Wakuu heshima kwenu,
Bila kupoteza muda niwe straight. Nipo kwenye mahusiano na msichana ambaye kimsingi ana maadili, mzuri wa sura na maumbile yake, tabia zake, anajua mapishi, ana akili kwa ufupi ana sifa zote za wife material.
Sasa huyu binti hivi karibuni amepata sana bahati za watu ambao wapo tayari kumuoa. Ni watu ambao nikiwaangalia kiuhalisia wanajiweza kihali. Huyu binti kwao ni maisha ya chini. Nilimpenda na niseme ukweli nampenda sana. Tatizo ni maisha yangu. Bado sioni dira na muelekeo wa kufanikiwa. Kila nikijitahidi vikwazo hivi hapa.
Niliahidi Mungu akipenda ningemuoa, lakini kila leo matumaini ya hali yangu ya kimaisha bado inagoma. Nilimueleza akubali kuolewa kwa kuwa wanaume wanaomtaka ni watu wenye staha zao na wanamuendea kwa uadilifu basi akubali aolewe asitirike. Maana mimi nikiangalia naona ninazidi kumpotezea muda wake, si kwamba nafanya hivi sababu simpendi la hasha! Ni ndoto zangu za maisha na mipango kuwa migumu. Sioni dalili, kwanini niendelee kumpa matumaini yasiyokuwapo? Nilimueleza lakini naona mwenzangu anakua mkali kama mbogo.
Kuna jamaa mmoja mpaka nilimueleza, kaka kama unampenda huyu binti naomba usimchezee umuoe kweli, jamaa mpaka leo ananisumbua maana nilijitambulisha kama kaka yake. Jamaa yupo serious na anaonyesha nia ya dhati juu ya kumuoa huyu binti.
Ushauri tafadhali ninafikiria kumuacha kwa nguvu lengo ikiwa ni kwa faida yake. Je, ushauri wakuu mnaonaje juu ya hili?
NB: Nimejifunza ndoto nyingi za vijana juu ya wasichana au wanawake waliowapenda zinakatishwa kutokana na kutotimia kwa ndoto za vijana wengi huku umri ukiwatupa mkono, hapo hapo familia nayo ikikusimanga. Ni msongo wa mawazo juu ya msongo.