Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Habari za asubuhi wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
Usichukue mikopo ya muda mrefu chukua ya miaka miwili then ikiisha. Ukope tena
 
Usichukue mikopo ya muda mrefu chukua ya miaka miwili then ikiisha. Ukope tena
Haya ni mfano wa mawazo au maoni ya watu wenye roho mbaya,roho ambazo sio za kibiashara roho za kimasikini(sikushambulii wewe mkuu samahani ila nashambulia mawazo uliyoyatoa)

Yani tunashuri mtu asichukue mkopo wa muda mrefu ati kwa sababu benki watafaidika sana.

Badala yake tunashsuri watu wakope kidogo kidogo.

Alafu watu wenye mawazo kama haya ndio hukopa na kwenda kujengea hivyo kwao wanaona ni mawazo bora sana kuwashauri watu wakope taratibu wakati kiuhalisia hayo sio mawazo bora.

Huyu kama ni mwajiriwa mkopo wa muda mrefu kwake sio tatizo kwa sababu anakTwa kqenye mshahara.

MKuu sio busara kumshauri mtu akope kidogo kidogo kwa sababu unamfanya awe mteja wa mikopo.

Kwa sababu ni bora mkopo wa muda mrefu utakaokukwamua kimaisha moja kwa moja,kuliko mkopo wa muda mfupi utakaokufanya uendelee kuishi maisha ya hali ya chini.

wengine wanashauri eti aweke akiba kwa hiyo miaka 9 then atapata hiyo 50M.
.
Watu wanakimbizana na muda,mtu anataka hiyo miaka 9 ya mbele awe hatua fulani.

Akiweka akiba maana yake miaka hiyo 9 ndio atakuwa anaanza mchakato wa kuitafuta ile hatua ambayo angeianza hivi leo 2023 badala yake akiweka akiba tunamlazimisha mchakato wake auanze 2032,does it make sense kweli muda huu wote alioutupa kwa kuweka akiba ambayo angeliipata kwa mkopo ?

WAajiriwa ambao hukopa kupitia mishahara yao wanatakiwa kupewa ushauri wa peke yao tofauti na wafanya biashara ambao hukopa na kurejesha benki kupitia faida ama mzunguko wa biashara.

Muajiriwa kukopa mkopo hata wa miaka 20 sio hasara kwake maadamu mkopo huo ataenda kuupigania na kufanyia mambo yenye tija kwake.

Muajiriwa anaweza akakopa mkopo wa miaka 7 na akautafunia kuku wote na bado aswe na stress na madeni ya benki kwa sababu mzigo unakatwa kwenye mshahara.

Alafu watu wengi wanahofia riba ya benki kwamba wanapata pesa nyingi,wewe kama ni miwekezaji angalia utapata ngapi na sio unaangalia yeye benki atapata ngapi.

Kuna mdau mmoja alichukua 30M sehemu kwa miaka mi4 marejesho akaenda kupiga dili kama miezi mi3 hivi akapiga faida kama ya 20M jumla ikawa 50M.

Aliwarudishia benki pesa yao ndani ya miezi mi2 then akabaki na profit ya 20M ya bure bure,sijui mnaona faida ya mikopo kama una oshu za uhakika ?

Anaweza kuchukua hiyo 50M then ndani ya miaka mi2 tu akapiga 200M,wakati huo benki wao ndani ya miaka 9 ndio wanapata hiyo 40M ya riba,nani atakuwa mjanja ?

So watu wanaangalia maokoto kwa upande wao tu,usianze kuweka wivu kwamba mwenzio stspata kikubwa.
 
Sitaweka bond fund Mkuu nitaweka liquid fund na jikimu....narely kwenye compounding effect nitakaa pesa zikae zijizalishe Kwa miaka 30

Nimekuelewa, utaziweka kwa mda mrefu.

Ila kwanini usifanye hivi;

Hiyo amount ambayo unapanga kuirejesha benki kila mwezi kwa miaka tisa, badala ya kuchukua mkopo na uipeleke benki, basi kila mwezi iweke UTT, naamini ukifanya hivyo ndani ya hiyo miaka 9, hela yako ya UTT inaweza kufika zaidi ya 50M plus na faida juu. Halafu baada ya hapo ndo uiache kwa miaka kadhaa kwa mfano miaka 21 izidi kujizalisha.

Kwa hivyo utakuwa umesave ile riba ambayo ulibidi kuipa benki, na utakuwa umeokoa hela nyinigi na hasa kuitajirisha benki kirahisi.

Ni mawazo yangu tu lakini Mkuu.
 
Kwa hivyo utakuwa umesave ile riba ambayo ulibidi kuipa benki, na utakuwa umeokoa hela nyinigi na hasa kuitajirisha benki kirahisi.
Kwa hiyo akishakwepa kuinufaisha benki yeye anapata faida gani mkuu 😀 ?

AU ni roho zetu zimetutawala na ile hali ya bora tukose sote tu mkuu.

Haya maisha unatakiwa uangalie wewe unapata nini na sio benki anapats nini.

Ukiangalia hivyo hautanunua hata simu inayotoka china maana wanapiga faida nzuri sana kuliko wewe unayenunua.
 
Huyu jamaa asipoangalia atakufa maskini. Yani uchukue mkopo 50m kwa miaka Tisa kwa return ya 833k kila mwezi the ukaweke UTT upewe 400k? What kind of investment? Yani uteseke miaka 9 Ili 50m ndo iwe mali yako😀😀 Bora ufanye biashara Ili update rejesho na faida nzuri. Any way akili ni nywele!
 
Kwa moyo wa dhati kabisa napenda kuwashukuru nyote mlionisapot kimawazo kupitia Uzi huu....nimeamua kuchukua huo mkopo Kwa moyo mkunjufu mengine Mungu atanisaidia
Kanyaga twende kiongozi tumechelewa mnoo.
 
Mil 90 Kwa Miaka 9 Unarudisha Mil 10 Kila Mwaka Ambayo Kwa Mwez Ni Kama Lak 8 Hv Utatakiwa Kurejesha. Chukua Hyo Mil 50 Tafuta Ist Au Passo Za Mil 7,8 Mpaka 9 Chukua Gari 6 Zisajili Na Bolt,uber Tafuta Madereva Waaminifu Wawe Wanakuletea Kwa Siku Kila Mmoja Elfu 30 Kama Faida Kwa Hzo Gari Sita, Kwa Siku Utaingiza Laki Na 80 Ambayo Kwa Mwezi Una Kama Mil 5 Na Nusu,rudisha Marejesho Kila Mwez Mil 2 Deni Unalimaliza Mapema Kabla Hata Ya Hyo Miaka 9.Za Kuambiwa Changanya Na Zako Ila Sikushauri Uchukue Mkopo Laana Ya Dhambi Ya Riba Haiwajawah Kumuacha Mtu
 
Habari za asubuhi wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
Security yako huo mkopo ni nini Ili niweze kukushauri vizuri?

Ni mshahara wako au ni Hati ya nyumba?
 
Nakushauri uachane na huo mkopo. Unaweza kufikiri 50m, ni pesa nyingi, lakini kwa hali ya uchumi ilivyo sasa, ni pesa kidogo sana.

Badala yake save benki hiyo pesa ambayo ungelipia huo mkopo. Iweke kwenye fixed deposit account kwa miaka mitano. Tanzania commercial bank

Baada ya miaka mitano utakuwa umesave 50m, ukijumlisha na riba inaweza kufika 70m
Achana na kusave pesa bank bora aweke UTT
 
ushauri wa bure ndugu yangu,kukopa harusi kulipa ni matanga miaka 9 ni mingi mnoo kama unauwezo dunduliza pesa yako,nnamkopo wa miaka 4 naliona joto lake nilikopa nikaekeza ktk biashara,plani ikaenda mrama nalipa uku nnaumia
Ukweli mchungu sema nini muache achukue maana ni kama kashaamua halafu iko siku atakuja hapa kuusoma tena huu uzi kwa uchungu [emoji23][emoji23]
 
Mkuu ulishavuta ndinga?..
Vuta ndinga kali ule maisha ili maumivu uyapunguzie kweny mbususu
 
Angalia Bank nyingine, yaani wakupe 50m uwatengenezee Faida ya 40m kwa miaka 9 sio sawa.
 
Habari za asubuhi wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
Huwezi kutajirika na hela benki ,utapoteza wewe
 
Back
Top Bottom