Ninataka kuwadai Halotel fidia kwa usumbufu walionipatia

Ninataka kuwadai Halotel fidia kwa usumbufu walionipatia

Blogaboy

Member
Joined
Jun 21, 2020
Posts
13
Reaction score
9
Wakuu kwema?

Nina shida hapa imenitokea, mnamo tarehe 23 nilituma pesa kama Tshs 500k kwenda namba ya voda tokea halotel, ila nikajagundua nimekosea namba,

Nikawapigia halopesa, wakaniambia nisubiri masaa 72 pesa itarudi,

Nikawa mpole nikasubiri, masaa yamefika 100,pesa haijarudi,

Nikawapigia tena, wakaniambia nisubiri tena masaa 72 pesa yangu, haijashughulikiwa ,maana yake mpaka tar 1.

Nikawauliza swali, endapo niliemtumia ataitoa,Si nitakosa haki? Wakanijibu niwe mvumilivu,

Sasa,

Naomba mnishauri nataka kuwapeleka kwa mwaka sheria na TCRA nataka wanilipe pesa yangu na nidai fidia,

Naombeni ushauri wenu,nipitie njia gani!
 
Jiuluze mwenye makosa nani? Kabla ya kutumia kulikuwa na option ya kuthibitisha na ukabonyeza moja kuthibitisha kutuma fedha kwa maana ulihakiki mtumiwaji.
 
Wakuu kwema?

Nina shida hapa imenitokea, mnamo tarehe 23 nilituma pesa kama tshs 500k kwenda namba ya voda tokea halotel, ila nikajagundua nimekosea namba,

Nikawapigia halopesa,wakaniambia nisubiri masaa 72 pesa itarudi,

Nikawa mpole nikasubiri, masaa yamefika 100,pesa haijarudi,

Nikawapigia tena,wakaniambia nisubiri tena masaa 72 pesa yangu, haijashughulikiwa ,maana yake mpaka tar 1.

Nikawauliza swali, endapo niliemtumia ataitoa,Si nitakosa haki? Wakanijibu niwe mvumilivu,

Sasa,

Naomba mnishauri nataka kuwapeleka kwa mwaka sheria na Tcra nataka wanilipe pesa yangu na nidai fidia,

Naombeni ushauri wenu,nipitie njia gani!
HALOLET Bwana noma kweli
 
Kwa maelezo yako ukiwapeleka mahakamani wewe ndio utakutwa na hatia

mitandao yote kabla ya kutuma pesa inaleta jina la unayemtumia na wewe unathibitisha kuwa ni yeye ninayemtumia
 
Kwa maelezo yako ukiwapeleka mahakamani wewe ndio utakutwa na hatia

mitandao yote kabla ya kutuma pesa inaleta jina la unayemtumia na wewe unathibitisha kuwa ni yeye ninayemtumia
Basi,walitakiwa kukataa kunihudumia..,au wangetoa hiyo huduma

Bro,inaonekana upo mbali sana na swala la digital networking, subiria vyombo vya habari
 
Kwa uandishi wako nadiriki kusema HUSTAHILI KULIPWA HATA 100, rudi darasani kwanza
 
Basi,walitakiwa kukataa kunihudumia..,au wangetoa hiyo huduma

Bro,inaonekana upo mbali sana na swala la digital networking, subiria vyombo vya habari
We uliye karibu na digital networking, UMESHINDWA KUTHIBITISHA JINA LA MTUMIWAJI KABLA HUJASEMA OK au SEND..!?
 
Back
Top Bottom