidogo.
Alafu watu wenye mawazo kama haya ndio hukopa na kwenda kujengea hivyo kwao wanaona ni mawazo bora sana kuwashauri watu wakope taratibu wakati kiuhalisia hayo sio mawazo bora.
Huyu kama ni mwajiriwa mkopo wa muda mrefu kwake sio tatizo kwa sababu anakTwa kqenye mshahara.
MKuu sio busara kumshauri mtu akope kidogo kidogo kwa sababu unamfanya awe mteja wa mikopo.
Kwa sababu ni bora mkopo wa muda mrefu utakaokukwamua kimaisha moja kwa moja,kuliko mkopo wa muda mfupi utakaokufanya uendelee kuishi maisha ya hali ya chini.
wengine wanashauri eti aweke akiba kwa hiyo miaka 9 then atapata hiyo 50M.
.
Watu wanakimbizana na muda,mtu anataka hiyo miaka 9 ya mbele awe hatua fulani.
Akiweka akiba maana yake miaka hiyo 9 ndio atakuwa anaanza mchakato wa kuitafuta ile hatua ambayo angeianza hivi leo 2023 badala yake akiweka akiba tunamlazimisha mchakato wake auanze 2032,does it make sense kweli muda huu wote alioutupa kwa kuweka akiba ambayo angeliipata kwa mkopo ?
WAajiriwa ambao hukopa kupitia mishahara yao wanatakiwa kupewa ushauri wa peke yao tofauti na wafanya biashara ambao hukopa na kurejesha benki kupitia faida ama mzunguko wa biashara.
Muajiriwa kukopa mkopo hata wa miaka 20 sio hasara kwake maadamu mkopo huo ataenda kuupigania na kufanyia mambo yenye tija kwake.
Muajiriwa anaweza akakopa mkopo wa miaka 7 na akautafunia kuku wote na bado aswe na stress na madeni ya benki kwa sababu mzigo unakatwa kwenye mshahara.
Alafu watu wengi wanahofia riba ya benki kwamba wanapata pesa nyingi,wewe kama ni miwekezaji angalia utapata ngapi na sio unaangalia yeye benki atapata ngapi.
Kuna mdau mmoja alichukua 30M sehemu kwa miaka mi4 marejesho akaenda kupiga dili kama miezi mi3 hivi akapiga faida kama ya 20M jumla ikawa 50M.
Aliwarudishia benki pesa yao ndani ya miezi mi2 then akabaki na profit ya 20M ya bure bure,sijui mnaona faida ya mikopo kama una oshu za uhakika ?
Anaweza kuchukua hiyo 50M then ndani ya miaka mi2 tu akapiga 200M,wakati huo benki wao ndani ya miaka 9 ndio wanapata hiyo 40M ya riba,nani atakuwa mjanja ?
So watu wanaangalia maokoto kwa upande wao tu,usianze kuweka wivu kwamba mwenzio stspata kikubwa.