Ninataka nimuache msichana kwa faida ya maisha yake

Ninataka nimuache msichana kwa faida ya maisha yake

Ruble

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
845
Reaction score
1,579
Wakuu heshima kwenu,

Bila kupoteza muda niwe straight. Nipo kwenye mahusiano na msichana ambaye kimsingi ana maadili, mzuri wa sura na maumbile yake, tabia zake, anajua mapishi, ana akili kwa ufupi ana sifa zote za wife material.

Sasa huyu binti hivi karibuni amepata sana bahati za watu ambao wapo tayari kumuoa. Ni watu ambao nikiwaangalia kiuhalisia wanajiweza kihali. Huyu binti kwao ni maisha ya chini. Nilimpenda na niseme ukweli nampenda sana. Tatizo ni maisha yangu. Bado sioni dira na muelekeo wa kufanikiwa. Kila nikijitahidi vikwazo hivi hapa.

Niliahidi Mungu akipenda ningemuoa, lakini kila leo matumaini ya hali yangu ya kimaisha bado inagoma. Nilimueleza akubali kuolewa kwa kuwa wanaume wanaomtaka ni watu wenye staha zao na wanamuendea kwa uadilifu basi akubali aolewe asitirike. Maana mimi nikiangalia naona ninazidi kumpotezea muda wake, si kwamba nafanya hivi sababu simpendi la hasha! Ni ndoto zangu za maisha na mipango kuwa migumu. Sioni dalili, kwanini niendelee kumpa matumaini yasiyokuwapo? Nilimueleza lakini naona mwenzangu anakua mkali kama mbogo.

Kuna jamaa mmoja mpaka nilimueleza, kaka kama unampenda huyu binti naomba usimchezee umuoe kweli, jamaa mpaka leo ananisumbua maana nilijitambulisha kama kaka yake. Jamaa yupo serious na anaonyesha nia ya dhati juu ya kumuoa huyu binti.

Ushauri tafadhali ninafikiria kumuacha kwa nguvu lengo ikiwa ni kwa faida yake. Je, ushauri wakuu mnaonaje juu ya hili?

NB: Nimejifunza ndoto nyingi za vijana juu ya wasichana au wanawake waliowapenda zinakatishwa kutokana na kutotimia kwa ndoto za vijana wengi huku umri ukiwatupa mkono, hapo hapo familia nayo ikikusimanga. Ni msongo wa mawazo juu ya msongo.
 
Kwani tatzo nini huna hela ya kumtunza.

Mi ushauri wangu oa huyo mchuchu. Kama kweli ana sifa ulizozitaja hapo juu. Weka ndani huyo. Atakusaidia hata kwenye upambanaji wa kimaisha.

Hao jamaa wanaomfuata usikute ni mafisi waliojivika ngozi ya kondoo.
 
20220225_171338.jpg
 
Kwani tatzo nini huna hela ya kumtunza.

Mi ushauri wangu oa huyo mchuchu. Kama kweli ana sifa ulizozitaja hapo juu. Weka ndani huyo. Atakusaidia hata kwenye upambanaji wa kimaisha.


Hao jamaa wanaomfuata usikute ni mafisi waliojivika ngozi ya kondoo.
Mkuu mimi mwenyewe kujitunza bado ni mtihani. Kumhudumia ni kama bahati nasibu.
Kiufupi uwezo wa kumuoa sina mkuu na sioni hata dalili za kuwa na huo uwezo.
 
Kama yeye pe amekubaliana na hali usimuache kaa ishi naye amini 3 years mbele hamtokua hapo mlipo. Jishughulishe huku yeye akitambua una hali gani utakua na amani sana.

Nimeshuhudia mtu na mke wanaamani ila kula ya familia yao kuanzia watoto ni changamoto. Ila wao wako na furaha wanaongea na kupeana pole ya majukumu
 
Wakuu heshima kwenu,

Bila kupoteza muda niwe straight.
Nipo kwenye mahusiano na msichana ambaye kimsingi ana maadili, mzuri wa sura na maumbile yake, tabia zake, anajua mapishi, ana akili kwa ufupi ana sifa zote za wife material.
Kuna watu wanajuta sasa kwa kuacha mwanamke kama huyo.
 
MUNGU akubaliki Sana,
Niombee na Mimi basi niwe na moyo Kama wako mkuu, maana nmenasa kwelikweli[emoji4]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wakuu heshima kwenu,

Bila kupoteza muda niwe straight.
Nipo kwenye mahusiano na msichana ambaye kimsingi ana maadili, mzuri wa sura na maumbile yake, tabia zake, anajua mapishi, ana akili kwa ufupi ana sifa zote za wife material.
Daahh,hii Hali unayoipitia namm naipitia the same way,Ila tatizo mm nimezaa nae,huyo binti nimeahidi kumsauport Ila I'm not ready Kwa marriage kwasababu ya masuala yakutimiza ndoto binafsi,nimemueleza kuhusu kua tayari kuolewa nawatu wanaoonesha Nia nayy ili asitirike kwasababu yy Yuko Tyr kuanzisha maisha
 
Back
Top Bottom