Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Habar za asubuh wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
16% ni kubwa ila kwakuwa una lipa kwa muda mrefu ni sawa.
Wao wananunua BOT BOND , wanapata faida ya milioni 125
 
Sasa mzee aende halmashauri kwenye mambo ya vikundi tena ?

Halafu nionyeshe taasisi yeyote ya fedha au benk wanakotoa riba nzuri zaidi ya hio ya 16% kwa mkopo wa miaka 9 hapa Tz,
Mimi bado sijaelewa hiyo riba ya 16% inapatikana vipi.
Kama mkopo ni 50M, inakuwaje interest ya 40M kuwa 16%?

Nielewesheni jamani
 
Mimi bado sijaelewa hiyo riba ya 16% inapatikana vipi.
Kama mkopo ni 50M, inakuwaje interest ya 40M kuwa 16%?

Nielewesheni jamani
Eddo nakupongeza na nlitaka niache watu wanaofikiri wanajua wabaki na ujinga wao.
Fomu za mikopo ya benki huwa zina clause ambazo zina maandishi madogo sana, huko kuna interest na compaunding interest.
Usijidanganye kuwa mkopo wa 50 M utalipa only 16%.
Kuna underlying charges nyingi sana mpaka legal fee, processing fee, insurance unaweka wewe na hapo afisa mikopo anataka laki 5.
Sikukatisheni tamaa ila huku mahakamani kila siku nyumba zenu zinauzwa hamkomi.
Ukitaka kukopa kapate ushauri wa wanasheria.
 
Mimi bado sijaelewa hiyo riba ya 16% inapatikana vipi.
Kama mkopo ni 50M, inakuwaje interest ya 40M kuwa 16%?

Nielewesheni jamani
Wew bana,
Hio 16% ni kwa mwaka mmoja tu, endapo angechukua mkopo wa mwaka mmoja ndio hesabu ingekuja hio unayowaza wew,
Ila kwa kuwa ni miaka 9 hapo hesabu nyingi zinaingia katikati mambo ya reducing balance na ndugu zake ndo wataleta hio riba ya juu,
Japo kimahesabu ilibidi ije 72M sijui yeye kafanyaje kupata hio 90M
 
Back
Top Bottom